Uongozi wa mabingwa wa
ligi kuu soka ya Vodacom Tanzania Bara Dar Es Salaam Young African
imemtambulisha rasmi mshambuliaji MRISHO HALFAN NGASA kuwa mchezaji wao
kwa ajili wa msimu ujao wa ligi hiyo. NGASA alikuwa anacheza kwa mkopo kwa wapinzani wa jadi wa Yanga , Simba akitokea katika Klabu ya Azam ya Jijini Dar Es Salaam. Akimtambulisha
rasmi mbele ya Waandishi wa Habari hii leo Makao Makuu ya Klabu hiyo
Katibu wa Yanga LAWRANCE MWALUSAKO amesema wamefikia hatua hiyo baada ya
kufanya mazungumza na mshambuliaji na kuamua kurejea katika Klabu yake
hiyo ya zamani. MWALUSAKO amesema NGASA ambaye amekiri kuwa na mahaba ya dhati na Klabu hiyo ameingia mkataba wa miaka miwili. Akizungumza
baada ya kutambulishwa rasmi NGASA amesema anamshukuru Mungu kwa
kumwezesha kurejea katika Klabu yake hiyo ya zamani ambaye amesema ni
kama Nyumbani kutokana na mapenzi aliyonayo. Mshambuliaji
huyo pia amewataka mashabiki wake kuendelea kumuunga mkono na anaimani
kuwa atafanya vizuri katika Klabu hiyo ambayo amewahi kuichezea huko
nyuma.
Monday, May 20, 2013
Sunday, May 19, 2013
MOKOCHA 20 WANAOFUNDISHA SHULE ZA SECONDARI WAPEWA MAFUNZO.
MAKOCHA 20 wanaofundisha soka shule za sekondari na msingi sambamba na wale wa timu za mitaani mkoani Rukwa wamepewa mafunzo ya awali ya ukocha ili kuwaongezea ujuzi na ufanisi.
Mafunzo hayo ambayo yanafanywa na mkufunzi kutoka Chama cha Makocha Tanzania (Tafca), George Komba, yanafadhiliwa na Chama cha Makocha Mkoa wa Rukwa, ambako yatakuwa ya siku 12, yakishirikisha washiriki kutoka wilaya zote mkoani hapa.
Akizungumza na mwandishi wa blog hii Katibu wa Tafca Rukwa, Lusungu Kihaha ameeleza kuwa lengo ni kuwanoa makocha hao ili waweze kuzielewa kwa kina kanuni zote 17 za soka.
Ameongeza na kusema kuwa ni matarajio yake ifikapo 2013-14 kuona soka la kistaarabu likichezwa viwanjani, kwani mpira wa miguu si uwanja wa vita, bali ni kuboresha mahusiano baina ya wachezaji, pia makocha na makocha wenzao.
Katibu wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (Rurefa), Godfrey Seko, alisema kuwa mara baada ya mafunzo hayo, hakuna kocha yeyote asiye na sifa atakayeruhusiwa kuketi katika benchi la ufundi kiwanjani wakati timu yake ikicheza.
Aidha amesema ni makocha wale tu wenye cheti cha awali, ndio watakaoruhusiwa kuketi kwenye benchi la ufundi wakati timu zao zikiumana na si vinginevyo.
hata hivyo Awali akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Sumbawanga, Kevas Masawe, amewataka washiriki hao kuutumia ujuzi huo shuleni na katika timu za mitaani ili kuinua vipaji vya soka vya Mkoa wa Rukwa.
WALIMU MASHULENI WATAKIWA KUHIMIZA NIDHAMU KWA WANAFUNZI
WALIMU wa michezo katika shule za msingi, sekondari na vyuo
wametakiwa kuhamasisha suala la nidhamu kwa wanafunzi ili kuwajengea msingi
ilio bora utakaowafanya wafike mbali.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Tabora, Joyce
Ndonda, aliyekuwa mgeni rasmi katika bonanza maalumu la mchezo wa netiboli,
lililofanyika kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini humo.
Akizungumza na wanamichezo mbalimbali walioshiriki katika
bonanza hilo, Ndonda ameipongeza Chaneta Tabora kwa kuanzisha bonanza hilo na
kuwataka kuendelea na utaratibu huo, kwani ni chachu ya kukuza vipaji kwa
vijana na kuinua hamasa ya michezo.
Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Mkoa wa
Tabora, Kulwa Kavula, amesema lengo la bonanza hilo ni kuhamasisha wasichana na
wadau wengine kuupenda mchezo huo.
Hata hivyo amewaomba wadau katika halmashauri zote za Mkoa wa
Tabora kuwapa ushirikiano ili waweze kufanikisha harakati za kuinua michezo huo
nchini.
BPL YAFIKIA TAMATI MAN U, MAN CITY, CHELSEA, ARSENAL KUCHEZA UEFA.
