KIUNGO nyota wa Chelsea na timu ya Taifa ya Ghana Michael Essien amesema kuwa amejiandaa kucheza nafasi yoyote chini ya kocha mpya wa klabu hiyo Jose Mourinho. Kiungo huyo wa kimataifa wa Ghana alikuwa akipewa nafasi kidogo ya kucheza chini Roberto Di Matteo baada kusumbuliwa na majeraha ya mguu lakini alipata ahueni wakati Mourinho alipomwita kwa mkopo wakati akifundisha Real Madrid. Mourinho amekuwa akimchezesha Essien kama beki au kiungo wakati akiwa Santiago Bernabeu na sasa yuko tayari kucheza nafasi yoyote ambayo Mreno huyo atamchezesha. Essien mwenye umri wamiaka 30 alisajiliwa na Mourinho wakati akiwa Chelsea mwaka 2005 kwa ada ya paundi milioni 29 akitokea klabu ya Lyon ya Ufaransa.
Thursday, June 13, 2013
Wednesday, June 12, 2013
MWAIKIMBA KATIKA HARAKATI ZA MAISHA YA SOKA:
JINA
KAMILI: Gaudence Mwaikimba
KUZALIWA: Oktoba 5, 1984
ALIPOZALIWA: Kyela,
Mbeya
KLABU YAKE: Azam FC
NAFASI UWANJANI; Mshambuliaji
UREFU; 189 cm
KLABU ZA AWALI:
MWAKA CLUB
2003-2004:
Tukuyu Stars
2004-
2005: Kahama United
2005-
2006: Ashanti United
2006-
2009: Yanga SC
2009-2010:
Sur (Oman)
2010: Prisons
FC
2011-
2012: Kagera
Sugar
2012: Moro
United
2012 hadi sasa Azam FC
WASIFU
Baadhi ya Picha Zikimuonyesha Gaudence Mwaikimba akiwa n
|
DAVID VILLA KATIKA ULIMWENGU WA SOKA JE WAMJUA?
![]() Villa in 2008 | |||
Personal information | |||
---|---|---|---|
Full name | David Villa Sánchez[] | ||
Date of birth | 3 December 1981 (age 31)] | ||
Place of birth | Langreo, Spain | ||
Height | 1.75 m (5 ft 9 in)[2] | ||
Playing position | Striker | ||
Club information | |||
Current club | Barcelona | ||
Number | 7 | ||
Youth career | |||
1991–1999 | Langreo | ||
Senior career* | |||
Years | Team | Apps† | (Gls)† |
1999–2001 | Sporting Gijón B | 65 | (25) |
2001–2003 | Sporting Gijón | 80 | (38) |
2003–2005 | Zaragoza | 73 | (32) |
2005–2010 | Valencia | 166 | (108) |
2010– | Barcelona | 77 | (33) |
National team‡ | |||
2000–2003 | Spain U21 | 7 | (0) |
2005– | Spain | 88 | (53) |
2002 | Asturias | 1 | (0) |
CLUB MATAJI |
- Real Zaragoza
- Copa del Rey (1): 2003–04
- Supercopa de España (1): 2004
- Valencia
- Copa del Rey (1): 2007–08
- Barcelona
- La Liga (2): 2010–11, 2012–13
- Copa del Rey (1): 2011–12
- Supercopa de España (2): 2010, 2011
- UEFA Champions League (1): 2010–11
- UEFA Super Cup (1): 2011
- FIFA Club World Cup (1): 2011
SIMBA NA YANGA YAZIWEKEA NGUMU KUSHIRIKI MICHUANO YA KAGAME-SERIKALI
SERIKALI imesisitiza kuwa timu za Simba na Yanga hazitashiriki katika michuano ya klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati maarufu kama kombe la Kagame. Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Amos Makala ametoa taarifa hiyo leo Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Sumve Mheshimiwa Richard Ndasa. Katika swali lake mheshimiwa Ndasa ametaka kujua msimamo wa Serikali juu ya timu za Simba na Yanga kushiriki michuano ya Kagame inayotarajia kuanza Juni 18 hadi Julai 2, mwaka huu huko Sudan Kusini. Akijibu swali hilo mheshimiwa MAKALA amesema kumekuwa na taarifa za hali ya usalama katika Nchi ya Sudan kuwa sio nzuri. Amesema kumekuwa na taarifa kulingana na hali ya usalama nchini Sudan na kwamba Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mheshimiwa Benard Membe tayari amelitolea taarifa na ndani ya Serikali kuna taarifa za kutosha kuwa Sudan hakuna usalama. Amesema msimamo wa Serikali ni kuwa hawawezi kupeleka timu mahali ambapo hakuna usalama.
