MWANADADA nyota dunia katika
tenisi kutoka Marekani, Serena Williams ametolewa nje katika michuano ya
Wimbledon baada ya kukubali kipigo kutoka kwa Sabine Lisicki wa
Ujerumani kwa 6-2 1-6 6-4. Williams
ambaye mbali na kupewa nafasi kubwa ya kunyakuwa taji hilo pia alikuwa
bingwa mtetezi wa michuano hiyo aliyonyakuwa mwaka jana. Kwa
upande mwingine bingwa wa zamani wa michuano hiyo Petra Kvitova
alifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya
kumgaragaza Carla Suarez wa Hispania kwa 7-5 6-3. Mashindano
ya Wimbledon mwaka huu yamekuwa sio mazuri kwa nyota wengi wanaoshika
nafasi za juu katika orodha za ubora wa mchezo huo duniani baada ya
Maria Sharapova anayeshika namba mbili kuenguliwa katika mzunguko wa
pili huku Victoria Azarenka anayeshika namba tatu yeye akijitoa baada ya
kupata majeraha.
Tuesday, July 2, 2013
Saturday, June 29, 2013
ARSENAL WAMTAKA KIPA JULIO CESAR WA QPR ILIYOSHUKA DARAJA"
WASHIKA Bunduki wa jiji London Club
ya Arsenal itaangalia uwezekano wa kukamilisha usajili wa kipa namba wa
Brazil na klabu ya Queens Park Rangers, Julio Cesar baada ya Kombe la
Mabara.
Arsene Wenger anataka kipa mzoefu atengeneze ushindani kwa Lukasz Fabianski na Wojciech Szczesny.
Mazungumzo
baina ya wawakilishi wa Cesar na viongozi wa Gunners tayari
yamefanyika, lakini hayajamalizika kwa kuwa kipa huyo yupo kwenye
majukumu ya kimataifa.

ARSENAL sasa inatarajiwa kumaliza dili hilo mara moja tu, baada ya
kubainika Roma ya Italia nayo imeingia kwenye mbio za kuwania saini ya
Cesar.
Kipa
huyo wa kimataifa wa Brazil ambaye yupo huru kuondoka Loftus Road
kufuatia kushuka kwa QPR hadi Championship, anataka kubaki London ambako
amezoea maisha tangu awasili msimu uliopita akitokea Inter Milan.
Na
The Gunners – ambayo inatumai kukamilisha pia usajili wa Gonzalo
Higuain wiki ijayo, baada ya kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti
kufungua njia kwa mshambuliaji huyo kuondoka Hispania – inajiamini dili
hilo litakamilishwa baada ya Fainali ya Kombe la Mabara Jumapili.
Wenger
alitaka kusajili kipa wa Stoke, Asmir Begovic na wa Liverpool, Pepe
Reina lakini, licha ya kuwa na fungu la bajeti ya usajili la Pauni
Milioni 70, kocha huyo wa Arsenal ameona hana sababu ya kutumia fedha
nyingi kwa ajili ya kipa.
Rangers
itasikiliza ofa ya kiasi cha Pauni Milioni 2 kwa Cesar, wakati mshahara
wake wa Pauni 70,000 kwa wiki halitakuwa tatizo kwa The Gunners, ambayo
imetuma waangalia vipaji wake nchini Brazil kumuangalia Cesar
anachokifanya katika Kombe la Mabara.
Pamoja
na mpango wa kuwasajili Cesar na Higuain, The Gunners pia wanataka
kumsajili beki wa Swansea, Ashley Williams na kiungo wa Everton,
Marouane Fellaini. Lakini masuala ya kifedha yanatia saka kama Arsenal itaweza kusajili wachezaji wote hao.
Hadi
sasa, Arsenal imegoma kumpa Fellaini mshahara wa Pauni 100,000 kwa wiki
na pia imeshindwa kufika dau la Pauni Milioni 24 za kumnunua.
