Thursday, February 13, 2014

SIMBA SC :MKUTANO MKUU WA KATIBA MACHI 16.

Mkutano Mkuu wa Marekebisho ya Katiba ya klabu ya Simba umepangwa kufanyika Machi 16 mwaka huu badala ya Machi 23 kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.
Uamuzi wa kurudisha nyuma tarehe ya mkutano huo ulifikiwa jana (Jumatano), katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya Klabu kilichokutana usiku Makao Makuu ya Klabu, Mtaa wa Msimbazi, jijini Dar es Salaam.

Kamati ya Utendaji ya Simba imefikia uamuzi huo kufuatia maelekezo kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), iliyowataka wanachama wake wote mpaka kufikia Machi 20 mwaka huu wawe wameshazifanyia marekebisho katiba zao kwa kuweka kipengele kinachoitambua Kamati za Maadili.

Simba ilipokea barua hiyo na kwa kuzingatia umuhimu huo Uongozi ukaamua kuifanyia kazi kwa kuitisha Mkutano Mkuu ambapo agenda itakuwa ni moja tu nayo ni marekebisho ya katiba.

Mbali na kipengele hicho mkutano huo pia utajadili mapendekezo yote ya marekebisho ya katiba yaliyowasilishwa kwa uongozi ili kujadiliwa na kutolewa maamuzi.

Uongozi wa Simba unawataka wanachama wake kujitokeza kwa wingi siku hiyo kushiriki katika zoezi hilo kwa maslahi ya klabu yao.

Kwa sasa uongozi unafanya mipango ya kutafuta mahali pazuri utakapofanyika mkutano huo na mara baada ya kupatikana basi uongozi utawatangazia wanachama wake.

Asha Muhaji

Ofisa Habari, Simba Sports Club

OKWI APATA KIBALI CHA FIFA KUKIPIGA YANGA

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limeruhusu mshambuliaji Emmanuel Okwi kuichezea Yanga Taariifa za uhakika kutoka ndani ya TFF ambazo zimethibistishwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo, Mwesigwa Celestine zimesema kuwa Okwi sasa ni huru. 
Kweli hilo tumetaarifiwa lakini tutalizungumzia baadaye,” alisema.  
TFF ndiyo ilisimamisha usajili wa Okwi kwa madai ya kutaka ufafanuzi kutokana na kesi tatu za kimsingi kati ya Okwi, Etoile du Sahel. 
Sasa Okwi atakuwa huru kuanza kuitumikia Yanga ambayo imesamjili kwa dau la zaidi ya dola 100,000 (Sh milioni 160).

TWIGA STAR YAFIKA SALAMA LUSAKA ZAMBIA.

Kikosi cha wachezaji 19 wa Twiga Stars kimetua Lusaka, Zambia leo (Februari 13
mwaka huu) huku Kocha Mkuu Rogasian akiahidi ushindani kwenye mechi dhidi
ya wenyeji itakayochezwa Uwanja wa Nkoloma.
Kocha Kaijage aliwaambia waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Kenneth Kaunda mara baada ya kikosi chake kutua kwa ndege ya
Fastjet saa 3.30 asubuhi kwa saa za Zambia kuwa wamekuja kushindana, na si kushiriki.
Twiga Stars ambayo mara ya mwisho ilikutana na Zambia kwenye michuano ya
COSAFA miaka miwili iliyopita na kuibuka na ushindi imefikia hoteli ya Golden
Peacock, na katika uwanja wa ndege ilipokewa na viongozi wa Chama Soka
Zambia (FAZ) na Ofisa Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia, Jeswald Majuva.
Timu hiyo leo saa 9 alasiri kwa saa za Zambia ambapo Tanzania ni saa 10 jioni
itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Nkoloma ambao ndiyo utakaotumika kwa
mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) itakayochezwa kesho.
Wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho ni Amina Ali, Anastazia Katunzi, Asha
Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe Mlenzi, Everine Sekikubo, Fatuma
Issa, Fatuma Makusanya, Fatuma Mwisendi, Fatuma Omari, Happiness Mwaipaja,
Maimuna Mkane, Mwapewa Mtumwa, Sherida Boniface,Sophia Mwasikili, Therese
Yona, Vumilia Maarifa na Zena Said.

