Monday, June 3, 2013

BRAZIL YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 DHIDI YA ENGLAND KATIKA MECHI YA KIRAFIKI"

Katika Mechi ya ufunguzi rasmi Uwanja wa Maracana iliyopigwa jana  kati ya wenyeji brazil na England jina rasmi  la uwanja huo kwa sasa ni Estadio Jornalista Mário Filho huko Mjini Rio De Janeiro Wenyeji Brazil walilazimishwa  sare ya kufungana Bao 2-2 na England hapo jana Usiku.

Brazil walitawala Kipindi chote cha kwanza lakini hawakupata Bao hasa kutokana na kusimama imara kwa Kipa Joe Hart.

MAGOLI:

Brazil 2
-Fred Dakika ya 57
-Paulinho 82
-England 2
- Oxlade-Chamberlain Dakika ya 67
-Rooney 79
Bao zote 4 za Mechi hiyo ziliwekwa kimiani Kipindi cha Pili na Brazil ndio waliotangulia kufunga kupitia Fred lakini Alex Oxlade-Chamberlain alisawazisha Bao hilo.
mchezo huo ulikuwa ni wakati wa kukumbukwa sana  kutokana na Baba yake Mzazi Alex Oxlade-Chamberlain, Mark Chamberlain, aliekuwa Winga wa Stoke City, aliichezea England mara ya mwisho ilipocheza Maracana Mwaka 1984 na kuifunga Brazil Bao 2-0 katika Mechi ya Kirafiki.
England walikuwa kifua mbele kwa Bao 2-1 kwa Bao la Wayne Rooney kwa Shuti la Mita 25 huku zikiwa zimebaki Dakika 11 Mpira kwisha lakini Paulinho aliisawazishia Brazil Dakika 3 tu baadae.
MATOKEO MECHI NYINGINE ZA KIRAFIKI :
Lesotho 0 South Africa 2
Sudan 0 Tanzania 0
Algeria 2 Burkina Faso 0
Ireland 4 Georgia 0
Ukraine 0 Cameroon 0
United States 4 Germany 3

WENGER AKIRI KUWA NA NIA YA KUMSAJILI ROONEY WA MANCHESTER UNITED"

KOCHA wa klabu ya Arsenal The gunners, Arsene Wenger amekiri kuwa na nia ya kumsajili mshambuliaji nyota wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney. Wenger amekuwa akifuatilia nyendo za nyota huyo aliyeomba kuondoka mwishoni mwa msimu huu huku klabu za Chelsea na Paris Saint-Germain nazo pia zikionyesha nia ya kutaka saini ya mchezaji huyo. Akihojiwa na luninga ya Al Jazeera, Wenger amesema Rooney ni aina ya mchezaji ambaye timu yoyote kubwa duniani itahitaji huduma yake ndio maana wanafuatilia nyendo zake kama akishindwa kubakia United watajaribu kumsajili. Arsenal inategemewa kutumia kiasi cha paundi milioni 80 kwa ajili ya usajili katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi huku wakijipanga kusaini mkataba mpya wa jezi zao na kampuni ya Puma. Kwa mujibu wa ripoti zilizotoka jana, PSG wao wamepanga kumpa Rooney mshahara wa paundi milioni 350,000 kwa wiki baada ya kukatwa kodi ili kumshawishi nyota huyo kwenda Ufaransa.

JAPAN KUJITUPA DIMBANI KATIKA HARAKATI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA"

