KLABU ya soka ya Anzhi Makhachkala ya Urusi imeliandikia Shirikisho la Soka nchini Cameroon-Fecafoot kuwataka kutomtumia mshambualiaji nyota wa timu hiyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Samuel Eto’o katika mechi zao ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014. Daktari wa viungo wa klabu hiyo Stijn Vendenbroucke amesema nyota huyo aliumia msuli katika fainali ya Kombe Urusi Jumamosi iliyopita na alitaka apumzike kwa wiki chache kabla ya kurejea uwanjani tena. Eto’o atasafiri kuelekea Cameroon leo ili aweze kufanyiwa vipimo vingine na daktari wa timu ya taifa ambaye ndiye atakayetoa uamuzi wa mwisho wa kama nyota huyo atakuwa fiti kucheza mechi dhidi ya Togo Juni 9 na nyingine dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC wiki moja baadae. Cameroon kwasasa wanaongoza kundi I wakiwa na alama sita, alama moja zaidi ya Libya wakati DRC wana alama nne na Togoalama moja.
Monday, June 3, 2013
BRAZIL YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 DHIDI YA ENGLAND KATIKA MECHI YA KIRAFIKI"
Katika Mechi ya ufunguzi rasmi Uwanja wa Maracana iliyopigwa jana kati ya wenyeji brazil na England jina rasmi la uwanja huo kwa sasa ni Estadio Jornalista Mário Filho huko Mjini Rio De Janeiro Wenyeji Brazil walilazimishwa sare ya kufungana Bao 2-2 na England hapo jana Usiku.
Brazil walitawala Kipindi chote cha kwanza lakini hawakupata Bao hasa kutokana na kusimama imara kwa Kipa Joe Hart.
MAGOLI:
Brazil 2
-Fred Dakika ya 57
-Paulinho 82
-England 2
- Oxlade-Chamberlain Dakika ya 67
-Rooney 79
Bao zote 4 za Mechi hiyo ziliwekwa kimiani Kipindi cha Pili na Brazil ndio waliotangulia kufunga kupitia Fred lakini Alex Oxlade-Chamberlain alisawazisha Bao hilo.
mchezo huo ulikuwa ni wakati wa kukumbukwa sana kutokana na Baba yake Mzazi Alex Oxlade-Chamberlain, Mark Chamberlain, aliekuwa Winga wa Stoke City, aliichezea England mara ya mwisho ilipocheza Maracana Mwaka 1984 na kuifunga Brazil Bao 2-0 katika Mechi ya Kirafiki.
England walikuwa kifua mbele kwa Bao 2-1 kwa Bao la Wayne Rooney kwa Shuti la Mita 25 huku zikiwa zimebaki Dakika 11 Mpira kwisha lakini Paulinho aliisawazishia Brazil Dakika 3 tu baadae.
MATOKEO MECHI NYINGINE ZA KIRAFIKI :
Lesotho 0 South Africa 2
Sudan 0 Tanzania 0
Algeria 2 Burkina Faso 0
Ireland 4 Georgia 0
Ukraine 0 Cameroon 0
United States 4 Germany 3
WENGER AKIRI KUWA NA NIA YA KUMSAJILI ROONEY WA MANCHESTER UNITED"
KOCHA wa klabu ya Arsenal The gunners, Arsene Wenger amekiri kuwa na nia ya kumsajili mshambuliaji nyota wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney. Wenger amekuwa akifuatilia nyendo za nyota huyo aliyeomba kuondoka mwishoni mwa msimu huu huku klabu za Chelsea na Paris Saint-Germain nazo pia zikionyesha nia ya kutaka saini ya mchezaji huyo. Akihojiwa na luninga ya Al Jazeera, Wenger amesema Rooney ni aina ya mchezaji ambaye timu yoyote kubwa duniani itahitaji huduma yake ndio maana wanafuatilia nyendo zake kama akishindwa kubakia United watajaribu kumsajili. Arsenal inategemewa kutumia kiasi cha paundi milioni 80 kwa ajili ya usajili katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi huku wakijipanga kusaini mkataba mpya wa jezi zao na kampuni ya Puma. Kwa mujibu wa ripoti zilizotoka jana, PSG wao wamepanga kumpa Rooney mshahara wa paundi milioni 350,000 kwa wiki baada ya kukatwa kodi ili kumshawishi nyota huyo kwenda Ufaransa.
JAPAN KUJITUPA DIMBANI KATIKA HARAKATI ZA KUFUZU KOMBE LA DUNIA"

Bara la Asia litaingiza
moja kwa moja Timu 4 kwenye Fainali za Kombe la Dunia, mbili toka kila Kundi la michuano yao, na Timu ya 5 itapatikana baada ya Timu zitazoshika Nafasi za 3 kwenye Makundi kucheza Mechi kati yao na Mshindi kwenda kucheza na Timu kutoka Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini itakayomaliza Nafasi ya 5.
moja kwa moja Timu 4 kwenye Fainali za Kombe la Dunia, mbili toka kila Kundi la michuano yao, na Timu ya 5 itapatikana baada ya Timu zitazoshika Nafasi za 3 kwenye Makundi kucheza Mechi kati yao na Mshindi kwenda kucheza na Timu kutoka Kanda ya Nchi za Marekani ya Kusini itakayomaliza Nafasi ya 5.
