Tuesday, February 18, 2014

VPL:KESHO PRISON KUTUPA KARATA YAKE VS JKT RUVU

UWANJA wa Sokoine huko Jijini Mbeya, Kesho unatarajiwa kuchukua Nafasi kwa pambano la VPL, Ligi Kuu Vodacom, ambapo Wenyeji Tanzania Prison wakishuka dimbani kuvaana  na Jkt Ruvu Kutoka Kibaha Mkoani pwani.VPL_2013-2014-FP
Tanzania Prison watashuka dimbani kuhakikisha wanapata alama tatu muhimu ili Kujiweka mahala Pazuri kuepuka Janga la kushaka daraja.
a,mbapo kwa sasa Katika msimamo wa VPL Prison ipo Nafasi ya pili kutoka mwisho ikiwa na Alama 13 huku mpinzani wake akiwa katika Nafasi ya 9 na alama 19a Magoli.
­­

MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
PTS
1
Azam FC
16
10
6
0
19
36
2
Yanga SC
16
10
5
1
22
35
3
Mbeya City
18
9
8
1
10
35
4
Simba SC
18
8
8
2
17
32
5
Ruvu Shooting
17
6
7
4
3
25
6
Kagera Sugar
18
5
8
5
0
23
7
Coastal Union
18
4
10
4
3
22
8
Mtibwa Sugar
18
5
7
6
-1
22
9
JKT Ruvu
17
6
1
10
-8
19
10
Ashanti United
17
3
5
9
-14
14
11
JKT Oljoro
18
2
8
8
-14
14
11
Mgambo
18
3
5
10
-18
14
14
Prisons FC
15
2
7
6
-9
13
12
Rhino Rangers
18
3
6
9
-10
13

RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumatano Februari 19
Tanzania Prisons v JKT Ruvu
Jumamosi Februari 22
Ruvu Shooting v Yanga
Kagera Sugar v Rhino Rangers
Mtibwa Sugar v Ashanti United
Coastal Union v Mbeya City
JKT Oljoro v Mgambo JKT
Azam FC v Tanzania Prisons
Jumapili Februari 23
Simba v JKT Ruvu

KATIBU MKUU WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII AKEMEA DAWA ZA KULEVYA

KATIBU Mkuu wa wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na watoto Anna Maembe ametaka vijana vijana nchini kuachana kabisa na biashara ya dawa za kulevya kwani inawasababishia matatizo makubwa katika maisha yao badala yake wajiunge na kutengeneza vikundi vya kijasiriamali ili serikali iweze kuwasaidia kujikwamua kimaisha na kufikia ndoto zao.
Katibu Mkuu Anna Maembe akisalimiana na akina mama wanakikundi cha kutunza Mazingira katika kata ya Matai wilayani Kalambo Mkoani Rukwa jana. PICHA ZOTE NA RAMADHANI JUMA
Amesema takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa, zaidi ya vijana 500 wa Kitanzania wako kizuizini katika nchini tofauti duniani walikokamatwa wakisafirisha dawa hizo, huku vijana wengine wapatao 100 wakiwa wamehukumiwa kunyongwa nchini China.
Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na makundi mbalimbali ya kijamii wakati wa ziara yake katika kata ya Matai wilayani Kalambo Mkoa wa Rukwa jana, ambapo alisema biashara hiyo inachafua sana jina la Tanzania katika Jumuia ya Kimataifa kutokana na idadi kubwa ya vijana kujihusisha na biashara hiyo.
Akizungumzia sera ya Jinsia inayotekelezwa na wizara yake, Katibu Mkuu huyo alisema haina lengo la kuwafanya wanawake kuwatunishia misuli wanaume katika familia bali ni kuwawezesha wanawake kushiriki katika uzalisha na kukuza kipato cha familia na taifa  kwa ujumla ili kukabiliana na gharama za maisha ambazo zimepanda sana kwa sasa.
Vilevile alitoa wito kwa wazazi kuhakikisha wanatenga muda wa kukaa na kuzungumza na watoto ili kujua changamoto zinazowakabili ikiwemo unyanyasaji wa kijinsi na kisaikolojia wanazokumbana nazo na pia kuwapatia haki zao za kimsingi kama elimu, afya na kusikilizwa kama  ambavyo sera ya watoto hapa nchini inavyoelekeza.
Katika kuimarisha vikundi vya wanawake mkoani Rukwa, katibu mkuu Maembe ametoa shilingi milioni 43 kutoka katika wizara yake, ambapo vikundi kutoka katika Halmashauri za wilaya ya Nkasi, Kalambo, Sumbawanga Vijijini na Manispaa vitanufaika kwa mtindo wa wanachama wa vikundi hivyo kupatiwa mikopo kwa ajili ya kutekeleza shughuli zao za kiuchumi.
                                 Na Ramadhani Juma,
                   Afisa Habari Ofisi ya Mkurugenzi -Kalambo

