Tuesday, July 2, 2013

NEYMAR NA ALBA KUFANYIWA UPASUAJI WA MAFINDIFINDO YA SHIGONI"TOSEZI"


Mkali mpya wa FC Barcelona, Neymar na beki Jordi Alba wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa kuondoa mafindofindo Ijumaa na wanatarajiwa kupona baada ya siku 10. Upasuaji huo ulipangwa kufanyika baada ya fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho iliyofanyika jijini Rio de Janeiro Jumapili iliyopita ambapo Brazil iliisambaratisha Hispania kwa mabao 3-0. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo Neymar anatarajiwa kufanyiwa upasuaji huo huko Rio na baadhi ya madaktari wa Barcelona wanakuwepo kusaidia. Wakati Alba mwenye miaka 24 yeye atafanyiwa upasuaji wake siku hiyohiyo lakini katika kliniki iliyopo karibu na jiji la Barcelona na wote wanatarajiwa kupona ndani siku 10 baada ya upasuaji huo.

ARSENAL SASA YAJIWEKA KAMILI GADO KWA MSIMU MPYA WA BPL NCHINI UINGEREZA"

Wakiwa chini ya kocha Mfaransa, Aserne Wenger Timu ya soka ya Arseanal wamefanikiwa kuinasa saini ya nyota kinda wa kimataifa kutoka nchini Ufaransa, Yaya Sanogo kwa kumpa mkataba mrefu Emirates.
Kinda huyo kwa sasa yupo na timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa chini ya umri wa miaka 20m katika fainali za Kombe la Dunia la vijana chini ya umri wa miaka 20 huku akiwa amefumania nyavu mara mbili kati ya matatu ya timu yake nchini Uturuki.
Akicheza ligi daraja la kwanza nchini Ufaransa, Sanogo  amefunga mabao tisa  katika mechi 13 huku akiandamwa na majeruhi ya mara kwa mara.
Target man: Sanogo has built an excellent reputation for himself in France 
Mtu mwenye dili kwa sasa: Sanogo amejijengee nafasi nzuri sana katika taifa la Ufaransa
More to come? Higuain (left) and Rooney (right) are also thought to be on Wenger's wishlist 
Nyota wengine wa kutua Emirates? Higuain (kushoto) na Rooney (kulia) pia wapo katika rada za Wenger ambaye anataka kupata nyota wakali wa kuimarisha kikosi chake msimu ujao
Gonzalo Higuain na Wayne Rooney wameripotiwa kuwa katika mipango ya Wenger msimu ujao, lakini kocha huyo raia wa Ufaransa amevutiwa na kinda Sanogo.
‘Sanogo ni mchezaji mzuri sana atakayesaini kwetu, ameonesha kiwango kikubwa katika klabu yake ya Auxerre na katika kikosi cha timu ya taifa chini ya umri wa miaka 20″. Alisema Wenger.

MTIBWA SUGAR YAJIPANGA KUJIWEKA SAWA NA MAANDALIZI YA MSIMU MPYA WA LIGI KUU TZ BARA"

Kikosi cha mtibwa sukari
Timu ya Mtibwa Sugar ya manungu turiani ya mkoani morogoro inayonolewa na kocha mzawa Mecky Mexime wanatarajia kujiweka sawa katikati ya mwezi huu wa saba ili kujiandaa na mshikemshike wa msimu mpya waligi kuu soka Tanzania bara unaotarajiwa kuanza Agosti 24.
Mwenyekiti mwenye dhamana ya kuiongoza timu hiyo kubwa nchini Tanzania yenye historia ya kuzisumbua Simba na Yanga na kutwaa taji miaka ya nyuma, Jamal Baiser amesema kwa sasa wanafanya mipango ya kusajili wachezaji wa kuziba nafasi zilizoachwa wazi  kufuatia baadhi ya wachezaji kutimka klabuni hapo.
“Mpaka sasa hatujasajili wachezaji, lakini mipango yetu ni kusajili wachezaji wapatao watano, na baada ya kukamilisha taratibu zote, tutawajulisha mashabiki wetu. Kikubwa ni kwamba, tunahitaji kuwa na timu nzuri zaidi kuliko misimu mitatu iliyopita”. Alisema Baiser.
Baiser alisema kwa muda mrefu sasa,  Mtibwa sugar haifanyi vizuri sana wala vibaya sana, lakini kwa msimu ujao wanajiandaa kuwa timu bora zaidi,  huku wakichanganya damu changa na kongwe katika kikosi chao.
Mwenyekiti huyo alisema timu yao amepoteza baadhi ya wachezaji akiwemo Issa Rashid “Baba Ubaya” aliyejiunga na wekundu wa Msimbazi Simba pamoja na Hussein Javu anayesemekana kusaini yanga, lakini wana wachezaji wengine wa kuziba nafasi zao na wengine watawasajili.
“Walikuwa wachezaji muhimu sana, lakini hatuna jinsi, soka ni ajira yao, hatuna uwezo wa kuwabania nafasi ya kucheza klabu  nyingine, ila kiuhakika tunao wachezaji wengi sana wa kuziba nafasi zao nab ado tunatafuta nyota wengine wa kuwasainisha”. Alisema Baiser.
Akizungumzia suala la Javu kusaini Yanga, Baiser alisema Mtibwa Sugar  ilikuwa na mkataba naye, lakini Yanga waliomba ruhusa ya kuzungumza naye na wao wakakubali.
“Walituomba kuongea na Javu, tuliwaruhusu. Kama wamekubaliana na kumpa mkataba sisi bado hatuna taarifa ofisini, Yanga bado hawajaja kufanya taratibu za uhamishoi, kwahiyo hatujui kama wameshamalizana naye, hivyo sitaki kulizungumzia sana kwa sasa, wakati utafika nitazungumza”. Alisema Baiser.
Baiser alisema Javu alikuwa mchezaji muhimu sana, lakini wanajipanga kutafuta mbadala wake.