MESSI AWEKA REKODI FC BARCA JANA ATUPIA 1

Mshambuliaji mahiri wa argentina na club ya barcelona Lionel Messi amefanikiwa kuweka rekodi nyingine ya mabao wakati Barcelona ikitinga fainali ya Kombe la Hispania kuelekea mechi na Manchester City wiki ijayo Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Messi alifanikiwa kuifungia timu yake jana katika sare ya 1-1 na Real Sociedad na kufikisha mabao 335 hivyo kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika klabu hiyo ya Hispania.

Barca imeingia fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1 baada ya awali kushinda 2-0 na sasa itakutana na Real Madrid katika mechi ya kuwania Kombe.
COPA del REY
NUSU FAINALI

{Saa za Bongo}

Marudiano

Jumanne Februari 11

Atletico de Madrid 0          Real Madrid CF 2 {0-5}

Jumatano Februari 12

Real Sociedad 1 FC Barcelona 1 {1-3}

FAINALI

Aprili 19

Real Madrid v Barcelona

LIVER YAICHAPA FULHAM 3-1-TOURE AENDELEA KUJIFUNGA:

Timu ya Liverpool imefanikiwa kupanda hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kuifunga mabao 3-2 Fulham jana usiku .

Kolo Toure alijifunga dakika ya nane kuipatia Fulham bao la kwanza na Richardson akaifungia timu hiyo bao la pili dakika ya 63.

Mabao ya Liverpool yalifungwa na Daniel Sturridge dakika ya 41, Coutinho dakika ya 40 na mkongwe Steven Gerrard dakika ya 90 kwa penalti.

Liverpool sasa imetimiza pointi 53 baada ya kucheza mechi 26 na inabaki nafasi ya nne.
MATOKEO
Jumatano Februari 12
Arsenal 0 Man United 0

Everton v Crystal Palace {Imeahirishwa}

Man City v Sunderland     {Imeahirishwa}

Newcastle 0 Tottenham 4

Stoke 1 Swansea 1

Fulham 2 Liverpool 3

MSIMAMO:TIMU

NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Chelsea 26 17 6 3 48 21 27 57
2 Arsenal 26 17 5 4 48 26 22 56
3 Man City 25 17 3 5 68 27 41 54
4 Liverpool 26 16 5 5 66 32 34 53
5 Tottenham 26 15 5 6 36 32 4 50
6 Everton 25 12 9 4 37 26 11 45
7 Man United 26 12 6 8 41 31 10 42
8 Southampton 25 10 9 7 37 29 8 39
9 Newcastle 26 11 4 11 32 38 -6 37
10 Swansea City 26 7 7 12 33 36 -3 28
11 West Ham 26 7 7 12 28 33 -5 28
12 Aston Villa 26 7 7 12 27 36 -9 28
13 Hull 26 7 6 13 25 31 -6 27
14 Stoke 26 6 9 11 27 41 -14 27
15 Crystal Palace 25 8 2 15 18 34 -16 26
16 Norwich 26 6 7 13 19 39 -20 25
17 West Brom 26 4 12 10 30 38 -8 24
18 Sunderland 25 6 6 13 25 38 -13 24
19 Cardiff 26 5 7 14 19 44 -25 22
20 Fulham 25 6 2 18 26 58 -32 20
    TAZAMA MAPUNGUFU YA TOURE
Mchoro Kuhusu Toure Jinsi ilivyo Kuwa
TOURE AKIJIFUNGA

RAGE ASEMA APOKEA BARUA TATU TOKA FIFA-IPO YA OKWI

SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa), limetuma barua tatu tofauti kwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, moja ikiwa ni ile inayomhusu Emmanuel Okwi ambaye sasa yuko Yanga.

