Wednesday, July 2, 2014

KIRAFIKI GABORONE: BOTSWANA YAICHAPA 4 TANZANIA 2

TAIFA_STARS-BORA1Katika mechi ya kirafiki Wenyeji Botswana wamefanikiwa kuilaza taifa stars katika Uwanja wa Taifa Jijini Gaborone wameichapa Tanzania Bao 4-2 katika Mechi ya Kirafiki.
Taifa Stars ndio waliotangulia kufunga kwa Bao la Mcha Khamisi kufuatia Difensi ya Botswana kujichanganya lakini Timu hiyo, inayoitwa Zebras, ilisawazisha kabla Mapumziko kwa Bao la Kichwa la Jerome Ramatlhatwane.
Hadi Mapumziko, Zebras 1 Taifa Stars 1.
Kipidi cha Pili, Zebras walikuja moto na kupiga Bao 3 kupitia Lemponye Tshireltso, Bonolo Phuduhudu na Kijana wa Miaka 19, Karabo Phiri.
Taifa Stars walifunga Bao lao la Pili kwa Penati ya Dakika ya 76 ya John Bocco.
Mechi hii ilikuwa ya kujipima nguvu kwa Timu zote mbili kwa ajili ya Mechi za Mchujo za AFCON 2015 ambapo Taifa Stars wataivaa Msumbiji Jijini Dar es Salaam hapo Julai 20 na Zebras kucheza na Guinea Bissau Julai 19.
Taifa Stars, ambao wako chini ya Kocha Mart Nooij, waliwasili huko Gaborone kwa Kambi ya Mazoezi tangu Juni 24 na wamekuwa wakifanya Mazoezi Uwanja wa SSKB wakiwa na Kikosi kamili kasoro Wachezaji wawili wa TP Mazembe, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.
Jumamosi, huko huko Gaborone, Taifa Stars watajipima nguvu na Lesotho.

Friday, June 27, 2014

SIMBA SC YAWAALIKA WADAU KUONA MAENDELEO YA UWANJA BUNJU



SIMBA wekundu wa msimbazi wamesema kuwa sasa wapo katika kuondoa dhama kama club kongwe ilianzishwa mwaka 1936 kuhakikisha wanakamilisha uwanja huo.
hivyo basi wameamua kuwaalika wanachama wanahabari kuona maendeleo ya uwanja wa Bunju Jinsi unavyo endelea ambapo sasa umefika hatua nzuri kilicho baki ni kuanza kuweka nyasi.

Yote  kwa yote Azam fc kwa hapa tz ndio timu pekee ndio klabu ya Tanzania yenye uwanja wake wa kisasa kwa ajili ya mazoezi, mechi za ligi kuu na michuano yote inayosimamiwa na shirikisho la soka barani Afrika, CAF.
Katika historia ya soka la Tanzania, Azam fc haiwezi kunusa ukongwe wa klabu mbili za Simba na Yanga.
Hizi ni klabu zenye mafanikio ndani na nje ya uwanja. Ni klabu zenye mashabiki kila kona ya nchi hii.
Lakini licha ya kukaa miaka mingi katika soka la ushindani nchini Tanzania na michuano ya Kimataifa, Yanga na Simba hazijawahi kumiliki viwanja vyake vya mazoezi na mechi za ligi kuu.
Kwa miaka mingi sasa viongozi wanaopita katika klabu hizo wanakuja na ndoto za kujenga viwanja, lakini zinayeyuka kutokana sababu mbalimbali ikiwemo kuendekeza siasa kuliko vitendo.

