Mshambuliaji mahiri wa argentina na club ya barcelona Lionel Messi amefanikiwa kuweka rekodi nyingine ya mabao wakati Barcelona ikitinga
fainali ya Kombe la Hispania kuelekea mechi na Manchester City wiki
ijayo Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Messi alifanikiwa kuifungia timu yake jana katika sare ya 1-1 na Real Sociedad na kufikisha mabao 335 hivyo kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika klabu hiyo ya Hispania.
Barca
imeingia fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1 baada ya awali
kushinda 2-0 na sasa itakutana na Real Madrid katika mechi ya kuwania
Kombe.
NUSU FAINALI
{Saa za Bongo}
Marudiano
Jumanne Februari 11
Atletico de Madrid 0 Real Madrid CF 2 {0-5}
Jumatano Februari 12
Real Sociedad 1 FC Barcelona 1 {1-3}
FAINALI
Aprili 19
Real Madrid v Barcelona