Friday, June 7, 2013

TAIFA STARS YAIKABILI MOROCCO UGENINI KESHO DIMBANI.

Taifa Stars inatupa karata yake ya pili ugenini kwenye mechi za mchujo za Kombe la Dunia kwa kesho (Juni 8 mwaka huu) kuikabili Morocco (Lions of the Atlas) kwenye Uwanja wa Grand Stade hapa Marrakech, Morocco.

Ilipoteza ya kwanza ugenini dhidi ya Ivory Coast mwaka jana, na kushinda mbili mfululizo nyumbani dhidi ya Gambia na Morocco. Mechi hiyo itakayochezwa kuanzia saa 3 usiku kwa saa za Morocco ni ya pili kwa Stars katika uwanja huo ambapo mwaka juzi ilifungwa mabao 3-1.

Washabiki wa Morocco wanaonekana kuikatia tama timu yao yenye pointi mbili tu nyuma ya Ivory Coast inayoongoza kundi hilo la C ikiwa na pointi saba ikifuatiwa na Tanzania yenye sita. Huo ni mtazamo wa washabiki, lakini kwa upande wa timu inaonekana imepania kujichomoa katika nafasi za chini.

Kwa upande wa Kocha wa Stars, Kim Poulsen amesema timu yake imepania mechi hiyo, lengo likiwa ni kuona inapata matokeo mazuri baada ya dakika 90 za mechi hiyo itakayokuwa chini ya refa Daniel Frazier Bennett wa Afrika Kusini.

Amesema timu yake itacheza kwa umakini na uangalifu kwa vile wanajua wapinzani wao wakicheza mbele ya washabiki wao watakuwa katika shinikizo za kushinda, jambo ambalo wamejiandaa kukabiliana nalo.

Kwa upande wa maandalizi, Kim amesema Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadhamini wa timu hiyo Kilimanjaro Premium Lager wameiandaa vizuri kwani iko kambini kwa wiki tatu sasa na kupata mechi ya kirafiki dhidi ya Sudan iliyochezwa wiki iliyopita nchini Ethiopia.

Stars iliifunga Morocco mabao 3-1 zilipokutana Machi 24 mwaka huu jijini Dar es Salaa. Lakini zilipokutana hapa Marrakech mara ya mwisho mwaka 2011, Morocco iliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Kim amesisitiza kuwa kikosi chake kimepania kufanya vizuri katika michuano hii ya mchujo ya Kombe la Dunia, ha hiyo inathibitishwa na matokeo ya timu kadri inavyoendelea kucheza mechi za mashindano.

“Moja ya mipango yetu katika mechi hizi za Kombe la Dunia ni kushinda nyumbani, hilo hadi sasa tumelifanya kwa asilimia 100. Lakini ili tukae vizuri zaidi tumekuja hapa Morocco kwa lengo la kupata matokeo mazuri, ingawa tunajua mechi itakuwa ngumi,” amesema kocha huyo raia wa Denmark.

Kwa hapa Marrakech mechi hiyo imekuwa haizungumzwi mara kwa mara, na kubwa ni kuwa Wamorocco wengi wanaamini kuwa timu yao ambayo hadi sasa ina pointi mbili haina nafasi ya kusonga mbele katika hatua inayofuata ya michuano hiyo.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Marrakech, Morocco
+212 610120619

GAZIDIS ATHIBITISHA KUWA ARSENAL WENGER ATAONGEZA MKATABA MPYA.