Moja ya barua ambazo Rage amepewa kopi na Fifa ni ile ambayo Shirikisho la Soka la Uganda (Fufa), limemuomba Okwi kurejea Uganda na kuitumikia timu ya taifa katika michuano ya kimataifa.
Pamoja na barua hiyo, Rage amethibitisha kupokea barua hizo tatu kutoka Fifa ikiwemo ile ya Etoile du Sahel ya Tunisia kuomba kuongezewa muda wa kulipa deni la dola 300,000 wanazodaiwa na Simba kutokana na mauzo ya Okwi.
“Kweli nimepokea barua hizo, moja ni ile ambayo Etoile ambao mwezi huu ndiyo ulikuwa mwisho kulipa dola 300,000, sasa wameomba waongezewe muda hadi Septemba, mwaka huu ili waweze kulipa.
“Fifa wao wamenitumia kopi lakini barua hiyo ni kutoka kwao Etoile kwenda Fifa na wamethibitisha kwamba ni kweli Simba inawadai,” alisema Rage.
Barua ya tatu kati ya hizo kwa mujibu wa Rage ni ile ambayo inaonyesha namna klabu hiyo ya Tunisia ilivyomshitaki Okwi kwa Fifa kutokana na kuonyesha kukiuka mambo kadhaa wakati akijua mkataba wake nao unamalizika mwaka 2016.
“Katika ile barua ya kuhusiana na suala la kulipa, Fifa wametaka tusaini na kukubali kwamba sasa mwisho utakuwa Septemba 30 na tayari barua hiyo nimeikabidhi kwa Hans Pope,” aliongeza Rage.
Tayari Okwi yuko nchini na Yanga imemsajili ingawa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeamua kusimamisha usajili wake hadi litakapopata ufafanuzi kuhusiana na usajili wake.
Wakati Fifa ilitoa kibali kwa Okwi kucheza SC Villa ya Uganda kwa miezi sita, lakini Yanga ikamnunua na kuingia naye mkataba wa miaka miwili, suala ambalo limezua mzozo mkubwa huku Simba wakiendelea kusisitiza kulipwa fedha zao ambazo mwanzo walimuuza na hawakulipwa. 
Okwi amekuwa akisisitiza kwamba anataka kuichezea Yanga ambayo imemsajili, huku akieleza amekuwa akiumia moyoni kuona wenzake wakicheza naye akiwa jukwaani kama mtazamaji.
SOURCE: CHAMPIONI

KOCHA TWIGA STAR ASEMA WAPO VIZURI VS ZAMBIA

Kocha Mkuu wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage amesema kikosi chake kiko tayari kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Zambia itakayochezwa keshokutwa (Ijumaa) jijini Lusaka.
Akizungumza kwenye hafla ya kuiaga timu hiyo iliyofanyika leo (Februari 12 mwaka huu) kwenye ofisi za TFF jijini Dar es Salaam, Kocha Kaijage amesema wachezaji wake wako vizuri, ingawa hakuwa tayari kutoa ahadi kuhusu matokeo.
“Vijana wako vizuri, lakini sitaki kutoa ahadi. Watanzania watuombee, watuunge mkono ili tuweze kufanya vizuri,” amesema Kocha Kaijage katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi.
Twiga Stars inaondoka na kikosi cha wachezaji 19 na benchi la ufundi lenye watu watano kwa ndege ya Fastjet kwa ajili ya mechi hiyo itakayooanza saa 9 kamili kwa saa za Zambia. Msafara wa timu hiyo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Wachezaji waliopo kwenye kikosi hicho chini ya nahodha Sophia Mwasikili ni Amina Ali, Anastazia Katunzi, Asha Rashid, Donisia Minja, Esther Chabruma, Etoe Mlenzi, Everine Sekikubo, Fatuma Issa, Fatuma Makusanya, Fatuma Mwisendi, Fatuma Omari, Happiness Mwaipata, Maimuna Mkane, Mwapewa Mtumwa, Sherida Boniface, Therese Yona, Vumilia Maarifa na Zena Said.
Wakati huo huo, timu ya Azam imeondoka leo alfajiri (Februari 12 mwaka huu) kwenda Beira, Msumbiji kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho dhidi Ferroviario da Beira itakayochezwa Jumamosi. Msafara wa timu hiyo unaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, James Mhagama.

Naye mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Nassib Ramadhan ataongoza msafara wa timu ya Yanga inayoondoka kesho mchana kwenda Comoro kwa ajili ya mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Komorozine itakayochezwa Jumamosi.