Saturday, February 15, 2014

YANGA KUTUPA KARATA LEO VS KOMOROZINE.


YANGA SC Mabingwa wa Tanzania Bara, jioni ya leo wanashuka dimbani kucheza mechi yao ya mwisho ya Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji Komorozine mjini Moroni.
Katika me

chi ya kwanza Yanga SC walishinda mabao 7-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Wacomoro Dar es Salaam Jumapili na leo wanatakiwa kumalizia vyema kazi yao dhidi ya timu hiyo dhaifu.
Endapo Yanga SC itafanikiwa kukamilisha vyema matokeo ya Randi ya Awali, basi itakutana na mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misiri katika Raundi ya Kwanza. 

BALOTELI AIPA MILAN BAO LA DAKIKA ZA LALA SALAMA

Kunako dakika za  lala salama Mario Balotelli amefanikiwa kuipatia AC Milan ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Bologna katika mchezo wa Serie A usiku wa jana.
Balotelli alifunga bao lake  la 10 msimu huu kwa shuti la umbali wa mita 30 dakika nne kabla ya filimbi ya mwisho na kuipandisha Milan hadi nafasi ya 10 ikifikisha pointi 32 sawa na Lazio iliyo nafasi ya tisa.
SERIE A
RATIBA/MATOKEO:
Ijumaa Februari 14
AC Milan 1 Bologna 0
[Saa za Bongo]
Jumamosi Februari 15
2245 ACF Fiorentina v Inter Milan
Jumapili Februari 16
1430 Calcio Catania v SS Lazio
1700 Atalanta BC v Parma FC
1700 Juventus FC v AC Chievo Verona
1700 Cagliari Calcio v AS Livorno Calcio

1700 Genoa CFC v  Udinese Calcio
1700 US Sassuolo Calcio v SSC Napoli
2245 AS Roma v UC Sampdoria
Jumatatu Februari 17
2245 Hellas Verona FC v Torino FC
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Juventus FC 23 19 3 1 56 18 38 60
2 AS Roma 22 15 6 1 45 11 34 51
3 SSC Napoli 23 14 5 4 47 27 20 47
4 ACF Fiorentina 23 13 5 5 42 24 18 44
5 Inter Milan 23 9 9 5 40 27 13 36
6 Hellas Verona 23 11 3 9 39 37 2 36
7 Torino FC 23 8 9 6 36 30 6 33
8 Parma FC 22 8 9 5 32 27 5 33
9 AC Milan 24 8 8 8 37 35 2 32

TWIGA STARS YA TANZANIA YALALA 2-1 ZAMBIA

Twiga Stars imepoteza mechi ya kwanza ya raundi ya kwanza kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wanawake (AWC) baada ya leo kufungwa mabao 2-1 na Zambia (Shepolopolo) kwenye Uwanja wa Nkoloma jijini Lusaka.

Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika katika mechi hiyo iliyochezeshwa na mwamuzi Salma Mukansanga timu hizo zilikuwa suluhu.

Wenyeji ndiyo walianza kupata bao lililofungwa na Hellen Mubanga dakika ya 75. Mfungaji huyo aliyeingia kipindi cha pili nchini alimalizia wavuni mpira uliotemwa na kipa Fatuma Omari.

Dakika nne baadaye Zambia ambao walikuwa wakishangiliwa kwa nguvu na washabiki wao baada ya kufunga la kwanza, walipata bao la pili ambalo nahodha wa Twiga Stars, Sophia Mwasikili alijifunga mwenyewe.

Mwasikili alikuwa akijaribu kutoa nje mpira uliopigwa na nahodha wa Shepolopolo, Mupopo Kabange ambapo ulipishana na kipa Fatuma Omari kabla ya kujaa wavuni.

Bao la Twiga Stars lilifungwa na Donisia Daniel dakika ya 90. Beki huyo wa kushoto ambaye pia ni mchezaji wa Tanzanite alipanda mbele kuongeza mashambulizi ambapo akiwa nje ya eneo la hatari alipiga shuti lililomshinda kipa Hazel Nali.