KESHO Jumanne Mei 4 Japan inaweza kuwa Nchi ya kwanza Duniani kufuzu kutinga michuano ya Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 huko Nchini Brazil ambapo kanda ya Nchi za Asia itamaliza hatua yake ya mwisho ya Mechi za Mchujo kwa Mechi za Makundi yake mawili Mwezi huu Juni na 
Bara la Asia litaingiza
moja kwa moja Timu 4 kwenye Fainali za Kombe la Dunia, mbili toka kila Kundi la michuano yao, na Timu ya 5 itapatikana baada ya Timu zitazoshika Nafasi za 3 kwenye Makundi kucheza Mechi kati yao na Mshindi kwenda kucheza na Timu kutoka Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini itakayomaliza Nafasi ya 5.
Japan, wanaoongoza Kundi B  wakiwa na Pointi 13, watakuwa Nyumbani kucheza na Australia na wanahistaji sare tu ili watinge Brazil na kuwa Nchi ya kwanza Duniani kufanya hivyo lakini pia hiyo kesho wanaweza kuingia Fainali hata wakifungwa ikiwa tu Iraq, wanaocheza Ugenini, watashindwa kuifunga Oman.
Japan wangeweza kufuzu kwenda Brazil kwenye Mechi za Raundi iliyopita lakini walifungwa 2-1 bila kutegemewa walipocheza Ugenini na Jordan lakini Mechi hii na Australia, itakayochezwa huko Saitama World Cup Stadium ni ngumu kwa vile Australia wana Wachezaji wazoefu na wao wanasaka ushindi ili nao waweze kufuzu.
Matumaini ya Japan yapo kwa Wachezaji wao kina Keisuke Honda, Yuto Nagatomo na Shinji Kagawa huku Australia ikitegemea Kikosi chao chenye Wachezaji wakongwe ambao nusu yao wako kwenye Umri unaozidi Miaka 30.
Katika Mechi yao ya kwanza kwenye Kundi lao Timu hizi zilitoka sare ya Bao 1-1.
RATIBA MECHI ZILIZOBAKI:
Jumanne Juni 4
[Saa ni za Bongo, Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
13:30 Japan v Australia [1-1]
13:00 Oman v Iraq [1-1]
16:15 Qatar v Iran [0-0]
17:30 Lebanon v South Korea [0-3]
Jumanne Juni 11
8:00 Australia v Jordan [1-2]
11:00 South Korea  v Uzbekistan [2-2]
14:30 Iraq v Japan [0-1]
16:30 Iran v Lebanon [0-1]
Jumanne Juni 18
11:00 Australia v Iraq [2-1]
15:00 South Korea v Iran [0-1]
15:00 Uzbekistan v Qatar [1-0]
19:00 Jordan v Oman [1-2]
MSIMAMO:
KUNDI A
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Uzbekistan
6
3
2
1
6
4
2
11
2
South Korea
5
3
1
1
11
5
6
10
3
Iran
5
2
1
2
2
2
0
7
4
Qatar
6
2
1
3
4
7
-3
7
5
Lebanon
6
1
1
4
2
7
-5
4
KUNDI B
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Japan
6
4
1
1
14
4
10
13
2
Jordan
6
2
1
3
6
12
-6
7
3
Australia
5
1
3
1
6
6
0
6
4
Oman
6
1
3
2
6
9
-3
6
5
Iraq
5
1
2
2
4
5
-1
5

PEREZ AWA RAIS WA NADRID KWA MARA NYINGINE TENA:

Rais wa Real madrid FLORENTINO Perez amechaguliwa kwa kipindi kingine tena katika nafasi ya urais wa klabu hiyo katika mkutano wa uchaguzi uliofanyika mapema leo. mchakato wa uteuzi wa majina lilimalizika Jumamosi usiku wakati muda wa kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo ulipomalizika bila ya kutokea mgombea yoyote wa kushindana na Perez. Kutokana na hilo bodi ya uchaguzi ya klabu hiyo ilimpitisha na kumpigia kura kama mgombea pekee kwenye uchaguzi huo na baadae kutoa taarifa kupitia katika mtandao wake. Perez mweye umri wa miaka 66 ameiongoza klabu hiyo toka mwaka 2000.

