Friday, June 7, 2013

MAN CITY YATANGAZA RASMI KUMTWAA KIUNGO WA KIBRAZILI FERNADINHO.

Mabingwa wa ligi kuu nchini uingereza msimu wa 2011-2012 klabu ya Manchester City imetangaza rasmi kumsajili kiungo wa kimataifa wa Brazil Fernadinho kutoka klabu ya Shakhtar Donetski ya Ukraine. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 amekuwa katika rada za City kwa karibu msimu mzima na anajulikana nchini Uingereza kwa kuifungia klabu yake bao katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Chelsea katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi msimu uliopita. City ambao mpaka sasa hawajapa mbadala wa kocha Roberto Mancini aliyeondoka, hawakutoa taarifa zozote za kiasi cha fedha walizomnunulia mchezaji huyo lakini kumekuwa na tetesi katika vyombo vya habari nchini Uingereza kuwa amewagharimu kiasi cha paundi milioni 30. Akihojiwa Fernadinho amesema kuwa hayo ni mabadiliko, changamoto na nafasi aliyokuwa akiisubiria kwa kipindi kirefu na kuichezea City ni kama ndoto zake zimekuwa kweli. 

FALCAO AWEKA WAZI KUWA NIA KUBWA NI KUIPA MAFANIKIO MONACO.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao amesema nia yake kubwa ni kuisadia klabu ya Monaco ya Ufaransa kuwa moja ya klabu bora barani Ulaya kwa mara nyingine tena. Akihojiwa baada ya mazoezi na timu yake ya taifa jana Alhamisi Falcao amesema anajisikia fahari kubwa kuwapo Monaco hivyo kutokana na kuvutiwa na mipango waliyokuwa nayo katika kipindi kijacho hivyo mategemeo yao nikuifikisha timu hiyo katika anga za mafanikio. Akiwa Monaco nyota huyo wa zamani wa klabu ya Atletico Madrid ataungana na winga James Rodriguez ambaye pia ni raia wa Colombia baada ya kukubali uhamisho akitokea klabu ya FC Porto. Falcao amesema ana mahusiano mazuri na winga huyo na sio katika soka pekee bali wamekuwa marafiki wa karibu hata nje ya uwanja, na kummwagia sifa kwamba ni mchezaji bora ndio maana Monaco wametumia fedha nyingi kumsajili. 

BOLT MKALI WA MBIO FUPI DUNIANI KUKABIDHI ZAWADI NCHINI UFARANSA.

SHIRIKISHO la Tenisi nchini Ufaransa limetangza kuwa mshindi wa michuano ya wazi ya Ufaransa kwa upande wa wanaume atakabidhiwa zawadi na mkimbiaji nyota wa mbio fupi duniani raia wa Jamaica Usain Bolt.

Bolt bingwa mara sita wa michuano ya Olimpiki ambaye jana alishindwa kutamba katika mashindano ya Diamond League yaliyofanyika jijini Rome itali baada ya kushindwa na Justin Gatlin wa Marekani, atakuwa mwanariadha wa kwanza kupata heshima hiyo kwenye michuano mikubwa ya tenisi. 

Nusu fainali kwa upande wanaume inatarajiwa kufanyika leo ambapo bingwa mtetezi wa michuano hiyo Rafael Nadal anatarajia kuchuana na Novak Djokovic ukifuatiwa na mchezo mwingine wa nusu fainali kati ya Jo-Wilfried Tsonga dhidi ya David Ferrer. Kwa upande wa wanawake ambapo fainali itafanyika Jumamosi kati ya Serena Williams na maria Sharapova, tuzo yao itakabidhiwa na bingwa mara tatu wa zamani wa michuano hiyo ambaye pia amewahi kuongoza katika orodha za ubora kwa wanawake Arantxa Sanchez Vicario wa Hispania. 

Thursday, June 6, 2013

GALLIANI ASEMA HATUNA MPANDO NA KAKA KUJA MILAN.

Adriano Galliani ambaye ni ofisa mkuu wa klabu ya AC Milan ya Italia,ametanabaisha na kuweka wazi kuwa klabu hiyo haina mpango wa kumsajili kiungo wa klabu ya Real Madrid Kaka ambapo amesema mchezaji huyo ameshakuwa mtu mzima. Kaka mwenye umri wa miaka 31 amekuwa akihusishwa na tetesi za kurejea San Siro kwa zaidi ya mara moja toka alipoondoka Milan kwenda Madrid mwaka 2009 lakini Galliani amekanusha tetesi hizo za kumsajili nyota huyo kutokana na umri wake. Kiungo huyo mshambuliaji bado ana mkataba na Madrid naomalizika katika kipindi majira ya kiangazi mwaka 2015 lakini anategemewa kuondoka katika klabu hiyo kutokana na kushindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza kwa miaka kadhaa sasa. Kaka amecheza mechi 19 pekee katika msimu wa 2012-2013 na kufunga mabao matatu. 

