Wednesday, August 13, 2014

GHANA YAIKATALIA SIERRA LEONE KUOGOPA EBOLA.

SHIRIKISHO la Soka la Ghana-GFA limetoa taarifa ya kuinyima ruhusa Sierra Leone ya kutumia moja ya viwanja vyake kwa ajili ya mechi yao ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika. Sierra Leone ilikuwa imeomba ruhusa kucheza baadhi ya mechi zake za kufuzu michuano hiyo nchini Ghana kutokana na mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa Ebola nyumbani kwao. Katika taarifa ya Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF iliyotolewa jana imedai kuwa Sierra Leone walielekeza mechizao za nyumbani katika mzunguko wa mwisho wa kufuzu zichezewe Ghana. Baada ya CAF kutuma maombi hayo ya Sierra Leone kwenda kwenye mamlaka husika Ghana, GFA walijibu kwa kuwataka majirani zao hao kushughulikia suala hilo kiserikali. GFA limelitaka Shirikisho la Soka la nchini hiyo kutuma maombi yao serikalini kwani suala hilo linahusisha mambo ya afya hivyo wao watakuwa hawana kauli kwenye hilo.

VAN GAAL AWATAKA SHABIKI WA MAN UNITED KUWA NA SUBIRA

BOSI mpya wa Manchester United Louis van Gaal anadhani atahitaji muda zaidi ili kuibadilisha timu hiyo pamoja na kukamilisha mechi sitaza kujipia nguvu kabla ya kuanza kwa msimu kwa ushindi. United ilimaliza ratiba yao ya mechi zao kujipima nguvu kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Valencia jana usiku na kumpa Mholanzi huyo ambaye alichukua mikoba baada ya kuingoza nchi yake kushika nafasi ya tatu katika Kombe la Dunia, ushindi wa kwanza katika Uwanja wa Old Trafford. Sasa United wanakabiliwa na mchezo dhidi ya Swansea City katika ufunguzi wa Ligi Kuu nyumbani Jumamosi lakini Van Gaal hana uhakika kama Jonny Evans, Luke Shaw na Antonio Valencia ambao hawakucheza mechi ya jana kutokana na majeruhi kama watakuwa fiti. Watatu hao wakiwa benchi, Van Gaal alilazimika kuwatumia Phil Jones, Chris Smalling na Tyler Blackett katika nafasi ya ulinzi wa kati huku Asley Young na Reece James wakicheza kama katika wingi.Akiwa amefanikiwakufanya usajili wa wachezaji wawili pekee ambao ni Shaw na Ander Herrera kiangazi hiki, Van Gaal amesema bado anahitaji muda kwani timu wala wachezaji hawawezi kubadilika katika kipindi cha wiki mbili au tatu.


TFF YASEMA HAITAMBUI UONGOZI MPYA COASTAL UNION.

SHIRIKISHO la Soka wa nchini-TFF limedai kutotambua mabadiliko ya uongozi ndani ya Coastal Union yanayodaiwa kufanywa na mkutano wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika hivi karibuni. 

Katika taarifa ya shirikisho hilo iliyotumwa na Ofisa Habari wake
Boniface Wambura, TFF imesema wao wanatambua uongozi wa Coastal Union uliochaguliwa na mkutano wa uchaguzi wa klabu na ndio wataendelea kufanya nao kazi, na sio uongozi mwingine wowote ule. Shirikisho hilo limewakumbusha wanachama wakewakiwemo Coastal Union kuheshimu katiba ya TFF pamoja na katiba zao, kwani hazitambui mapinduzi ya uongozi wala kamati za muda za utendaji. TFF inafanya kazi za kamati za utendaji zilizopatikana kwa njia ya uchaguzi tu. Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa tayari TFF imepokea barua kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mnguto ikilalamikia kusimamishwa kwake na wanalifuatilia suala hilo kwa kina, na ikibainika kuwa kuna viongozi wamehusika katika mapinduzi hayo watafikishwa katika vyombo husika kwa hatua zaidi.

Saturday, August 9, 2014

MTIBWA SUGAR 2-0 AZAM KIKOSI CHA PILI TAMASHA LA MATUMAINI

Timu ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kukichalaza kikosi cha pili cha Azam fc mabao 2-0 dhidi ya katika mechi maalumu ya kirafiki ya Tamasha la Usiku wa Matumaini usiku huu uwanja wa Taifa, uliopo maeneo ya Chang’ombe, jijini Dar es salaam.
Kwa ushindi huo, wakata miwa wa mashamba ya Manungu Turiani Mkoani Morogoro wamefanikiwa kutwaa Ngao ya Matumaini.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa maalumu kwa kocha mkuu wa Mtibwa, Mecky Mexime kuonesha wachezaji wake jinsi walivyoiva, wachezaji wawili wakongwe, Musa Hassan Mgosi na Vicent Barnabas walionesha kandanda l
a kuvutia na kudhihirisha kuwa utu uzima dawa.
Baada ya mechi ya leo , kikosi hicho cha Azam kitasafiri muda wowote kuelekea mjini Kigali  nchini Rwanda kikifuata kikosi cha kwanza kinachoshiriki kombe la Kagame.

UJIO WA MAOFISA WA FIFA NCHINI.

imagesMaofisa wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wanawasili nchini kesho (Agosti 10 mwaka huu) kuangalia jinsi mchezo huo unavyoondeshwa nchini.
Ujumbe huo wa FIFA utakaokuwa na maofisa sita, baada ya ziara yake utashauri jinsi ya kuboresha uendeshaji huo katika kikao cha pamoja kati yake na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kitakachofanyika mwishoni mwa wiki ijayo.

Wednesday, August 6, 2014

SIMBA YA MNASA ABDI BANDA WA COASTAL UNION

CLUB ya Simba sc wazee wa Msimbazi wamefanikiwa kumsajili beki wa kushoto wa Coastal Union Abdi Banda baada ya kumuweka kwenye rada zake kwa muda mrefu.
Nyota huyo kinda mwenye uwezo wa kucheza nafasi zote za ulinzi, lakini beki ya kushoto ndio mahala pake haswaa , alisaini mkataba wa miaka mitatu jana na mara moja atajiunga na kikosi cha Simba kinachofanya mazoezi chini ya kocha mkuu, Mcroatia, Zdravko Logarusic.

Banda aliwahi kuripotiwa kuwindwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili mwaka huu, lakini ilishindikana kwasababu alikuwa na mkataba na wagosi wa kaya na viongozi wa klabu hiyo walilalamika kitendo cha wanajangwani kumrubuni kijana huyo.

YANGA WAISHANGA CECAFA KUWEKA PEMBENI.

UONGOZI wa klabu ya Young Africans leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu na kusema kilichofanywa na waandaji wa michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuiondoa timu isishiriki ni cha kushangaza sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.

Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema walipata barua ya mwaliko wa kushiriki mashindano tarehe 25/7/2014 na kudhibitisha kushiriki michuano hiyo kwa kuandika barua iliyokwenda TFF na kisha wao kuiwasilisha kwa CECAFA.