TAIFA STAR YALAZIMISHWA SARE YA KTUFUNGANA ZA SUDANI MECHI YA KIRAKI:

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imetoka sare ya bila kufungana na Sudan (Nile Crodcodile) katika mechi ya kirafiki iliyochezwa leo (Juni 2 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Addis Ababa nchini Ethiopia. Mechi hiyo iliyochezeshwa na mwamuzi Bamlak Tessema wa Ethiopia ilikuwa sehemu ya maandalizi kwa timu zote ambazo wikiendi ijayo zinacheza mechi za mchujo za Kombe la Dunia. Wakati Stars itakuwa ugenini nchini Morocco, Sudan itacheza nyumbani dhidi ya Ghana. Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ilicheza vizuri mechi hiyo, hasa kipindi cha pili ambapo ilifanikiwa kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini ama washambuliaji walipiga nje au mipira yao kuokolewa na kipa Ehab Abdelfatahh wa Sudan. Washambualiji wa Stars akina Khamis Mcha, Mrisho Ngasa na Amri Kiemba wakiongozwa na John Bocco walilitia msukosuko mara kwa mara lango la Sudan ambalo lilikuwa chini ya beki wa kati Nadir Eltayeb ambaye alifanya kazi ya ziada dakika ya 72 kuokoa mpira uliokuwa ukielekea wavuni. Stars katika mechi hiyo iliwakilishwa na Juma Kaseja, Nadir Haroub/Vicent Barnabas, Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Aggrey Morris, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, John Bocco/Haruni Chanongo, Amri Kiemba/Khamis Mcha na Simon Msuva/Athuman Idd. Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Joram Biswaro amewataka wachezaji wa Taifa Stars kuhakikisha wanaipeleka timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil. Timu inaondoka kesho alfajiri kwenda Morocco kwa kupitia Cairo, Misri ambapo inatarajia kuwasili Casablanca saa 8 mchana.

Sunday, June 2, 2013

DJOKOVIC ASONGA MBELE MICHUANO YA WAZI FRANCE

MCHEZAJI tenisi anae kamata namba moja kwa ubora duniani, Novak Djokovic amefanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya wazi ya Ufaransa baada ya kumchakaza mchezaji anayechipukia Grigor Dimitrov. Djokovic alifanikiwa kumfunga Dimitrov kwa 6-2 6-2 6-3 kabla ya kupewa taarifa mbaya za kifo cha kocha wake wa zamani Jelena Gencic ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 77. Gencic ambaye amewahi pia kufanya kazi na Monica Seles na Gora Ivanisevic, ndio alikuwa kocha wa kwanza wa Djokovic akiwa na miaka sita ambapo alimfundika kwa kipindi cha miaka mitano. Kwa kuonyesha jinsi gani alivyoguswa na msiba huo Djokovic alishindwa kuzungumza na vyombo vya habari baada ya mchezo wa jana ambapo anatarajia kurejea uwanjani tena Jumatatu kukwaana na Philipp Kohlschreiber wa Ujerumani.

Tuesday, May 28, 2013

TAIFA STARS YAANZA KUJINOA ADDIS ABABA.

  1. Taifa Stars imetua jijini Addis Ababa, Ethiopia leo (Mei 28 mwaka huu) alfajiri kwa ndege ya EgyptAir ambapo itaweka kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech. Stars iliyotua na kikosi cha wachezaji 21 imefikia hoteli ya Hilton, na imeanza mazoezi leo (Mei 28 mwaka huu) saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Addis. Kwa mujibu wa Kocha Kim Poulsen, Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na vipindi (sessions) vinne vya mazoezi kabla ya kucheza mechi ya kirafiki na Sudan (Nile Crocodile). Mechi dhidi yan Sudan itachezwa Jumapili kuanzia saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Addis. Sudan ambayo pia imeweka kambi yake Addis Ababa kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia ilicheza mechi yake ya kwanza jana (Mei 27 mwaka huu) dhidi ya wenyeji Ethiopia na kulala mabao 2-0. Wachezaji wanaounda Stars ni nahodha Juma Kaseja, nahodha msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi. Kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka Addis Ababa kwenda Marrakech alfajiri ya Juni 3 mwaka huu kwa ndege ya EgyptAir. Stars itatua siku hiyo hiyo Casabalanca na kuunganisha moja kwa moja kwenda Marrakech.