Amekosekana? Arsenal inataka kuwasajili Marouane FellainiMBEYA MWENYEJI WA NETIBOLI TENA KWA MARA YA PILI MFULULIZO".
Jiji la Mbeya kwa
mara ya pili mfululizo,litakuwa mwenyeji wa ligi kuu ya
Netiboli taifa ambapo naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Philip Mulugo anatarijiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi kuanzia
Agosti 24 hadi Septemba 7.
Mwenyekiti
wa chama cha Netiboli Mkoa wa Mbeya, Mary Mung’ong’o ameumabia mtandao
huu kuwa ligi hiyo inafanyika kwa mara nyingine kutokana na ombi la
Waziri Mulugo kwa vile ligi hiyo haikuwa imefana, hivyo akaiomba CHANETA
kuwapa Mbeya fursa nyingine ya uwenyeji.
Alisema
maandalizi ya ligi yameanza na kusema zinahitajika sh milioni 16
kufanikisha na kuongeza kuwa hadi sasa, hawajajua timu ngapi zitashiriki
kutokana na jukumu hilo kuwa chini ya Chama cha Netiboli Tanzania
(CHANETA).
Hata
hivyo, mwenyekiti huyo ametoa wito kwa viongozi wa ngazi mbalimbli
wakiwemo wadau wenye mapenzi na mchezo kutoka mkoani hapa kujitoa kwa
hali na mali kuyafanikisha ili yawe chachu ya kukua kwa mchezo huo
nchini kwa maslahi ya vijana na taifa.
Aidha, mwenyekiti huyo alitamtambulisha Nwaka Mwakisu kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo.
Akizungumzia
mashindano hayo, Mwakisu alisema ni fursa kwa watu wa Mbeya kujitangaza
kibiashara kupitia mchezo huo na kufuta makosa yaliyofanyika mwaka
jana.
Alisema
katika kufakisha mashindano hayo, nguvu ya pamoja inahitajika kuanzia
viongozi wa kisiasa, serikari na vyombo vya habari.
MBASPO FC YATWAA UBINGWA WA AIRTEL RISING KWA MKOA WA MBEYA"
Mbaspo
walianza mbio zao za kutwaa ubingwa kwa kutoshana nguvu ya 3-3 dhidi ya
Mbosa siku ya Jumatatu Juni 24 kabla ya kufanya mauaji makubwa ya 6-0
dhidi ya timu dhaifu ya Mbeya Sekondari siku ya Jumanne. Michezo yote
imefanyika kwenye uwanja wa Magereza jijini Mbeya.
Mbosa
walifikisha point nne juzi Jumatano walipoitandika Mbeya Sekondari 3-0
hivyo kumaliza wakiwa na point nne na magoli sita wakati wapinzani wao
Mbaspo wakifikisha jumla ya magoli tisa ya kufunga. Katika mechi ya
juzi, magoli ya Mbosa yalitiwa kwenye kamba na Michael Mwashilanga,
Riziki Juma na Julius Landa.
Wakati
huo huo, chama cha mpira wa miguu mkoa wa Mbeya kimetangaza kikosi cha
wachezaji 18 kuuwakilisha mkoa huo kwenye michuano ya Taifa ya Airtel
Rising Stars inayoanza kutimua vumbi kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 2.
Wachezaji
hao ni Ismail Yesaya, Emmanuel Alex, Gift Sanga, Jackson Mwaibambe,
Boaz Mwangole, Costa Sanga, Seif Zubery, Stanley Angelo, Enock Sikaonga,
Kaunda Malata, Joel Kasimila, Hamprey Nyeo, Elia Salengo, Peter Noah,
Emmaneul Mtimbi, Michael Bosco, Richard Kalinga na Zamoyoni Mwashambwa.
