Mabingwa wa Dunia timu ya taifa ya Spain bado ndio inaendelea kushika namba moja katika Listi ya viwango vya FIFA vya Ubora Duniani iliyotolewa leo ikifuatiwa na timu ya taifa ya ujerumani ambapo nafasi ya tatu inashikiliwa na Argentina ambapo nafasi ya nne ikishikiliwa na Croatia, huku Tanzania Taifa star ikipanda Nafasi 7 kutoka 116 hadi 109.
Katika 10 Bora, Netherlands imepanda mpaka Nafasi ya 5, Portugal kushuka Nafasi moja hadi ya 6, Colombia, wameshuka Nafasi 2 na wapo nafasi ya 7 huku timu ya taifa ya England ikiporomoka Nafasi 2 na sasa wako Nafasi ya 9.
Kwa Nchi za Afrika, Côte d'Ivoire ndio ipo Nafasi ya juu kabisa ikiwa Nafasi ya 13 ikifuatiwa na Ghana iliyokatika Nafasi ya 20.
Brazil, ambayo imeathirika kwa kucheza Mechi za Kirafiki tu kwa Miaka miwili, imeporomoka Nafasi 2 hadi Nafasi ya 22 lakini kushiriki kwao katika Mashindano rasmi ya FIFA ya kugombea Kombe la Mabara yatakayochezwa Nchini brazil kuanzia Juni 15 kama watafanya vizuri basi itawaletea faida nzuri na sana katika harakati za kupanda chati.
Toleo jingine la Listi ya FIFA ya Ubora Duniani litatolewa Julai 4.
25 BORA:
1 Spain
2 Germany
3 Argentina
4 Croatia
5 Netherlands
6 Portugal
7 Colombia
8 Italy
9 England
10 Ecuador
11 Russia
12 Belgium
13 Côte d'Ivoire
14 Switzerland
15 Bosnia-Herzegovina
16 Greece
17 Mexico
18 France
19 Uruguay
20 Denmark
21 Ghana
22 Brazil
23 Mali
24 Czech Republic
25 Chile
NCHI ZINAZOIZUNGUKA TANZANIA:
104 Qatar
105 Lithuania
106 Ethiopia
107 Niger
108 Saudi Arabia
109 Malawi
109 Tanzania {imepanda nafasi 7]
111 Kuwait
112 Tajikistan
113 Suriname
114 Korea DPR
115 Benin 308
116 Northern Ireland