Mabingwa wa BPL msimu uliopita Club ya soka ya Manchester
United imeamua kumtengea kitita cha paundi milioni 15 kwa ajili ya
kumnasa beki wa Everton, Leighton Baines. Baada
ya kukataa ofa ya awali ya United ya Pauni Milioni 12, Everton
imesisitiza kuwa beki huyo wa kushoto wa kimataifa wa England hauzwi. Lakini United imepania kupanda dau hadi paundi milioni 20 katika kuwania saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. Mrithi
wa Moyes, Everton, Roberto Martinez anataka kumbakzia beki huyo na
klabu hiyo inataka kumpa mkataba mpya ikimuongezea mshahara hadi paundi
70,000 kwa wiki. Mpango
huu unamuweka shakani beki Mfaransa, Patrice Evra juu ya mustakabali
wake Old Trafford na wazi sasa anaweza kuhamia Monaco au Paris
Saint-Germain.