SHIRIKISHO la Soka la Ghana-GFA limetoa taarifa ya kuinyima ruhusa Sierra Leone
ya kutumia moja ya viwanja vyake kwa ajili ya mechi yao ya kufuzu
michuano ya Mataifa ya Afrika. Sierra Leone ilikuwa imeomba ruhusa
kucheza baadhi ya mechi zake za kufuzu michuano hiyo nchini Ghana
kutokana na mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa Ebola nyumbani kwao. Katika
taarifa ya Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF iliyotolewa jana imedai
kuwa Sierra Leone walielekeza mechizao za nyumbani katika mzunguko wa
mwisho wa kufuzu zichezewe Ghana. Baada ya CAF kutuma maombi hayo ya
Sierra Leone kwenda kwenye mamlaka husika Ghana, GFA walijibu kwa
kuwataka majirani zao hao kushughulikia suala hilo kiserikali. GFA
limelitaka Shirikisho la Soka la nchini hiyo kutuma maombi yao
serikalini kwani suala hilo linahusisha mambo ya afya hivyo wao watakuwa
hawana kauli kwenye hilo.
Wednesday, August 13, 2014
VAN GAAL AWATAKA SHABIKI WA MAN UNITED KUWA NA SUBIRA
BOSI mpya wa Manchester United Louis van Gaal anadhani atahitaji muda zaidi ili kuibadilisha timu hiyo pamoja na kukamilisha mechi sitaza kujipia nguvu kabla ya kuanza kwa msimu kwa ushindi. United ilimaliza ratiba yao ya mechi zao kujipima nguvu kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Valencia jana usiku na kumpa Mholanzi huyo ambaye alichukua mikoba baada ya kuingoza nchi yake kushika nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia, ushindi wa kwanza katika Uwanja wa Old Trafford. Sasa United wanakabiliwa na mchezo dhidi ya Swansea City katika ufunguzi wa Ligi Kuu nyumbani Jumamosi lakini Van Gaal hana uhakika kama Jonny Evans, Luke Shaw na Antonio Valencia ambao hawakucheza mechi ya jana kutokana na majeruhi kama watakuwa fiti. Watatu hao wakiwa benchi, Van Gaal alilazimika kuwatumia Phil Jones, Chris Smalling na Tyler Blackett katika nafasi ya ulinzi wa kati huku Asley Young na Reece James wakicheza kama katika wingi.Akiwa amefanikiwakufanya usajili wa wachezaji wawili pekee ambao ni Shaw na Ander Herrera kiangazi hiki, Van Gaal amesema bado anahitaji muda kwani timu wala wachezaji hawawezi kubadilika katika kipindi cha wiki mbili au tatu.
TFF YASEMA HAITAMBUI UONGOZI MPYA COASTAL UNION.
SHIRIKISHO la Soka wa nchini-TFF limedai kutotambua mabadiliko ya uongozi ndani ya Coastal
Union yanayodaiwa kufanywa na mkutano wa wanachama wa klabu hiyo
uliofanyika hivi karibuni.
Katika taarifa ya shirikisho hilo iliyotumwa
na Ofisa Habari wake

Saturday, August 9, 2014
MTIBWA SUGAR 2-0 AZAM KIKOSI CHA PILI TAMASHA LA MATUMAINI
Timu ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kukichalaza kikosi cha pili cha Azam fc mabao 2-0 dhidi ya katika mechi
maalumu ya kirafiki ya Tamasha la Usiku wa Matumaini usiku huu uwanja wa Taifa,
uliopo maeneo ya Chang’ombe, jijini Dar es salaam.
Kwa
ushindi huo, wakata miwa wa mashamba ya Manungu Turiani Mkoani Morogoro
wamefanikiwa kutwaa Ngao ya Matumaini.
Katika
mchezo huo ambao ulikuwa maalumu kwa kocha mkuu wa Mtibwa, Mecky Mexime
kuonesha wachezaji wake jinsi walivyoiva, wachezaji wawili wakongwe, Musa
Hassan Mgosi na Vicent Barnabas walionesha kandanda l
a kuvutia na kudhihirisha kuwa utu uzima dawa.
Baada
ya mechi ya leo , kikosi hicho cha Azam kitasafiri muda wowote kuelekea mjini Kigali
nchini Rwanda kikifuata kikosi cha kwanza kinachoshiriki kombe la Kagame.
a kuvutia na kudhihirisha kuwa utu uzima dawa.
UJIO WA MAOFISA WA FIFA NCHINI.

Ujumbe huo wa FIFA utakaokuwa na
maofisa sita, baada ya ziara yake utashauri jinsi ya kuboresha
uendeshaji huo katika kikao cha pamoja kati yake na Kamati ya Utendaji
ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kitakachofanyika mwishoni
mwa wiki ijayo.
Wednesday, August 6, 2014
SIMBA YA MNASA ABDI BANDA WA COASTAL UNION
CLUB ya Simba sc wazee wa Msimbazi wamefanikiwa kumsajili beki wa kushoto wa
Coastal Union Abdi Banda baada ya kumuweka kwenye rada zake kwa muda mrefu.
Banda aliwahi kuripotiwa
kuwindwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili mwaka huu, lakini
ilishindikana kwasababu alikuwa na mkataba na wagosi wa kaya na viongozi wa
klabu hiyo walilalamika kitendo cha wanajangwani kumrubuni kijana huyo.
YANGA WAISHANGA CECAFA KUWEKA PEMBENI.
UONGOZI wa klabu ya Young Africans leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu na kusema kilichofanywa na waandaji wa michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuiondoa timu isishiriki ni cha kushangaza sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.
Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema walipata barua ya mwaliko wa kushiriki mashindano tarehe 25/7/2014 na kudhibitisha kushiriki michuano hiyo kwa kuandika barua iliyokwenda TFF na kisha wao kuiwasilisha kwa CECAFA.
Subscribe to:
Posts (Atom)