KIKOSI CHA IVORY COAST KUWASILI JUNI 13
Msafara wa timu ya Taifa ya Ivory Coast (The Elephants) wa watu 80 wakiwemo wachezaji 27 unatarajiwa kuwasili nchini kesho (Juni 13 mwaka huu) kwa ndege maalum kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars.
Mechi hiyo itachezwa Jumapili (Juni 16 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 9 kamili alasiri, na itachezeshwa na Charef Mehdi Abdi kutoka Algeria.
Kikosi hicho kitawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 2.50 usiku na kitafikia hoteli ya Bahari Beach iliyoko nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Timu hiyo inatarajia kuondoka saa chache baada ya mechi hiyo.
Wachezaji walioko katika kikosi hicho ni Abdoul Razak, Akpa Akpro Jean-Daniel Dave Lewis, Angoua Brou Benjamin, Arouna Kone, Aurier Serge Alain Stephane, Bamba Souleman, Barry Boubacar, Boka Etienne Arthur, Bolly Mathis Gazoa Kippersund, Bony Wilfried Guemiand, Cisse Abdoul Karim, Diarrassou Ousmane Viera na Dja Djedje Brice Florentin.
Doumbia Seydou, Gbohouo Guelassiognon Sylvain, Gosso Gosso Jean-Jacques, Kalou Salomon Armand Magloire, N’dri Koffi Christian Romaric, Sangare Badra, Serey Die Gnonzaroua Geoffroy, Sio Giovanni, Tiote Cheik Ismael, Toure Yaya Gnegneri, Traore Lacina, Ya Konan Didier, Yao Kouassi Gervais na Zokora Deguy Alain Didier.
Taifa Stars iko kambini hoteli ya Tansoma tangu iliporejea kutoka Marrakesh, Morocco ambapo leo na kesho itafanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 9 kamili alasiri. Ijumaa itapumzika, na itafanya mazoezi ya mwisho Jumamosi kwenye uwanja huo huo kuanzia saa 10 kamili.
Makocha wa timu zote mbili (Taifa Stars na The Elephants) watakutana na waandishi wa habari Jumamosi (Juni 15 mwaka huu) saa 4 asubuhi kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF kuzungumzia jinsi walivyojiandaa kwa mechi hiyo.
KIINGILIO MECHI YA STARS, IVORY COAST 5,000/-
Kiingilio cha chini katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Ivory Coast (The Elephants) itakayochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya kijani.
Viti vya kijani katika uwanja huo wenye uwezo wa kumeza watazamaji 60,000 viko 19,648. Kwa upande wa viti vya rangi ya bluu ambavyo viko 17,045 ni sh. 7,000. Kiingilio kwa viti vya rangi ya chungwa ambavyo viko 11,897 ni sh. 10,000.
Viingilio vya daraja la juu ni kama ifuatavyo; VIP C yenye watazamaji 4,060 ni sh. 15,000 wakati sh. 20,000 ni kwa VIP B yenye watazamaji 4,160. VIP A yenye watazamaji 748 kiingilio chake ni sh. 30,000.
Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo itakayoanza saa 9 kamili alasiri zitaanza kuuzwa siku mbili kabla ya mchezo (Ijumaa na Jumamosi) katika vituo vifuatavyo; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Sokoni Kariakoo, mgahawa wa Steers ulioko mtaa wa Ohio/Samora, Oilcom Ubungo, Kituo cha Mafuta Buguruni, Dar Live Mbagala na BMM Salon iliyoko Sinza Madukani.
Katika vituo hivyo tiketi zitauzwa katika magari maalumu. Magari hayo pia yatafanya mauzo ya tiketi uwanjani siku ya mechi. Tunapenda kuwakumbusha watazamaji kutonunua tiketi mikononi mwa watu au katika maeneo yasiyohusika ili kuepuka kununua tiketi bandia, hivyo kukosa fursa ya kushuhudia mechi hiyo.
Utaratibu katika mechi hiyo utakuwa kama ilivyokuwa katika mchezo wa Simba na Yanga, ambapo hayataruhusiwa kuingia uwanjani isipokuwa kwa yale yatakayokuwa na sticker maalumu kutoka TFF.
HATUA YA TATU RCL KUCHEZWA JUMAMOSI
Mechi za kwanza za hatua ya tatu ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kuwania nafasi tatu za kupanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao zitachezwa Jumamosi (Juni 15 mwaka huu) wakati za marudiano zitachezwa Jumatano ya Juni 19 mwaka huu.
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana jana (Juni 11 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kupitia ripoti za michezo iliyopita na kufanya uamuzi mbalimbali ikiwemo mechi ya marudiano kati ya Mpwapwa Stars na Machava FC ambayo haikuchezwa.