Katika
mkoa wa Morogoro, mji kasoro bahari, timu ya Moro Kids imetoka sare ya
bila kufungana na Techfort katika mchezo wa kushambuliana kwa zamu
uliopigwa kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Morogoro juzi Jumatano
na kushuhudiwa na mashabiki wengi wa mji huo
Airtel
Rising Stars vile vile imeanza kutimua vumbi katika jiji la Mwanza
ambapo timu ya Marsh Athletical imedhihirisha umwambe wake katika soka
baada ya kuifunga Nyamagana United 2-0 kwenye uwanja mkongwe wa
Nyamagana.
Timu
za mikoa zimepangwa kuanza kuwasili jijini Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki tayari kwa ajili ya kindumbwe ndumbwe cha Airtel Rising Stars ngazi
ya taifa katika uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Wachezaji 16
watachaguliwa wakati wa mashindano hayo ili kuunda timu
itakayoiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ya Airtel
Rising Stars. Nchi mwenyeji wa michuano hiyo itatangazwa baadaye mwezi
ujao.
Friday, June 28, 2013
YANGA YAITAKA TFF IWALIPE KABLA JUMAPIL
WAKATI
inasemekana TFF walishalipwa Shilingi Milioni 200 toka kwa Wadhamini wa
Ligi Kuu ya Bara, VODACOM, tangu Mwezi uliopita zikiwa ni Zawadi kwa
Washindi mbali mbali wa Ligi hiyo, Klabu zimelalamika kutolipwa Zawadi
zao na Yanga wametaka walipwe Milioni 70 zao kabla Jumapili.
Zawadi hizo ni kwa ajili ya kumtunukia
Bingwa, Yanga, pia wengine wanaostahili ni ni Azam FC, Simba, Kagera
Sugar pamoja na Wachezaji mbali mbali wakiwemo Kipa Bora, Mfungaji Bora,
ambae ni Kipre Tcheche wa Azam FC, Refa Bora, Kocha Bora na kadhalika.
Hata hivyo, Vodacom inasemekana
wameshatangaza Zawadi hizo zitagawiwa mapema Mwezi ujao na hilo
limegusiwa pia na TFF ambao wamesema wanaandaa Siku maalum ya kutoa
Zawadi hizo ikiwa ni pamoja na kualika Maafisa wa Serikali pamoja na
wale kutoka Wizara husika hasa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo.
Msimu uliopita hata Simba
walicheleweshwa kupata Zawadi yao kama Bingwa baada ya kusubiri karibu
Miezi miwili tangu Ligi imalizike ili kupata Tuzo yao.
Yanga walitwaa Ubingwa wa Ligi Kuu
Vodacom kwa Msimu wa 2012/13 uliomalizka Mwezi Mei lakini wao walitwaa
Ubingwa huo mapema kabla Msimu huo haujafika tamati.
WAWILI WALA SHAVU WACHAGULIWA KITUO CHA VIPAJI ASPIRE
Wachezaji
wawili kutoka Tanzania wamechaguliwa miongoni mwa 50 waliofanyiwa
majaribio nchini Uganda kwa ajili ya kuingia katika kituo cha kuendeleza
vipaji (centre of excellence) kilichoko Doha nchini Qatar kupitia
mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream.
Abdulrasul
Tahir Bitebo (15) ambaye ni mshambuliaji kutoka Kituo cha Uwanja wa
Karume, na Martin Omela Tangazi (14) ambaye ni beki kutoka Kituo cha
Ukonga ndiyo waliochaguliwa kutoka Tanzania kuingia katika kituo ambapo
watakaa kwa mwezi mmoja kabla ya kusaini mkataba rasmi wa kuendelezwa.
Wachezaji
wengine walikuwa wakitoka katika nchi za Uganda na Kenya. Mchezaji
mwingine aliyefuzu katika nafasi tatu zilizokuwepo ni kutoka nchini
Kenya.