Japan, wanaoongoza Kundi B wakiwa na Pointi 13, watakuwa Nyumbani kucheza na Australia na wanahistaji sare tu ili watinge Brazil na kuwa Nchi ya kwanza Duniani kufanya hivyo lakini pia hiyo kesho wanaweza kuingia Fainali hata wakifungwa ikiwa tu Iraq, wanaocheza Ugenini, watashindwa kuifunga Oman.
Japan wangeweza kufuzu kwenda Brazil kwenye Mechi za Raundi iliyopita lakini walifungwa 2-1 bila kutegemewa walipocheza Ugenini na Jordan lakini Mechi hii na Australia, itakayochezwa huko Saitama World Cup Stadium ni ngumu kwa vile Australia wana Wachezaji wazoefu na wao wanasaka ushindi ili nao waweze kufuzu.
Matumaini ya Japan yapo kwa Wachezaji wao kina Keisuke Honda, Yuto Nagatomo na Shinji Kagawa huku Australia ikitegemea Kikosi chao chenye Wachezaji wakongwe ambao nusu yao wako kwenye Umri unaozidi Miaka 30.
Katika Mechi yao ya kwanza kwenye Kundi lao Timu hizi zilitoka sare ya Bao 1-1.
RATIBA MECHI ZILIZOBAKI:
Jumanne Juni 4
[Saa ni za Bongo, Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
13:30 Japan v Australia [1-1]
13:00 Oman v Iraq [1-1]
16:15 Qatar v Iran [0-0]
17:30 Lebanon v South Korea [0-3]
Jumanne Juni 11
8:00 Australia v Jordan [1-2]
11:00 South Korea v Uzbekistan [2-2]
14:30 Iraq v Japan [0-1]
16:30 Iran v Lebanon [0-1]
Jumanne Juni 18
11:00 Australia v Iraq [2-1]
15:00 South Korea v Iran [0-1]
15:00 Uzbekistan v Qatar [1-0]
19:00 Jordan v Oman [1-2]
MSIMAMO:
KUNDI A
NA
|
TIMU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
F
|
A
|
GD
|
PTS
|
1
|
Uzbekistan
|
6
|
3
|
2
|
1
|
6
|
4
|
2
|
11
|
2
|
South Korea
|
5
|
3
|
1
|
1
|
11
|
5
|
6
|
10
|
3
|
Iran
|
5
|
2
|
1
|
2
|
2
|
2
|
0
|
7
|
4
|
Qatar
|
6
|
2
|
1
|
3
|
4
|
7
|
-3
|
7
|
5
|
Lebanon
|
6
|
1
|
1
|
4
|
2
|
7
|
-5
|
4
|
KUNDI B
NA
|
TIMU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
F
|
A
|
GD
|
PTS
|
1
|
Japan
|
6
|
4
|
1
|
1
|
14
|
4
|
10
|
13
|
2
|
Jordan
|
6
|
2
|
1
|
3
|
6
|
12
|
-6
|
7
|
3
|
Australia
|
5
|
1
|
3
|
1
|
6
|
6
|
0
|
6
|
4
|
Oman
|
6
|
1
|
3
|
2
|
6
|
9
|
-3
|
6
|
5
|
Iraq
|
5
|
1
|
2
|
2
|
4
|
5
|
-1
|
5
|
PEREZ AWA RAIS WA NADRID KWA MARA NYINGINE TENA:
Rais wa Real madrid FLORENTINO Perez
amechaguliwa kwa kipindi kingine tena katika nafasi ya urais wa klabu hiyo
katika mkutano wa uchaguzi uliofanyika mapema leo. mchakato wa uteuzi wa majina lilimalizika Jumamosi usiku wakati muda wa kuchukua
fomu za kugombea nafasi hiyo ulipomalizika bila ya kutokea mgombea
yoyote wa kushindana na Perez. Kutokana
na hilo bodi ya uchaguzi ya klabu hiyo ilimpitisha na kumpigia kura
kama mgombea pekee kwenye uchaguzi huo na baadae kutoa taarifa kupitia
katika mtandao wake. Perez mweye umri wa miaka 66 ameiongoza klabu hiyo toka mwaka 2000.
TAIFA STAR YALAZIMISHWA SARE YA KTUFUNGANA ZA SUDANI MECHI YA KIRAKI:

Sunday, June 2, 2013
DJOKOVIC ASONGA MBELE MICHUANO YA WAZI FRANCE
MCHEZAJI tenisi anae kamata namba moja kwa ubora duniani, Novak Djokovic amefanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya wazi ya Ufaransa baada ya kumchakaza mchezaji anayechipukia Grigor Dimitrov. Djokovic alifanikiwa kumfunga Dimitrov kwa 6-2 6-2 6-3 kabla ya kupewa taarifa mbaya za kifo cha kocha wake wa zamani Jelena Gencic ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 77. Gencic ambaye amewahi pia kufanya kazi na Monica Seles na Gora Ivanisevic, ndio alikuwa kocha wa kwanza wa Djokovic akiwa na miaka sita ambapo alimfundika kwa kipindi cha miaka mitano. Kwa kuonyesha jinsi gani alivyoguswa na msiba huo Djokovic alishindwa kuzungumza na vyombo vya habari baada ya mchezo wa jana ambapo anatarajia kurejea uwanjani tena Jumatatu kukwaana na Philipp Kohlschreiber wa Ujerumani.
Subscribe to:
Posts (Atom)