Akizungumza baada ya mechi, Kocha wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage alisema amebaini upungufu katika kikosi chake ambao ataufanyia kazi kabla ya mechi ya marudiano ili timu yake iweze kusonga mbele.

“Kwa matokeo haya bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi ya marudiano nyumbani na kusonga mbele,” alisema Kaijage.

Twiga Stars iliwakilishwa na Fatuma Omari, Fatuma Bashiru, Donisia Daniel, Fatuma Issa, Evelyn Sekikubo, Sophia Mwasikili, Vumilia Maarifa, Mwapewa Mtumwa/Amina Ali, Asha Rashid, Etoe Mlenzi/Zena Khamis na Shelida Boniface.

Timu hiyo inarejea nyumbani kesho kwa ndege ya Fastjet ambapo itatua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7 kamili mchana.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
+260 976375482
Lusaka, Zambia

Friday, February 14, 2014

VPL: KAZI IPO MBEYA CITY YAJIPANGA KUMUUWA MNYAMA SIMBA DIMBANI SOKOINE KESHO J"MOSI


RATIBA:
Jumamosi Februari 15

Rhino Rangers v Mgambo JKT

Ashanti United v Kagera Sugar

Mtibwa Sugar v Tanzania Prisons

JKT Oljoro v JKT Ruvu

Mbeya City v Simba

Ruvu Shooting v Coastal Union

­­
MSIMAMO:

NA TIMU P W D L GD PTS
1 Azam FC 16 10 6 0 19 36
2 Yanga SC 16 10 5 1 22 35
3 Mbeya City 17 9 7 1 10 34
4 Simba SC 17 8 7 2 17 31
5 Coastal Union 17 4 10 3 4 22
6 Ruvu Shooting 16 5 7 4 2 22
7 Mtibwa Sugar 17 5 7 5 0 22
8 Kagera Sugar 17 5 7 5 0 22
9 JKT Ruvu 16 6 0 10 -8 18
10 Ashanti UTD 16 3 4 9 -14 13
11 JKT Oljoro 17 2 7 8 -14 13
12 Mgambo 17 3 4 10 -18 13
13 Rhino Rangers 17 2 6 9 -10 12
14 Prisons FC 14 1 7 6 -10 10

RATIBA MECHI ZIJAZO:

Jumatano Februari 19

Tanzania Prisons v JKT Ruvu

Jumamosi Februari 22

Ruvu Shooting v Yanga

Kagera Sugar v Rhino Rangers

Mtibwa Sugar v Ashanti United

Coastal Union v Mbeya City

JKT Oljoro v Mgambo JKT

Azam FC v Tanzania Prisons

Jumapili Februari 23

Simba v JKT Ruvu

CHAMAZI NDIO HABARI YA MJINI-YANGA YAKUBALI KUWEKA KAMBI"

Dimba la Uwanja wa Azam Complex Chamazi
Yanga SC Kupitia Uongozi wake umetanabisha kuwa upo tayari kuweka kambi Chamazi kufuatia ofa waliyoitoa Azam ya kuwataka wakaweke kambi maeneo hayo kwa ajili ya kujiweka sawa na mchezo wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri.
KAama unakumbuka wiki iliyopita uongozi wa Azam FC ulikataa ombi la Al Ahly kuweka kambi kwenye eneo lao hilo wakati watakapokuja nchini kucheza dhidi ya Yanga katika hatua hiyo baada ya kufanikiwa kuitoa Komorozine ya morroco.
Wachezaji Wa Yanga Wakiwa Katika Swimming Pool
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Bin Kleb amesema hawawezi kuiachia ofa kama hiyo kwa kuwa mtazamo wao ni kuona wanafanikiwa kufanya vizuri katika mechi hiyo.
"Katika hali ya kawaida hakuna mtu anaeweza kukataa ofa kama hiyo, iwapo Azam wameamua kutusaidia sisi tupo tayari ila tunamsikiliza upande wa benchi la ufundi kupitia Kocha Mkuu mwalimu Hans Van Pluijm anahitaji kambi ya aina gani ili kuweza kujiandaa.
"Hata hivyo Bin Kleb amesema Kocha ndiye anayejua aina ya timu anayotarajia kukutana nayo, hivyo uongozi unamwachia kila kitu na yeye ndiye atakayetoa maamuzi.

