Tuesday, May 13, 2014

DIEGO COSTA KUELEKEA STAMFORD BRIDGE MAPEMA JUNI


Klabu ya Chelsea imekubali kutoa kiasi cha pauni milioni 32 kwa Atletico Madrid kwaajili ya kukamilisha dili la kumsajili mshambuliji mahiri,Diego Costa.
Costa ambaye amekuwa muhimili mkubwa kwa klabu hiyo ya Uhispania ikiwa na uwezo wa kuchukua La Liga na Ligi ya mabingwa barani Ulaya mpaka sasa, amekuwa akihusishwa na kuhamia London huku Jose Mourinho akihitaji mshambuliaji hatari zaidi.
Mourinho alisisitiza mara baada ya mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya Uingereza kuwa alikuwa na malengo ya kufanya usajili mkubwa sana Stamford Bridge katika kipindi cha soko la usajili haraka iwezekanavyo.
Dili la Costa halitarajiwi kutangazwa rasmi mpaka ifikapo mapema mwezi Juni mara baada ya michezo miwili mikubwa ambayo nyota huyo anapambana kuweza kuwa fiti kuisaidia timu yake.
Costa alipata majeraha ya misuli na alikosa mchezo waliotoka sare ya 1-1 dhidi ya Malaga Jumapili,mchezo ambao iwapo Atletico wangeshinda wangekuwa
tayari wametwaa taji la La Liga msimu huu.
Atletico watasafiri mpaka Camp Nou kupambana na Barcelona siku ya Jumapili katika mchezo ambao utaamua kombe linaenda wapi na siku saba baadae watakutana na wapinzani wao wa Jiji,Real Madrid kwenye fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya itakayopigwa Lisbon.
Chelsea walimaliza msimu wa 2013/14 katika nafasi ya tatu,pointi nne nyuma ya Manchester City na pointi mbili nyuma ya Liverpool huku rekodi yao ya kufunga magoli ikionekana ndiyo sababu ya kushindwa kwao kupata taji.
Kikosi cha darajani kilifunga magoli 71 ukilinganisha na magoli 102 ya Man City na 101 ya Liverpool na mchezaji mmoja pekee ndiye alikuwa
mhimili ambaye ni kiungo mshambuliaji Eden Hazard akifunga magoli 14.
Samuel Eto’o,Fernando Torres na Demba Ba walifunga jumla ya magoli 19 pekee wote kati yao hivyo kumshawishi Mourinho kutumia pesa nyingi kwaajili ya kupata saini ya mchezaji kama Costa ambaye amefunga magoli 27 kwenye michezo 33 ya La Liga msimu huu.

KOCHA TIM SHERWOOD ATUPIWA VIRAGO SPURS

KOCHA Tim Sherwood amefukuzwa Tottenham Hotspur kiasi cha miezi sita tang aanze kazi White Hart Lane.
Sherwood alirithi mikoba ya Andre Villas-Boas Desemba kwa Mkataba wa miezi 18, lakini ameshindwa kuingia katika msimu wa pili na klabu hiyo.
Tetesi za kuondolewa kwa Sherwood zilianza mwezi uliopita, na hatimaye Mwenyekiti Daniel Levy kutafuta mtu mwingine mwafaka zaidi.
Sherwood ameshinda mechi 14 kati ya 28 akiwa kazini, akitoa safe nne na kufungwa 10, Spurs ikimaliza katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi, ikizidiwa pointi 10 na Arsenal iliyomaliza nafasi ya nne.
Mwalimu huyo mwenye umri wa miaka 45 anaweza kupewa ofa mara moja kurejea kurejea klabu ya Daraja la kwanza, Brighton baada ya Oscar Garcia kujiuzulu baada ya kufungwa katika mechi ya Nusu Fainali ya mchujo dhidi ya Derby.

KIINGILIO MECHI YA TAIFA STARS VS ZIMBAMBWE SH. 5,000/-

Mkutano wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na wenyeviti wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kupata maoni yao juu ya changamoto zilizojitokeza katika ligi hiyo umefanyika juzi (Mei 11 mwaka huu).
Klabu za VPL zilizohudhuria mkutano huo n
i Azam, Coastal Union, JKT Ruvu, Mbeya City, Mgambo Shooting, Mtibwa Sugar, Polisi Morogoro, Ndanda FC, Ruvu Shooting, Stand United na Tanzania Prisons.
Simba na Yanga hazikuhudhuria mkutano huo,na wala klabu hizo hazikutoa udhuru wowote wa kutokuwepo.
Maazimio ya mkutano huo ni kuwa kwa misimu mitatu ijayo kuanzia msimu wa 2014/2015 klabu zimekubaliana ziruhusiwe kusajili wachezaji watano wa kigeni. Kamati ya Utendaji ya TFF itatoa uamuzi wa mwisho juu ya suala hilo katika kikao chake kijacho.
Pia klabu hizo zimekubali timu zao za U20 kuanzia msimu ujao zicheze ligi ya mkondo mmoja. Hata hivyo, utekelezaji wa hilo utategemea na upatikanaji wa mdhamini wa ligi hiyo ambapo TFF inafanya jitihada za kumpata mdhamini huyo.
Vilevile Mwenyekiti wa Kamati ya Mpira wa Miguu wa Wanawake, Lina Kessy amezishauri klabu za VPL kuanzisha timu za wanawake, ambapo klabu hizo zimesema zitaufanyia kazi ushauri huo.