LOGARUSIC NITAFANYA KWELI MSIMBAZI KUHUSU WACHEZAJI"L

Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic, amesema matokeo mabaya ya timu hiyo katika mechi za Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara ambayo iko hatua ya lala salama yanatokana na kuwa na baadhi ya wachezaji wasio na viwango 'mizigo'.

Logarusic alisema ili kikosi chake kiweze kurejea katika ushindani atawatema kwenye programu zake wachezaji hao ambao amewakuta wameshasajiliwa.

Hata hivyo, kocha huyo raia wa Croatia, hakuwa tayari kuwataja majina nyota hao wanaomwangusha katika mechi za ligi na kusababisha timu yao kuendelea kukaa kwenye nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu.

Baadhi ya wachezaji ambao wanadaiwa wamekuwa wakifanya 'ndivyo sivyo' na kumchanganya kocha huyo ni pamoja na Betram Mwombeki, Uhuru Selemani na Zahor Pazi ambaye Jumamosi jijini Mbeya aliingia kuchuka nafasi ya Haroun Chanongo katika dakika ya 54 na kupoteza nafasi zaidi ya tatu za kuifungia Simba na kufanya mechi hiyo imalizike kwa sare ya 1-1.

Baada ya mechi ya ugenini dhidi ya Mbeya City, Logarusic, alisema kwamba ubingwa wa ligi bado uko wazi na ili Simba iweze kurejesha matumaini ya kumaliza katika nafasi za juu ni lazima mabingwa watetezi, Yanga, Azam na Mbeya City zilizoko juu yake zifanye vibaya kwenye mechi zao.

Simba yenye pointi 31 huku ikiwa katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, jana jioni ilianza mazoezi kwenye Uwanja wa Kinesi, Sinza kwa ajili ya kujiandaa na mechi yake itakayofanyika Jumapili, Februari 23, mwaka huu dhidi ya JKT Ruvu.

Yanga ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania waliobakia katika mashindano ya kimataifa ndio mabingwa watetezi wa ligi wakati Azam ndio vinara wakiwa na pointi 36 wakifuatiwa na Yanga wenye pointi 35 na Mbeya City wakiwa na pointi 34 ni watatu.

MNYIKA: WADAU WASHIRIKISHWE KUTUNGA KANUNI ZA BUNGE LA KATIBA.

Mbunge  wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), amesema atawasilisha mapendekezo ya kutaka ratiba ya Bunge Maalumu la Katiba ibadilishwe, ili wadau washirikishwe kwenye mchakato wa kutunga kanuni za Bunge hilo.

Mnyika alisema hayo kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari jana.

Alisema  ratiba iliyotolewa inaonyesha kwamba baada ya kusomwa kwa tangazo la kuitisha Bunge hilo na uchaguzi wa mwenyekiti wa muda, kazi ya kutunga kanuni itaanza.

Mnyika alisema kanuni ndiyo msingi wa kufikia mwafaka wa kuboresha rasimu ya Katiba badala ya kuchakachua na kwamaba ili zisitungwe kanuni mbovu ipo haja ya wadau wote wanaohusika na mchakato wa Katiba mpya ndani na nje ya Bunge kushiriki.

“Nakusudia kuwasilisha mapendekezo kwamba ratiba  ya Bunge ifanyiwe mabadiliko ili kuwapo na kikao cha kusikiliza umma (Public hearing), juu ya kanuni hizo ili mawazo ya wadau yazingatiwe katika maandaluzi ya kanuni kabla ya Bunge kupitisha azimio la kuridhia kanuni hizo,” alisema Mnyika.