MATOKEO BPL LEO England - Premier League (Table) | |||
18:18 | May 19 | ||
FT | Chelsea | 2 - 1 | Everton |
FT | Liverpool | 1 - 0 | Queens Park R. |
FT | Manchester C. | 2 - 3 | Norwich C. |
FT | Newcastle U. | 0 - 1 | Arsenal |
FT | Southampton | 1 - 1 | Stoke C. |
FT | Swansea C. | 0 - 3 | Fulham |
FT | Tottenham H. | 1 - 0 | Sunderland |
FT | West Bromwich A. | 5 - 5 | Manchester U. |
FT | West Ham U. | 4 - 2 | Reading |
FT | Wigan Athletic | 2 - 2 | Aston Villa |
BABA WA NEYMAE ASISITIZA MWANAE KUBAKI BRAZIL MAPAKA 2014
BABA wa mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Brazil na klabu ya Santos, Neymar kwa mara nyingine amesisitiza kuwa mwanae atabakia nchini Brazil mpaka kipindi cha majira ya kiangazi 2014. Kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu nyota huyo kutimkia klabu ya Barcelona katika kipindi cha miezi michache ijayo huku kocha wake Tito Vilanova akithibitisha kuwa mazungumzo baina ya pande hizo mbili yamefanyika. Hata hivyo baba yake Neymar amesisitiza kuwa mwanae amepanga kumaliza mkataba wake na Santos akidai kuwa kama Barcelona na Real Madrid zina mpango ya kumsajili nyota huyo basi hawana budi kusogeza mipango yao mwakani. Mzee huyo amesema mipango iliyopo ni kuona mwanae anamaliza mkataba na Santos na kama klabu hiyo ikiamua kumuuza kabla ya mkataba wake kumaliza basi wanapaswa kutoa taarifa kabla ili aweze kuzungumza na mwanae kama yuko tayari kwenda Ulaya.
ROY AKERWA NA CHELSEA, MAN CITY VS TOTTENHAM KWENA MAREKANI.

Klabu
hizi 3 zitasafiri n kuelekea Marekani kuumana zenyewe kwa wenyewe katika
Mechimbili za kirafiki huku Tottenham wakitua Visiwa vya Bahamas kucheza na
Jamaica.
ZIARA:
Mei 23: Man
City v Chelsea [St Louis]
Mei 25: Chelsea
v Man City [New York]
Mei 23: Tottenham
v Jamaica [Thomas A. Robinson National Stadium, Nassau Paradise Island,
Bahamas]
England
nayo inatarajiwa kucheza na Republic of Ireland, Uwanjani Wembley hapo Mei 29
na kisha kuruka kwenda Brazil kucheza Uwanja wa Maracana Jijini Rio De Janeiro na
Brazil hapo Juni 2.
Kikosi
cha Hodgson alichokiteua kuiwakilisha England katika Mechi hizo mbili kina
Wachezaji wanane toka Timu hizo tatu.
Chelsea
inasemekana imekubali kuwaruhusu Frank Lampard, Ashley Cole na Gary Cahill
kuondoka baada ya Mechi yao ya kwanza ya Tarehe 23 na Man City ili kurudi
London kujiunga na England.
Lakini
Hodgson amesema wao walipanga Mechi zao za Kimataifa kwa makusudi ili kuwapa
Wachezaji wote mapumziko ya Wiki moja baada ya Msimu wa Klabu zao kumalizika
kisha kuwachukua wao kwa Wiki moja na baada ya hapo kuwaachia kwenda Vakesheni
zao kabla kurudi Klabuni kwao kwa matayarisho ya Msimu mpya wa 2013/14.
Hogson
amesema Ziara hizo za Klabu zitawafanya wasafiri safari ndefu kuvuka Bahari ya
Atlantic na kurudi tena na hilo halitasaidia matayarisho yao.
Akimalizia
Hodgson alisema: “Hii ndio hali ambayo tumejikuta tunayo na hatuwezi
kulazimisha Klabu nini wafanye.”
KIKOSI
KAMILI:
MAKIPA: Ben
Foster, Joe Hart, Alex McCarthy.
MABEKI: Leighton
Baines, Gary Cahill, Ashley Cole, Phil Jagielka, Glen Johnson, Phil Jones,
Joleon Lescott, Kyle Walker.
VIUNGO: Michael
Carrick, Tom Cleverley, Frank Lampard, James Milner, Alex Oxlade-Chamberlain,
Theo Walcott.
MAFOWADI: Andy
Carroll, Jermain Defoe, Wayne Rooney, Daniel Sturridge, Danny Welbeck.
PAMBANO LA SIMBA, YANGA LAINGIZA MIL 500/-
Pambalo la watani wa jadi Simba na Yanga la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Mei 18 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa mabingwa wapya Yanga kushinda mabao 2-0 limeingiza sh. 500,390,000.
Mechi hiyo namba 180 ambayo ilikuwa kati ya saba la kuhitimisha ligi hiyo msimu wa 2012/2013 ilishuhudiwa na watazamaji 57,406 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000.
Kila klabu imepata mgawo wa sh. 123,970,927.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 76,330,677.97.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo walikuwa 19,039 na kuingiza sh. 95,195,000 wakati kile cha sh. 7,000 kiliingiza watazamaji 17,647 na kupatikana sh. 123,515,000.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 63,036,064.81, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 37,821,638.88, Kamati ya Ligi sh. 37,821,638.88, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,910,819.44 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 14,708,415.12.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Subscribe to:
Posts (Atom)