WEBB ASEMA WAAMUZI WANAIMANI KUBWA NA MFUMO MPYA WA TEKNOLOGIA YA MSTARI WA GOLI

Howard Webb Mwamuzi wa Uingereza amedai kuwa waamuzi wana imani kubwa na mfumo mpya wa teknologia ya kompyuta katika mstari wa goli ambao utatumika katika michuano ya Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil. Hakuna bao lolote kati ya mabao 68 yaliyofungwa katika michuano ya Kombe la Shirikisho lililohitaji teknologia hiyo ambayo ndio ilikuwa imeanza kutumika kwa mara ya kwanza kwenye michuano hiyo. Lakini Webb aliwaambia waandishi wa habari jijini Rio de Janeiro kwamba uhakika wa mfumo huo unawapa faida kubwa na waamuzi wana imani kwa kiasi kikubwa na mfumo huo ambao umefungwa na kampuni ya Kijerumani iliyoshinda zabuni hiyo ya GoalControl. Webb amesema hawana shaka na uthabiti wa mfumo huo na umeonekana kufanya kazi vyema hivyo anadhani utaendelea kufanya kazi hata katika michuano ya Kombe la Dunia mwakani. Webb ambaye alichezesha mchezo wa fainali kati ya Kombe la Dunia mwaka 2010 kati ya Hispania na Uholanzi nchini Afrika Kusini ni mmoja katika orodha ya waamuzi 52 ambao watachujwa kwa ajili ya michuano hiyo mwakani.

UNDER-20 KOMBE LA DUNIA: RAUNDI YA MTOANO KUANZA KUTIMUA VUMBI

Kazi ipo Kweli Kweli Katika Hatua ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Vijana chini ya Miaka 20, U-20, yanayochezwa huko Nchini Turkey itaanza kutimua vumbi leo Jumanne julai 2 kwa Mechi 4 na Jumatano Mechi za mwisho 4.
FIFA_WORLD_CUP_U-20_TURKEY_LOGORATIBA:
RAUNDI YA MTOANO TIMU 16
Jumanne Julai 2
[Istanbul]
Spain v Mexico [Saa 12 Jioni]
Nigeria v Uruguay [Saa 3 Usiku]
[Gaziantep]
Greece v Uzbekistan [Saa 12 Jioni]
France v Turkey [Saa 3 Usiku]
Jumatano Julai 3
[Saa 12 Jioni]
Portugal v Ghana [Kayseri]
Croatia v Chile [Bursa]
[Saa 3 Usiku]
Colombia v Colombia [Trabzon]
Iraq v Paraguay [Antalya]
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
Washindi wa Raundi hii watatinga Robo Fainali na Afrika imebakiza Timu mbili, Nigeria na Ghana, baada Mali na Egypt kutolewa hatua za Makundi.
RATIBA:
RAUNDI YA MTOANO TIMU 16
37      02/07 18:00 Istanbul Spain v Mexico
38      02/07 18:00 Gaziantep Greece v Uzbekistan
39      02/07 21:00 Istanbul Nigeria v Uruguay
40      02/07 21:00 Gaziantep France v Turkey
41      03/07 18:00 Kayseri Portugal v Ghana
42      03/07 18:00 Bursa Croatia v Chile
43      03/07 21:00 Trabzon Colombia v Colombia
44      03/07 21:00 Antalya Iraq v Paraguay
ROBO FAINALI
45      06/07 18:00 Rize W40 v W38
46      06/07 21:00 Bursa W39 v  W37
47      07/07 18:00 Kayseri W44 v W43
48      07/07 21:00 Istanbul W41 v W42
NUSU FAINALI
49      10/07 18:00 Bursa W45 v  W48
50      10/07 21:00 Trabzon W47 v W46
MSHINDI WA TATU
51      13/07 18:00 Istanbul L49 v L50
FAINALI
52      13/07 21:00 Istanbul W49 v W50

MWAMBUSI ASEMA TUPO TAYARI KWA LIGI KUU TZ BARA MSIMU UJAO.

Baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi kuu tanzania bara kila timu imejipanga sawasawa katika harakati za usajili pamoja na maandalizi Kabambe ya msimu mpya wa ligi kuu  unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu.
Ambapo timu mpya katika ligi kuu na kipenzi kwa wakazi wa jiji la  mbeya Mbeya City ya jijini Mbeya wameanza kujiweka chimbo kujifua chini ya kocha wao mkuu Juma Mwambusi.
Akizungumza na mkali wa dimba Kocha Mwambusi amesema wachezaji kutoka mikoani wameanza kuwasili kuanzia jana, huku akitanabaisha kuwa anajipanga kuongeza wachezaji wachache katika kikosi chake alichotoka nacho  ligi daraja la kwanza msimu uliopita.
“Wachezaji wengi ni walewale, nina mpango wa kuongeza nyota wachache, wengi nitawapandisha kutoka kikosi B, lakini wachezaji wengi waliopandisha timu ligi kuu nimewaacha ila kuna nafasi chache nitaziba hivi karibuni”. Alisema Mwambusi.
Mwambusi amesema katika kikosi chake hana tabia ya kuwapa majina wachezaji kwa kuwapa uhakika wa namba, kwani falsafa yake ni kuchezesha wachezaji wote bila kujali majina yao.
“Mimi siku zote falasafa yangu ni ileile, wachezaji wote wanaofanya vizuri wameweza kupata nafasi hiyo kwa sababu walipewa nafasi ya kucheza, hivyo nitawapa wachezaji wote nafasi ya kucheza ili waongeze uzoefu”. Alisisitiza Mwambusi.
Kuhusu kusajili wachezaji wenye uzoefu mkubwa na mikikimikiki ya ligi kuu, Mwambusi alisema hana mpango wa kusajili wakongwe kutokana na kikosi chake kuwa na vijana wengi ambao wanafanya vizuri.
“Mbeya City ina kikosi bora cha vijana, ninavyozungumza hapa kipo mkoani Iringa wilaya ya Mufindi kushiriki michuano ya kombe la Muungano Mufindi, ni kikosi kizuri sana, kinaongozwa na kocha wangu msaidizi Maka Mwalwisyi ambaye anafanya kazi nzuri. Ni matumaini yangu hawa vijana ni msingi mkubwa wa klabu yangu na watapewa nafasi”.
Mwambusi alisema kikosi chake kinahitaji kujifua kwa nguvu kuhimili mitanannge ya ligi kuu, kwani ligi ya Tanzania bara imekuwa na ushindani mkubwa sana.
“Ligi imebadilika sana, niliifundisha Prisons miaka ya nyuma, sasa naona mambo yamebadilika sana, lakini nina uhakika kwa uzoefu wangu nitajipanga vizuri na kupambana hadi mwisho”. Alisema Mwambusi.
Mbeya City ni miongoni mwa timu tatu zilizopanda ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao, wakati nyingine ni Maafande wa Rhino Rangers ya Tabora, na Ashanti United ya Dar es salaam.
Msimu uliopita timu tatu za Africa Lyon ya Dar es salaam, Toto Africans ya Mwanza na Polisi Morogoro zilishuka daraja na sasa zinaendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi daraja la kwanza.

SERENA WILLIAMS ATOLEWA NJE KATIKA TENESI MICHUANO YA WIMBLEDON

MWANADADA nyota dunia katika tenisi kutoka Marekani, Serena Williams ametolewa nje katika michuano ya Wimbledon baada ya kukubali kipigo kutoka kwa Sabine Lisicki wa Ujerumani kwa 6-2 1-6 6-4. Williams ambaye mbali na kupewa nafasi kubwa ya kunyakuwa taji hilo pia alikuwa bingwa mtetezi wa michuano hiyo aliyonyakuwa mwaka jana. Kwa upande mwingine bingwa wa zamani wa michuano hiyo Petra Kvitova alifanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya kumgaragaza Carla Suarez wa Hispania kwa 7-5 6-3. Mashindano ya Wimbledon mwaka huu yamekuwa sio mazuri kwa nyota wengi wanaoshika nafasi za juu katika orodha za ubora wa mchezo huo duniani baada ya Maria Sharapova anayeshika namba mbili kuenguliwa katika mzunguko wa pili huku Victoria Azarenka anayeshika namba tatu yeye akijitoa baada ya kupata majeraha.