Aidha, alisema atawasiliana na Katibu wa Bunge na Katibu wa Baraza la Wawakilishi au Mwenyekiti wa muda atakayechaguliwa ili kanuni zisitolewe nakala kwa wajumbe hao pekee, bali iwekwe kwenye tovuti za Bunge, za Baraza la Wawakilishi, za serikali ili ziwe wazi kwa wadau wazijadili.
Alisema kanuni za kawaida za Bunge zimekuwa zikitoa mamlaka makubwa sana kwa maspika kwa kiwango, ambacho wamekuwa wakifanya maamuzi mabovu na kusababisha vurugu.

“Ni lazima Bunge la Katiba liwe na kanuni, ambazo zinatoa mamlaka zaidi kwa wajumbe na pia kuweka msingi wa kujenga mwafaka zaidi wa kitaifa kwa kuwa Katiba ni maridhiano ya wananchi na siyo ushindani wa vyama au makundi mbalimbali,” alisema Mnyika.

Alisema wajumbe ni wawakilishi tu wa kuwezesha mwafaka huo kufikiwa na kanuni ni nyenzo ya kuongoza majadiliano ya kufikia maridhiano kwa kuzingatia maoni ya wananchi na maslahi ya umma.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Katibu wa Bunge na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, leo wajumbe hao watakuwa na jukumu la kuandaa na kupitisha kanuni za Bunge Maalumu.
Chanzo:Nipashe.

RATIBA KAMILI RAUNDI YA KWANZA LIGI YA MABINGWA AFRIKA

Yanga SC (Tanzania) Vs Al Ahly (Misri)
Berekum Chelsea (Ghana) Vs Ahli Benghazi (Libya)
Gor Mahia (Kenya) Vs Esperance (Tunisia)
Enyimba (Nigeria) Vs AS Real (Mali)
Astres de Douala (Cameroon) Vs TP Mazembe (DRC)
B.Y.C (Liberia) Vs Sewe Sport (Ivory Coast)
Dedebit (Ethiopia) Vs CS Sfaxien (Tunisia)
Horoya (Guinea) Vs Raja Casablanca (Morocco)
Flambeau de l’Est (Burundi) Vs Coton Sport (Cameroon)
Entente Setif (Algeria) Vs ASFA Yennenga (Burkina Faso)
Stade Malien (Mali) Vs El Hilal (Sudan)
AC Leopards (Congo) Vs Primeiro de Agosto (Angola)
Kaizer Chiefs (Afrika Kusini) Vs Liga Muçulmana (Msumbiji)
Dynamos FC (Zimbabwe) Vs AS Vita Club (DRC)
Zamalek (Misri) Vs Kabuscorp (Angola)
Nkana (Zambia) Vs Kampala City Council (Uganda) 
(Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Februari 28 na Machi 2 
na marudiano zitachezwa kati ya Machi 7 na 9 mwaka huu)

VIDIC WA MAN UNITED AKUBALI KWENDA YAKE ITALY

BEKI Kisiki Nemanja Vidic wa Man united amekubali kujiunga na Inter Milan ya Italia. Nyota huyo wa kimataifa wa Serbia ambaye alitangaza Januari kuamua kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu huu anatazamiwa kuasaini dili la  mkataba wa miaka miwili ambao utamuwezesha kulipwa kitita cha euri milioni tatu kwa mwaka. Kuna taarifa kuwa Vidic aliwafahamisha viongozi wake wa United kuhusu uamuzi wake wa kukubali kwenda nchini Italia baada ya kufikia makubaliano kwenye mchezo waliotoka sare ya bila ya kufungana na Arsenal katika uwanja wa Emirates Jumatano iliyopita. Ofisa mkuu wa Inter, Piero Ausilio amekuwa na mawasiliano ya karibu na nyota huyo toka Januari alipotangaza kutaka kuondoka. Toka atangaze kuondoka Vidic amekuwa akiwendwa na vilabu mbalimbali huku Monaco ya Ufaransa na Galatasaray ya Uturuki zikiwa mojawapo lakini nyota huyo ameamua kwenda Italia. Vidic alijiunga na United akitokea klabu ya Spartak Moscow ya Urusi mwaka 2006 na amefanikiwa kushinda mataji matano ya Ligi Kuu na moja la Ligi ya Mabingwa barani ULaya katika kipindi cha miaka nane aliyokaa Old Trafford.