Machava FC ambayo ilishinda mechi ya kwanza iliyochezwa mjini Moshi kwa mabao 2-0 inaendelea katika hatua ya tatu kwa vile haikuhusika katika kukwamisha mchezo wa marudiano uliopangwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) kiliuhamishia mchezo huo kwenye Uwanja wa Mgambo mjini Mpwapwa kinyume na maelekezo ya Kamati ya Mashindano ya TFF. Kamati katika kikao chake cha awali iliekeleza kuwa mechi zote za RCL zitachezwa makao makuu ya mikoa isipokuwa kwa Morogoro ambapo timu ya Techfort FC iliruhusiwa kutumia Uwanja wa CCM Mkamba mjini Ifakara.
Hivyo timu nane zilizofuzu kucheza raundi hiyo ni Friends Rangers ya Dar es Salaam, Kariakoo ya Lindi, Katavi Warriors ya Katavi, Kimondo SC ya Mbeya, Machava ya Kilimanjaro, Njombe Mji ya Njombe, Polisi Jamii ya Mara na Stand United FC ya Shinyanga.
Wakati timu nyingine zimefuzu kwa kushinda mechi zao za raundi ya mbili, Njombe Mji imeingia hatua hiyo kwa kuwa timu yenye uwiano mdogo wa kufungwa (best looser) katika hatua ya pili.
Katika hatua hiyo mechi ni ifuatavyo; Kariakoo vs Friends Rangers, Machava FC vs Stand United FC, Polisi Jamii vs Katavi Warriors, na Kimondo SC vs Njombe Mji. Timu zilizoanza kutajwa ndizo zinazoanzia nyumbani.
Vilevile Kamati ya Mashindano imeagiza Kamishna wa mechi ya marudiano kati ya Mpwapwa Stars vs Machava FC, Mwijage Rugakingira wa Tanga ambaye alikwenda Uwanja wa Mgambo badala ya Uwanja wa Jamhuri kinyume na maelekezo ya TFF aondolewe kwenye orodha ya makamishna.
Pia waamuzi wa mechi hiyo ambao nao walikwenda Mpwapwa badala ya Dodoma Mjini wamepelekwa Kamati ya Waamuzi ya TFF kwa ajili ya kuchukuliwa hatua kutokana na tukio hilo.
Kamati ya Mashindano imekumbusha kuwa RCL ni mashindano yanayosimamiwa na TFF, hivyo maelekezo yoyote kuhusiana na mashindano hayo pia yatatoka TFF na si mahali pengine popote. Hivyo, msimamizi wa kituoa hana mamlaka ya kubadili uwanja.
Hatua ya nne ya RCL itachezwa kati ya Juni 23 na 23 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitachezwa kati ya Juni 29 na 30 mwaka huu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Tuesday, June 11, 2013
WAALGERIA KUCHEZESHA TAIFA STARS, IVORY COAST
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limeteua waamuzi kutoka Algeria kuchezesha mechi kati ya Taifa Stars na Ivory Coast itakayofanyika Jumapili saa 9 alasiri kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Waamuzi hao watakaochezesha mechi hiyo ya kundi C kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil wataongozwa na Charef Mehdi Abid atakayepuliza filimbi. Atasaidiwa na Hamza Hammou na Bouabdallah Omari wakati mezani atakuwa Sofiane Bousseter.
Abdi na wezake wanatarajiwa kutua nchini Ijumaa (Juni 14 mwaka huu) saa 12 asubuhi kwa ndege ya EgyptAir. Mtathmini wa waamuzi ni Athanase Nkubito kutoka Rwanda ambaye atatua nchini Ijumaa (Juni 14 mwaka huu) saa 12 jioni kwa ndege ya RwandAir.
Kamishna wa mechi hiyo ni Bernard Mfubusa kutoka nchini Burundi ambapo atawasili nchini Ijumaa (Juni 14 mwaka huu) saa 3.35 asubuhi kwa ndege ya Kenya Airways. Maofisa wote hao wa mechi hiyo watarejea makwao Jumatatu (Juni 17 mwaka huu).
HATUA YA TATU RCL KUCHEZWA JUMAMOSI
Mechi za kwanza za hatua ya tatu ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kuwania nafasi tatu za kupanda Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao zitachezwa Jumamosi (Juni 15 mwaka huu) wakati za marudiano zitachezwa Jumatano ya Juni 19 mwaka huu.
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo (Juni 11 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kupitia ripoti za michezo iliyopita na kufanya uamuzi mbalimbali ikiwemo mechi ya marudiano kati ya Mpwapwa Stars na Machava FC ambayo haikuchezwa.