MTENDAJI Mkuu wa The Gunners club ya Arsanal Ivan Gazidis ametanabaisha kuwa kocha wa timu hiyo Arsene Wenger anataka aongeze Mkataba wake mwishoni mwa msimu ujao na kuiongoza klabu hiyo kufanya vizuri katika soka ya Ulaya.
Mkataba wa Wenger unaisha mwakani na tayari amepata ofa kibao kuanzia nyumbani kwao Ufaransa, ambako Paris Saint-Germain na klabu yake ya zamani, Monaco zinamtaka.
Sign him up! Gazidis wants the French boss to extend his deal with Arsenal beyond next summer
Gazidis (chini kushoto) anataka Mfaransa aongeze Mkataba mwishoni mwa msimu ujao
Sign him up! Gazidis wants the French boss to extend his deal with Arsenal beyond next summer
Matokeo mabaya ya miaka ya karibuni yalitarajiwa kumuweka katika wakati mgumu kocha huyo mwenye umri wa miaka 63, lakini Gazidis anatarajia atabaki na kuunda kikosi cha nguvu.
Pato la mwaka la Arsenal linatarajiwa kuongezeka kwa Pauni Milioni 70, na kuwasogeza kwa wanaopata Pauni Milioni 300, Real Madrid, Barcelona, Manchester United na mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich.
Hiyo itawapa fursa ya kushindana na klabu hizo kununua wachezaji wa kuanzia Pauni Milioni 25 na kutaka mishahara ya kuanzia Pauni 200,000 kwa wiki kama Wayne Rooney, mmoja kati ya wachezaji inayowataka hivi sasa.
Klabu tatu za juu katika msimamo wa Ligi Kuu ya England, Manchester United, City na Chelsea zote zimebadilisha makocha wao, lakini Arsenal bado na imani na Wenger.

JOSE MOURINHO AJA NA KASI MPYA NA NGUVU MPYA KATIKA USAJILI".

Baada ya kukabidhiwa bikoba kwa mara ya pili ndani ya Chelsea jose mourinho amekuja kasi mapya ya kutafuta  washambuliaji kikosini hapo baada ya jana usiku kuanza mazungumzo na mchezaji mwenye thamani ya Pauni Milioni 50, Edinson Cavani wa Napoli, saa kadhaa baada ya kutoa ofa ya Pauni ya Milioni 34.9 kumnasa mshambuliaji wa Zenit St Petersburg, Hulk.
Kocha Mourinho ameorodhesha wachezaji wanne anaowataka wakiwemo kutoka Fiorentina, Stevan Jovetic na Manchester City, Edin Dzeko katika orodha hiyo.
Interest: Napoli have opened talks with Chelsea over Uruguay striker Edinson Cavani (left)
Napoli imeanza mazungumzo na Chelsea kuhusu mshambuliaji wa Uruguay, Edinson Cavani (kushoto)
Mourinho ameweka wzi na kuamini kuwa atamsajili mchezaji wa Pauni Milioni 25, Jovetic na kuwapiku Juventus, lakini anakabiliwa na ushindani kutoka klabu yake ya zamani, Real Madrid katika kuwania saini ya Cavani wakati Dzeko anaonekana kuwa mboni mbadala. Napoli haijakataa mpango wa kubadilishana Cavani na Dzeko na Manchester City, lakini mpango unaonekana kusinzia.
Rais wa Napoli, Aurelio de Laurentiis alisema jana usiku: "Kuna dhamira kutoka Chelsea kwa Cavani, watanipigia mimi saa chache zijazo. Nitafurahi akibaki, lakini ikiwa ataondoka atampata mbadala wake,".
Mshambuliaji wa Brazil, Hulk pia amethibitisha Mourinho anamtaka Stamford Bridge.
Target: Chelsea have made a £35m offer for Zenit St Petersburg's Brazilian forward Hulk
Chelsea imetoa ofa ya Pauni Milioni 35 kwa Zenit St Petersburg juu ya Mbrazil, Hulk.

MAN CITY YATANGAZA RASMI KUMTWAA KIUNGO WA KIBRAZILI FERNADINHO.

Mabingwa wa ligi kuu nchini uingereza msimu wa 2011-2012 klabu ya Manchester City imetangaza rasmi kumsajili kiungo wa kimataifa wa Brazil Fernadinho kutoka klabu ya Shakhtar Donetski ya Ukraine. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 amekuwa katika rada za City kwa karibu msimu mzima na anajulikana nchini Uingereza kwa kuifungia klabu yake bao katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Chelsea katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi msimu uliopita. City ambao mpaka sasa hawajapa mbadala wa kocha Roberto Mancini aliyeondoka, hawakutoa taarifa zozote za kiasi cha fedha walizomnunulia mchezaji huyo lakini kumekuwa na tetesi katika vyombo vya habari nchini Uingereza kuwa amewagharimu kiasi cha paundi milioni 30. Akihojiwa Fernadinho amesema kuwa hayo ni mabadiliko, changamoto na nafasi aliyokuwa akiisubiria kwa kipindi kirefu na kuichezea City ni kama ndoto zake zimekuwa kweli. 

