MSHAMBULIAJI nyota wa
kimataifa wa Argentina Lionel Messi ametua nchini Senegal jana kwa ndege
binafsi na kulakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Dakar na mashabiki wa
soka na vijana wadogo waliotoka pembe mbalimbali za nchi hiyo. Nyota
huyo anayecheza katika klabu ya Barcelona alialikwa na shule ya soka ya
Qatar Aspire ambao wana tawi lao nchini humo kwa ajili ya kwenda kwenye
kampeni ya kupiga vita ugonjwa wa malaria. Kwa
mujibu wa waratibu ya ziara hiyo maelfu ya neti ambazo zitakuwa na
picha ya Messi zitasambazwa kwa watoto na familia katika vijiji
mbalimbali nchini humo. Messi
atasafiri kwa helikopta kwenda Saly eneo la karibu na mji wa Dakar
ambapo atatembelea nyumba za yatima na kuongea na wenyeji wa hapo jinsi
watakavyoweza kujikinga na malaria.