
Simba
iliyo chini ya mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage, ilipanga kufanya mkutano wake
huo Machi 23, mwaka huu kwa ajenda moja ya marekebisho ya katiba yao ambapo
sasa imeamua kufanya mkutano huo mapema, Machi 16 ili kwenda sawa na maagizo ya
TFF.

“Mkutano
wa marekebisho hautafanyika tena Machi 23 kama wanachama na wadau wote wa Simba
walivyokuwa wakifahamu, tumepata barua kutoka TFF inayotuelekeza kufanya
mkutano huo kabla ya Machi 20, hivyo sasa mkutano utakuwa Machi 16.