Msafara wa watu 35 ukiwa na wachezaji 27 na benchi la Ufundi 8 wa timu ya Young Africans
tayari umeshawasili Kisiwani Pemba kwa ajili ya maandalizi ya mwisho
kujiandaa na mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2014/2015.
Kocha mkuuu Marcio Maximo na kikosi chake wamefikia katika hoteli ya
kitalii ya Pemba Misali iliyopo eneo la Wesha na watakua wakijifua kwa
muda wa takribani siku 10 kabla ya kurejea jijini Dar es
salaam mwisho wa mwezi huu.

Kikosi
cha Young Africans kitakua kikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gombani
mjini Chake Chake na siku ya alhamis wanataraji kucheza wa kwanza wa
kirafiki dhidi ya timu ya Chipukizi ya kisiwani Pemba.
Kulingana na program ya bench
la Ufundi kisiwani Pemba, Young Africans inatarajia kucheza michezo
mitatu ya kirafiki na timu za kutoka Visiwa vya Pemba na Unguja na
baadae kurejea Dar es salaam kwa michezo mwili ya kimataifa kabla ya
kucheza mchezo wa Ngao ya Hisani septemba 13, 2014.
Wachezaji waliondoka kuelekea Pemba ni:
Walinda Mlango:
Juma Kaseja, Ally Musatfa "Barthez" na Deogratias Munish "Dida"
Walinzi wa Pembeni:
Juma Abdul, Salum Telea, Oscar Joshua, Edwad Charles na Amos Abel
Walinzi wa Kati:
Kelvin Yondani, Nadir Haroub "Cannavaro", Rajab Zahir na Pato Ngonyani.
Viungo:
Mbuyu Twite, Said Juma "Makapu", Omega Seme, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima na Hamis Thabit.
Viungo wa Pembeni:
Saimon Msuva, Mrisho Ngasa, Nizar Khalfani na Andrey Coutinho.
Washambuliaji:
Geilson Santos "Jaja", Said Bahanuzi, Jerson Tegete, Hamis Kizza na Hussein Javu
Benchi la Ufundi walioko Kisiwani Pemba ni:
Kocha Mkuu : Marcio Maximo
Kocha wasaidizi Leonado Neiva, Salvatory Edward
Kocha wa Makipa: Juma Pondamali
Daktari wa timu: Dr Suphian Juma
Meneja wa timu: Hafidh Saleh
Mchua Misuli: Jaco Onyango
Mtunza Vifaa: Mahmod Omar "Mpogolo"