ETO"O ATWAA MCHEZAJI BORA WA LIGI NCHINI URUSI.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Cameroon na klabu ya Anzhi Makhachkala ya Urusi Samuel Eto’o ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa msimu wa Ligi Kuu ya nchi hiyo kwa msimu wa 2012-2013. Eto’o ambaye amewahi kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora Afrika mara nne, alikabidhiwa tuzo hiyo baada ya kuisadia timu yake kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wan chi hiyo. Akihojiwa mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Eto’o ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo amedai kufurahishwa na hatua hiyo na kuwashukuru mashabiki wa soka nchini humo pamoja na waandishi wa habari kwa kuwa nyuma yake wakati wote. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 atakosa mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014 wa timu ya taifa ya nchi yake dhidi ya Togo utakaochezwa Juni 9 mwaka huu kutokana na majeraha yanayomsumbua. 
SAMWELI ETO'O KATIKA ULIMWENGU WA SOKA
Samuel 2011.jpg
Eto'o in 2011.
Kuhusu yeye
Full nameSamuel Eto'o Fils
Date of birth10 March 1981 (age 32)
Place of birthDoualaCameroon[1]
Height1.80 m (5 ft 11 in)[2]
Playing positionStriker
Timu
Current clubAnzhi Makhachkala
Number9
academy
1992–1997Kadji Sports Academy
Timu za ukubwa
YearsTeammechi(Goli)"
1997–2000Real Madrid3(0)
1997–1998→ Leganés (mkopo)30(4)
1999→ Espanyol (mkopo)0(0)
2000→ Mallorca (mkopo)19(6)
2000–2004Mallorca120(48)
2004–2009Barcelona145(108)
2009–2011Internazionale67(33)
2011–Anzhi Makhachkala43(21)



SPAIN BADO NAMBA MOJA UBORA DUNIANI - FIFA

Mabingwa wa Dunia timu ya taifa ya Spain bado ndio inaendelea kushika namba moja katika Listi ya viwango vya FIFA vya Ubora Duniani iliyotolewa leo ikifuatiwa na timu ya taifa ya ujerumani ambapo nafasi ya tatu inashikiliwa na  Argentina  ambapo nafasi ya nne ikishikiliwa na  Croatia, huku Tanzania Taifa star ikipanda Nafasi 7 kutoka 116 hadi 109.
Katika 10 Bora, Netherlands imepanda  mpaka Nafasi ya 5, Portugal kushuka Nafasi moja hadi ya 6, Colombia, wameshuka Nafasi 2 na wapo nafasi ya 7 huku timu ya taifa ya England ikiporomoka Nafasi 2 na sasa wako Nafasi ya 9.
Kwa Nchi za Afrika, Côte d'Ivoire ndio ipo Nafasi ya juu kabisa ikiwa Nafasi ya 13 ikifuatiwa na Ghana iliyokatika Nafasi ya 20.
Brazil, ambayo imeathirika kwa kucheza Mechi za Kirafiki tu kwa Miaka miwili, imeporomoka Nafasi 2  hadi Nafasi ya 22 lakini kushiriki kwao katika Mashindano rasmi ya FIFA ya kugombea Kombe la Mabara yatakayochezwa Nchini brazil  kuanzia Juni 15 kama watafanya vizuri basi itawaletea faida nzuri na sana katika harakati za kupanda chati.
Toleo jingine la Listi ya FIFA ya Ubora Duniani litatolewa Julai 4.
25 BORA:
1        Spain
2        Germany
3        Argentina
4        Croatia
5        Netherlands
6        Portugal
7        Colombia
8        Italy
9        England
10      Ecuador
11      Russia
12      Belgium
13      Côte d'Ivoire
14      Switzerland
15      Bosnia-Herzegovina
16      Greece
17      Mexico
18      France
19      Uruguay
20      Denmark
21      Ghana
22      Brazil
23      Mali
24      Czech Republic
25      Chile
NCHI ZINAZOIZUNGUKA TANZANIA:
104    Qatar
105    Lithuania
106    Ethiopia
107    Niger
108    Saudi Arabia
109    Malawi
109    Tanzania {imepanda nafasi 7]
111    Kuwait
112    Tajikistan
113    Suriname
114    Korea DPR
115    Benin 308
116    Northern Ireland

JESUS AONGEZEWA MKATABA MPYA NDANI YA KLABU YA BENFICA.


KLABU ya Benfica ya Ureno imetangaza kumuongezea mkataba mpya kocha wake Jorge Jesus atakao dumu nao klubuni hapo mpaka katika kipindi cha majira ya kiangazi mwaka 2015. Kulikuwa na wasiwasi kama kocha huyo mwenye umri wa miaka 58 anaweza kubakia katika klabu hiyo baada ya kumaliza msimu na kuambulia patupu. Hata hivyo Jesus sasa amemaliza utata huo kwa kusaini miaka miwili zaidi na klabu hiyo inayotoka katika jijini Lisbon. Jesus alianza kuinoa Benfica kuanzia mwaka 2009 na kuingoza kushinda taji moja la Ligi Kuu na matatu ya Kombe la Ligi la nchi hiyo.