KIINGILIO MECHI YA TAIFA STARS 5,000/-
Kiingilio cha chini cha mechi ya kwanza ya raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika 2015 nchini Morocco kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe (Mighty Warriors) itakayochezwa Jumapili (Mei 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.
Washabiki watakaolipa kiingilio hicho ni kwa wale watakaokaa kwenye viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. 
Kwa upande wa VIP B na C kiingilio kitakuwa sh. 10,000 wakati kwa VIP A itakuwa ni sh. 20,000.
Tiketi zinatarajiwa kuanza kuuzwa siku moja kabla ya mechi hiyo katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam, na uwanja siku ya mchezo huo utakaoanza saa 10 kamili jioni.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ikiwa chini ya Kocha Mart Nooij inatarajia kurejea jijini Dar es Slaam kesho (Mei 14 mwaka huu) kutoka Mbeya kuendelea na maandalizi ya kuikabili Zimbabwe.

RAMBIRAMBI MSIBA WA MKUFUNZI KASINDE
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha Mkufunzi wa waamuzi nchini, Omari Kasinde kilichotokea jana (Mei 12 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Mbali ya kuwa Mkufunzi, Kasinde ambaye anazikwa leo (Mei 13 mwaka huu) mchana katika Makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam pia alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati iliyopita ya Waamuzi ya TFF iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Kapteni mstaafu Stanley Lugenge.
Msiba huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu nchini kwani, Kasinde enzi za uhai wake alitoa mchango mkubwa katika mchezo huu tangu akiwa mwamuzi na baadaye mkufunzi na kiongozi..
TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Kasinde, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), na Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu Tanzania (FRAT) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF

Monday, May 12, 2014

STARS, ZIMBABWE KUUMANA DAR JUMAPILI

Mechi ya kwanza ya raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika 2015 nchini Morocco kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe (Mighty Warriors) itafanyika Jumapili (Mei 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
UWANJA_WA_TAIFA_DAR
Awali mechi hiyo tulipanga ichezwe Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kwa nia ya kuhakikisha mikoa yote ya Tanzania inapata fursa ya kuwa mwenyeji wa mechi za kimataifa.
Ili Uwanja wa Sokoine uweze kuchezwa mechi za kimataifa za mashindano, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) lilituma Mkaguzi (inspector) wake kwenye uwanja huo Jumamosi (Mei 10 mwaka huu) ambapo imeamua kuwa marekebisho yanayofanyika hayatamalizika katika muda stahili, hivyo mchezo huo kutochezwa Sokoine.
Tunatoa mwito kwa wamiliki wote wa viwanja kuwasiliana na TFF ili Idara ya Ufundi iwaelekeze maboresho ya kufanya ili viwanja vingi iwezekanavyo viweze kukidhi viwango vinavyotakiwa na CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Taifa Stars ambayo ilikuwa kambini mkoani Mbeya itarejea Dar es Salaam keshokutwa (Mei 14 mwaka huu) kujiandaa kwa mechi hiyo.
BONIFACE WAMBURA 
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (T

Sunday, May 11, 2014

NIGERIA YAITANDIKA 2-0 NGORONGORO HEROES TAIFA

Timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20,Ngorongoro Heroes jioni hii imeambulia kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Nigeria uwanja wa taifa jijini dare s salaam katika Mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wa 20 ambapo kwa matokeo hayo yamempa kazi ngumu kocha mkuu John Simkoko kusonga mbele.
Ngorongora walipata nafasi kadhaa za kufunga kipindi cha kwanza, lakini bado ugonjwa wa kutotumia nafasi muhimu unazidi kuitafuna timu hii

Mshambuliaji Saady Kipanga alishindwa kuonesha makeke yake baada ya kupoteza nafasi kadhaa za kufunga.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika milango ya timu zote ilikuwa migumu, huku kipa namba moja wa Heroes, Aishi Manula akiumia.
Kipindi cha pili, Manula alishindwa kurejea uwanjani na kumpisha kipa namba mbili, Peter Manyika.
Katika Kipindi hicho cha pili Ngorongoro waliingia kizembe na kujikuta wakifungwa mabao mawili na kumaliza mechi kwa kipigo cha nyumbani cha mabao mawili kwa sifuri.

RAMBIRAMBI MSIBA WA BALOZI WA MALAWI

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha Balozi wa Malawi nchini, Flossie Gomile-Chidyaonga kilichotokea juzi (Mei 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

RUVU SHOOTING YAMNASA MCHEZAJI TOKA KAGERA SUGAR.

Club ya Ruvu Shooting ya mkoani  pwani imefanikiwa kumnsa mchezaji mahiri wa timu ya Kagera sugar nafasi ya midfild kwa kipindi cha misimu miwili iliyopita, Zuberi Kasim Dabi ambapo amesaini dili la  mkataba wa miaka miwili kuichezea timu  hiyo ya Pwani.
Dabi amesaini mkataba huo Ijumaa hii, Mei 9, 2014 katika ofisi za Ruvu shooting zilizoko Mlandizi, Pwani mbele ya uongozi wa timu hiyo ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Kanali Charles Mbuge.
Dabi kabla ya kujiunga na Kagera sugar amewahi pia kuzichezea timu za Villa Squad ya Dar es salaam, Polisi Morogoro ambayo musimu huu imefanikiwa kupanda daraja, kucheza ligi kuu.
Ruvu shooting ipo katika mchakato mkali na mkubwa kukisuka kikosi chake kwa kusajili wachezaji wenye uwezo kama kocha wake mkuu Tom Olaba alivyoshauri.
Wakati Ruvu shooting wakisajili wachezaji wa timu kubwa, tayari kikosi hicho kimeivunja timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 na kutangaza kukiunda upya kwa kuwafanyia majaribio wachezaji vijana kati ya Mei 15-28, majaribio ambayo yatafanyika katika uwanja wa Mabatini, Mlandizi