FALCAO AWEKA WAZI KUWA NIA KUBWA NI KUIPA MAFANIKIO MONACO.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao amesema nia yake kubwa ni kuisadia klabu ya Monaco ya Ufaransa kuwa moja ya klabu bora barani Ulaya kwa mara nyingine tena. Akihojiwa baada ya mazoezi na timu yake ya taifa jana Alhamisi Falcao amesema anajisikia fahari kubwa kuwapo Monaco hivyo kutokana na kuvutiwa na mipango waliyokuwa nayo katika kipindi kijacho hivyo mategemeo yao nikuifikisha timu hiyo katika anga za mafanikio. Akiwa Monaco nyota huyo wa zamani wa klabu ya Atletico Madrid ataungana na winga James Rodriguez ambaye pia ni raia wa Colombia baada ya kukubali uhamisho akitokea klabu ya FC Porto. Falcao amesema ana mahusiano mazuri na winga huyo na sio katika soka pekee bali wamekuwa marafiki wa karibu hata nje ya uwanja, na kummwagia sifa kwamba ni mchezaji bora ndio maana Monaco wametumia fedha nyingi kumsajili. 

BOLT MKALI WA MBIO FUPI DUNIANI KUKABIDHI ZAWADI NCHINI UFARANSA.

SHIRIKISHO la Tenisi nchini Ufaransa limetangza kuwa mshindi wa michuano ya wazi ya Ufaransa kwa upande wa wanaume atakabidhiwa zawadi na mkimbiaji nyota wa mbio fupi duniani raia wa Jamaica Usain Bolt.

Bolt bingwa mara sita wa michuano ya Olimpiki ambaye jana alishindwa kutamba katika mashindano ya Diamond League yaliyofanyika jijini Rome itali baada ya kushindwa na Justin Gatlin wa Marekani, atakuwa mwanariadha wa kwanza kupata heshima hiyo kwenye michuano mikubwa ya tenisi. 

Nusu fainali kwa upande wanaume inatarajiwa kufanyika leo ambapo bingwa mtetezi wa michuano hiyo Rafael Nadal anatarajia kuchuana na Novak Djokovic ukifuatiwa na mchezo mwingine wa nusu fainali kati ya Jo-Wilfried Tsonga dhidi ya David Ferrer. Kwa upande wa wanawake ambapo fainali itafanyika Jumamosi kati ya Serena Williams na maria Sharapova, tuzo yao itakabidhiwa na bingwa mara tatu wa zamani wa michuano hiyo ambaye pia amewahi kuongoza katika orodha za ubora kwa wanawake Arantxa Sanchez Vicario wa Hispania. 

Thursday, June 6, 2013

GALLIANI ASEMA HATUNA MPANDO NA KAKA KUJA MILAN.

Adriano Galliani ambaye ni ofisa mkuu wa klabu ya AC Milan ya Italia,ametanabaisha na kuweka wazi kuwa klabu hiyo haina mpango wa kumsajili kiungo wa klabu ya Real Madrid Kaka ambapo amesema mchezaji huyo ameshakuwa mtu mzima. Kaka mwenye umri wa miaka 31 amekuwa akihusishwa na tetesi za kurejea San Siro kwa zaidi ya mara moja toka alipoondoka Milan kwenda Madrid mwaka 2009 lakini Galliani amekanusha tetesi hizo za kumsajili nyota huyo kutokana na umri wake. Kiungo huyo mshambuliaji bado ana mkataba na Madrid naomalizika katika kipindi majira ya kiangazi mwaka 2015 lakini anategemewa kuondoka katika klabu hiyo kutokana na kushindwa kupata namba katika kikosi cha kwanza kwa miaka kadhaa sasa. Kaka amecheza mechi 19 pekee katika msimu wa 2012-2013 na kufunga mabao matatu.