Mpango
wa Aspire Football Dream unafadhiliwa na Mtoto wa Mfalme wa Qatar
katika nchi 16 duniani, na kwa hapa nchini uko chini ya Idara ya Ufundi
ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
TFF
ina jumla ya vituo 14 vya kuendeleza vipaji kupitia mpango huo wa
Aspire Football Dream. Vituo hivyo ni Karume, Kigamboni, Tandika, Kawe,
Ukonga, Kitunda, Mbagala, Magomeni, Makongo, na Tabata vilivyo katika
Mkoa wa Dar es Salaam. Vingine ni Bagamoyo kilichopo mkoani Pwani,
Morogoro, Arusha na Moshi mkoani Kilimanjaro.
Kituo kingine cha kuendeleza vipaji (centre of excellence) cha Aspire kipo Dakar nchini Senegal.
TFF KUENDESHA KOZI SITA KATI YA JULAI- SEPTEMBA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litaendesha kozi sita tofauti za mpira wa miguu kati ya Julai na Septemba mwaka huu.
Kozi
hizo ni FIFA 11 For Health itakayofanyika Hombolo mkoani Dodoma kuanzia
Julai 8 hadi 19 mwaka huu. Julai 6 hadi 15 mwaka huu kutakuwa na kozi
ya mpira wa miguu wa ufukweni (Beach Soccer) itakayofanyika jijini Dar
es Salaam.
Waamuzi
wa FIFA nao watakuwa na kozi itakayofanyika kati ya Agosti 22 hadi 26
mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati kozi ya ukocha kwa ajili ya Copa
Coca-Cola itafanyika jijini Dar es Salaam kati ya Agosti 12 na 17 mwaka
huu.
Vilevile kutakuwa na kozi ya mpango
wa grassroots unaolenga wachezaji mpira wa miguu (wasichana na
wavulana) wenye umri kuanzia miaka 6-12 itafanyika kuanzia Septemba 9
hadi 13 mwaka huu jijini Dar es Salaam wakati tamasha (festival) la
grassroots litafanyika Uwanja wa Karume, Septemba 14 mwaka huu.
RCL KUKAMILISHA HATUA YA NNE JUMAPILI
Mechi
za marudiano za hatua ya nne ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL)
zitachezwa Jumapili (Juni 30 mwaka huu) kwenye viwanja vya Sokoine
jijini Mbeya, na Kambarage mjini Shinyanga.
Friends
Rangers ya Dar es Salaam ambayo katika mechi ya kwanza ilifungwa
nyumbani mabao 3-0 itakuwa mgeni wa Stand United FC mjini Shinyanga
wakati Kimondo SC itaikaribisha Polisi Jamii ya Mara jijini Mbeya.
Katika mechi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.
Hatua
ya mwisho ya RCL itachezwa Julai 3 mwaka huu kwa mechi za kwanza wakati
zile za marudiano zitafanyika Julai 7 mwaka huu. Timu tatu za kwanza
zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
MAN UNITED USO KWA USO NDANI YA EVERTON WATAKA KUIBOMOA
Mabingwa wa BPL msimu uliopita Club ya soka ya Manchester
United imeamua kumtengea kitita cha paundi milioni 15 kwa ajili ya
kumnasa beki wa Everton, Leighton Baines. Baada
ya kukataa ofa ya awali ya United ya Pauni Milioni 12, Everton
imesisitiza kuwa beki huyo wa kushoto wa kimataifa wa England hauzwi. Lakini United imepania kupanda dau hadi paundi milioni 20 katika kuwania saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. Mrithi
wa Moyes, Everton, Roberto Martinez anataka kumbakzia beki huyo na
klabu hiyo inataka kumpa mkataba mpya ikimuongezea mshahara hadi paundi
70,000 kwa wiki. Mpango
huu unamuweka shakani beki Mfaransa, Patrice Evra juu ya mustakabali
wake Old Trafford na wazi sasa anaweza kuhamia Monaco au Paris
Saint-Germain.
Subscribe to:
Posts (Atom)






