Friday, February 14, 2014

CHAMAZI NDIO HABARI YA MJINI-YANGA YAKUBALI KUWEKA KAMBI"

Dimba la Uwanja wa Azam Complex Chamazi
Yanga SC Kupitia Uongozi wake umetanabisha kuwa upo tayari kuweka kambi Chamazi kufuatia ofa waliyoitoa Azam ya kuwataka wakaweke kambi maeneo hayo kwa ajili ya kujiweka sawa na mchezo wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri.
KAama unakumbuka wiki iliyopita uongozi wa Azam FC ulikataa ombi la Al Ahly kuweka kambi kwenye eneo lao hilo wakati watakapokuja nchini kucheza dhidi ya Yanga katika hatua hiyo baada ya kufanikiwa kuitoa Komorozine ya morroco.
Wachezaji Wa Yanga Wakiwa Katika Swimming Pool
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Bin Kleb amesema hawawezi kuiachia ofa kama hiyo kwa kuwa mtazamo wao ni kuona wanafanikiwa kufanya vizuri katika mechi hiyo.
"Katika hali ya kawaida hakuna mtu anaeweza kukataa ofa kama hiyo, iwapo Azam wameamua kutusaidia sisi tupo tayari ila tunamsikiliza upande wa benchi la ufundi kupitia Kocha Mkuu mwalimu Hans Van Pluijm anahitaji kambi ya aina gani ili kuweza kujiandaa.
"Hata hivyo Bin Kleb amesema Kocha ndiye anayejua aina ya timu anayotarajia kukutana nayo, hivyo uongozi unamwachia kila kitu na yeye ndiye atakayetoa maamuzi.