Machava FC ambayo ilishinda mechi ya kwanza iliyochezwa mjini Moshi kwa mabao 2-0 inaendelea katika hatua ya tatu kwa vile haikuhusika katika kukwamisha mchezo wa marudiano uliopangwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dodoma (DOREFA) kiliuhamishia mchezo huo kwenye Uwanja wa Mgambo mjini Mpwapwa kinyume na maelekezo ya Kamati ya Mashindano ya TFF. Kamati katika kikao chake cha awali iliekeleza kuwa mechi zote za RCL zitachezwa makao makuu ya mikoa isipokuwa kwa Morogoro ambapo timu ya Techfort FC iliruhusiwa kutumia Uwanja wa CCM Mkamba mjini Ifakara.
Hivyo timu nane zilizofuzu kucheza raundi hiyo ni Friends Rangers ya Dar es Salaam, Kariakoo ya Lindi, Katavi Warriors ya Katavi, Kimondo SC ya Mbeya, Machava ya Kilimanjaro, Njombe Mji ya Njombe, Polisi Jamii ya Mara na Stand United FC ya Shinyanga.
Wakati timu nyingine zimefuzu kwa kushinda mechi zao za raundi ya mbili, Njombe Mji imeingia hatua hiyo kwa kuwa timu yenye uwiano mdogo wa kufungwa (best looser) katika hatua ya pili.
Katika hatua hiyo mechi ni ifuatavyo; Kariakoo vs Friends Rangers, Machava FC vs Stand United FC, Polisi Jamii vs Katavi Warriors, na Kimondo SC vs Njombe Mji. Timu zilizoanza kutajwa ndizo zinazoanzia nyumbani.
Vilevile Kamati ya Mashindano imeagiza Kamishna wa mechi ya marudiano kati ya Mpwapwa Stars vs Machava FC, Mwijage Rugakingira wa Tanga ambaye alikwenda Uwanja wa Mgambo badala ya Uwanja wa Jamhuri kinyume na maelekezo ya TFF aondolewe kwenye orodha ya makamishna.
Pia waamuzi wa mechi hiyo ambao nao walikwenda Mpwapwa badala ya Dodoma Mjini wamepelekwa Kamati ya Waamuzi ya TFF kwa ajili ya kuchukuliwa hatua kutokana na tukio hilo.
Kamati ya Mashindano imekumbusha kuwa RCL ni mashindano yanayosimamiwa na TFF, hivyo maelekezo yoyote kuhusiana na mashindano hayo pia yatatoka TFF na si mahali pengine popote. Hivyo, msimamizi wa kituoa hana mamlaka ya kubadili uwanja.
Hatua ya nne ya RCL itachezwa kati ya Juni 23 na 23 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitachezwa kati ya Juni 29 na 30 mwaka huu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
MOYES AWEKA NIA YA DHATI KWA FABREGAS VS LEWANDOWSKI.

Kocha mpya wa United, David Moyes
ametanabaisha kuwa angependa kuwasajili wote.
kiungo wa Barcelona na mshambuliaji wa
Kipoland wa Borussia Dortmund katika klabu yake kabla ya kikosi chake
hakijakwenda katika ziara ya Asia na Australia katikati ya mwezi ujao.
Inafahamika kwamba, wachezaji wote hao
wameonyesha nia zao za kuhamishia cheche zao kwa mabingwa hao wa Ligi
Kuu ya England, hivyo United wanaweza kufanikisha dili hizo.

Robert Lewandowski
Klabu yake ya zamani Fabregas, Arsenal
haijaonyesha nia na malengo ya kumsajili tena iwapo mchezaji huyo mwenye umri
wa miaka 26 ataondoka Nou Camp, lakini United inafahamika wanamtaka kwa
dhati kiungo huyo aliyeichezea kwa miaka nane timu hiyo ya London kabla
ya kurejea Hispania miaka miwili iliyopita.

Lewandowski anaweza kuhamia England baada ya matumaini yake kuhamia kwa mabingwa wapya wa Ulaya, Bayern Munich kukatwa wiki hii.
United wamekuwa wakimfuatilia
mshambuliaji huyo wa Poland kwa miezi kadhaa na wanaamini anaweza
kuzalisha ushindani mzuri kwa Robin van Persie, ambaye atatimiza miaka
30 muda mfupi kabla timu haijaanza kutetea ubingw awake Agosti.
Changamoto: Robin van Persie anaweza kukabiliana na changamoto kubwa mwanzoni mwa msimu ujao Man United
Kuwasili kwake pia kunaweza kukuza
shinikizo kwa Wayne Rooney ambaye ameomba kuondoka Old Trafford tangu
mwishoni mwa msimu uliopita.
Subscribe to:
Posts (Atom)