TFF YAWATAKA WANACHAMA WAKE KUFAVYA MAREKEBISHO YA KATIBA KABLA YA MACHI 20

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeamuru wanachama wake wote kufanya marekebisho ya katiba zao kabla ya Machi 20, mwaka huu, hivyo kutengua tarehe ya mkutano mkuu wa Simba.

Simba iliyo chini ya mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage, ilipanga kufanya mkutano wake huo Machi 23, mwaka huu kwa ajenda moja ya marekebisho ya katiba yao ambapo sasa imeamua kufanya mkutano huo mapema, Machi 16 ili kwenda sawa na maagizo ya TFF.
Ofisa Habari wa Simba, Asha Muhaji alisema kuwa walitumiwa barua ya maagizo hayo na TFF wiki hii na hivyo wameamua kuurudisha nyuma ili marekebisho hayo yafanyike kabla ya Machi 20.
“Mkutano wa marekebisho hautafanyika tena Machi 23 kama wanachama na wadau wote wa Simba walivyokuwa wakifahamu, tumepata barua kutoka TFF inayotuelekeza kufanya mkutano huo kabla ya Machi 20, hivyo sasa mkutano utakuwa Machi 16.

NAPE ATOFAUTIANA NA JAJI WARIOBA BUNGE LA KATIBA.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye, amesema Bunge Maalumu la Katiba, litatekeleza majukumu yake kwa kufuata Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na si mawazo ya mtu yeyote.
Kauli hiyo ya Nape imekuja siku moja baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kusema kuwa litakuwa jambo lisilo la kawaida kwa Bunge hilo kubadili hoja ya msingi iliyopo kwenye Rasimu ya Katiba, akisisitiza kuwa jukumu lake ni kuifanyia marekebisho.
Warioba alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza katika mkutano ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), kuhusu tafakuri na maridhiano kuelekea katika Katiba Mpya.
Alisema kama Bunge Maalumu la Katiba likipewa jukumu la kuandika Katiba linaweza kubadili mambo mengi, lakini kama Katiba itakuwa imeandaliwa na chombo kingine, Bunge hilo linatakiwa kutobadili hoja za msingi.
Akizungumza na gazeti hili jana, Nape alisema: “Mchakato wote wa Katiba Mpya unasimamiwa na sheria na sio maneno ya Warioba. Sheria inazungumzia haki, wajibu na mamlaka ya Bunge hilo, hivyo inawezekana kabisa kuboreshwa na hata kubadilishwa kwa hoja.”
Nape alisema kulingana na sheria hiyo, Bunge hilo lina mamlaka ya kufanya jambo lolote katika Rasimu hiyo, ikiwa ni pamoja na kuifanyia maboresho kadri itakavyoonekana kuwa inafaa.
“Bunge haliwezi kutishwa na mtu yeyote kwa sababu lipo kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi. Ndiyo maana baada ya Bunge hilo kwisha wananchi watapiga kura ya maoni,” alisema.
Akitolea ufafanuzi kauli ya Jaji Warioba kwamba Bunge hilo lifanye maboresho na si kubadili hoja za msingi, Nape alisema: “Maboresho maana yake ni kubadili. Ukiwa na nyumba ya vyumba vinne na kuiboresha kwa kuweka chumba kimoja si umeibadili?”
Alisema Bunge hilo linatakiwa lisiingiliwe katika uamuzi wake.
Chanzo:Mwananchi".