RASMI" MAHAKAMA YAAMUA UCHAGUZI WA SIMBA SC KUFANYIKA JUNI 29

BAADA ya mvutano wa hapa na pale katika uchaguzi wa Simba sc sasa tamati imefika baada ya mahakamu kuu kuruhusu mchakato huo kuendelea kama kawaida.
Baadhi ya wanachama wa Simba walienda mahakama kuu wakihitaji chombo hicho cha dola kusimamisha uchaguzi wa Simba unaotarajia kufanyika juni 29 mwa
ka huu.
Sababu ya wanachama hao ilikuwa ni kupinga maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya Simba, chini ya mwenyekiti wake, Wakili Damas Daniel Ndumbaro, kuliengua jina la aliyekuwa mgombe wa Urais, Michael Wambura kwa mara ya pili.
Hata hivyo, suala la wanachama kupelekea suala la michezo katika mahakama ya kawaida ilikuwa ni hatari zaidi kwa klabu ya Simba kwasababu sheria za mpira ziko wazi na hairuhusiwi kupeleka mambo ya mpira mahakama za dola.
FIFA wanataka masuala ya mpira yasuluhishwe katika mifumo yake ya haki na si vinginevyo.
Kupeleka mambo ya mpira mahakama za kawaida ilikuwa moja ya sababu iliyokuwa na nguvu kumuengua Wambura kwa mara ya kwanza.
http://shaffihdauda.com/wp-content/uploads/2014/05/Wanachama-Simba1.jpgHata hivyo kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari na katibu mkuu wa Simba, Kamwaga jioni ya leo imesema kamati ya Uchaguzi ya Simba SC imesema kuwa inapenda kuwaalika wanachama wote wa Simba katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Klabu uliopangwa kufanyika Keshokutwa Jumapili, Juni 29 mwaka huu, katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Kamwaga alifafanua kuwa katika uchaguzi huo, jumla ya wagombea 27 wanatarajiwa kushiriki na Kamati ya Uchaguzi imeazimia kwamba suala la muda litazingatiwa sana safari hii kutokana na ukweli wa kuwepo kwa wagombea wengi.

RASMI:COUTINHO WA YANGA AWASILI DAR

Coutinho (kushoto) akiwa na msemaji wa Yanga Baraka Kizuguto
Kiungo mshambuliaji Mbrazil Andrey Macrcel Ferreira Coutinho amewasili leo na tayari kwa ajili ya kujiunga na kikosi cha Young Africans kwenye maandalizi ya msimu mpya wa 2014/2015

MAXIMO ATAMBULISHWA RASMI YANGA,NA HUU NDIO MKATABA ALIOPEWA

Uongozi wa klabu ya Yanga umemtambulisha rasmi kwa waandishi wa habari Kocha mbrazil Marcio Marcel Maximo  kama ndio
kocha atakayeweza kukinoa kikosi cha timu hiyo katika msimu ujao wa Ligi kuu Tanzania Bara.
Utambulishwaji huo ulifanywa katika makao makuu ya Klabu hiyo jijini Dar es salaam na kuuzuliwa na waandishi wa habari wengi pamoja na wanachama waliokuwa nje kwa ajili ya kumshuhudia kocha huyo.
Wakala aliyefahamika kwa jina moja la Ally ndiye aliyeweza kufanikisha mipango hiyo ya kumleta maximo.
"nawashukuru wana Yanga kwa uvumilivu wao kwani kwa miaka mitatu sasa nawasiliana na Marcio Maximo " aliseama Ally na kuongeza kuwa mtazamo wa kocha huyo ni kuinua vipaji na kuwataka wana Yanga wavumilie na kumpa muda kwa ajili ya kupata mafanikio.

Maximo amesaini mkataba wa miaka miwili ya kuifundisha Yanga na amekuja na msaidizi wake Leonardo Neiva.
Naye Maximo amesema kuwa sio rahisi kuipandisha timu ya Yanga na kupata mafanikio makubwa bali kwa kushirikiana kila kitu kitafanikiwa.
"Wakati nakuja kwa mara ya kwanza nilikuwa nasikia Yanga na Simba,lakini niliporejea tena kwa mara ya pili sasa nasikia Azam, mbeya City na virabu vingine" alisema kocha huyo huku akikubali kuwa upinzani ni mkubwa.
Kocha Marcio Maximo  anaaza kazi rasmi Siku ya Jumatatu na na atakuwa na msaidizi wake Leonardo Neiva ambapo watajihusisha sana na Vijana pamoja na timu ya wakubwa.

BRAZIL KOMBE LA DUNIA 2014 HATUA YA 16 BORA DIMBANI KESHO.

Michuano ya Kombe la Dunia huko Brazil sasa zimeingia Hatua ya Mtoano na zipo Timu 16 zinazowania kutinga Robo Fainali.

KOMBE LA DUNIA

RAUNDI YA PILI YA MTOANO
Saa za Bongo
JUMAMOSI, JUNI 28, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
19:00 usiku
49
Brazil v Chile
Mineirão
Belo Horizonte
23:00 usiku
50
Colombia v Uruguay
Maracanã
Rio de Janeiro
JUMAPILI, JUNI 29, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
19:00 usiku
51
Netherlands v Mexico
Castelao
Fortaleza
23:00 usiku
52
Costa Rica v Greece
Pernambuco
Recife
JUMATATU, JUNI 30, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
19:00 usiku
53
France v Nigeria
Nacional
Brasilia
23:00 usiku
54
Germany v Algeria
Beira-Rio
Porto Alegre
JUMANNE, JULAI 1, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
19:00 usiku
55
Argentina v Switzerland
Corinthians
Sao Paulo
23;00 usiku
56
Belgium v USA
Fonte Nova
Salvador