Wednesday, November 26, 2014

BARCA,MADRID,BAYERN YATAWALA ORODHA YA MABEKI FIFPRO WORD XI 2014


KLABU za Barcelona, Real Madrid na Bayern Munich zimetawala orodha ya mabeki wateule katika kikosi cha dunia cha FIFPro World XI 2014 chama cha wachezaji wakulipwa, baada majina 12 ya wachezaji wao kuingia katika orodha kati ya majina 20 yaliyoteuliwa.
Wachezaji wote wanne walioshinda nafasi ya kuwemo katika kikosi hicho mwaka jana wamejumuishwa wakiwemo Dani Alves, Philipp Lahm, Sergio Ramos na Thiago Silva. Leighton Baines, Ashley Cole, Dante na Nemanja Vidic ndio ambayo hayamo katika orodha hiyo ukilinganisha na ya mwaka jana. 
Kwa upande wa Madrid wamo Dani Carvajal, Pepe, Ramos, Raphael Varane na Marcelo wakati Barcelona wamo Jordi Alba, Alves, Javier Marscherano na Gerard Pique huku Bayern wakiwa na David Alaba, Lahm na Jerome Boateng. 
Mabeki wengine wnakamilisha orodha hiyo ni pamoja na David Luiz na Thiago Silva wa Paris Saint-Germain, Pablo Zabaleta na Vincent Kompany wa Manchester City, Branislav Ivanovic na Filipe Luis wa Chelsea, Diego Godin wa Atletico Madrid na Mats Hummels wa Borussia Dortmund. 
Majina manne ya washindi wa beki bora wa dunia yataamuliwa kwa kupiga kura miongoni mwa wachezaji ambapo zaidi ya wachezaji wa kulipwa 20,000 wanatarajiwa kushiriki zoezi hilo.

CAF YAZINDUA MPIRA AINA YA MARHABA KUTOKA ADIDAS KWA AJILI YA AFCON 2015


SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF na kampuni ya vifaa vya michezo ya Adidas wametoa mpira wa Marhaba kuwa maalumu kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon itakayofanyika huko Guinea ya Ikweta mwakani.
Mpira huo unatarajiwa kutambulishwa rasmi Desemba 3 mwaka huu katika shughuli za upangaji ratiba za michuano hiyo ambazo zitakazofanyika jijini Malabo. 
Mpira huo umebuniwa kwa rangi za aina mbalimbali ambazo zinawakilisha uwanda mpana wa bara la Afrika kuanzia jangwa la sahara, rangi ya ang’avu ya samawati katika anga la bahari ya Hindi na Atlantic. 
Mpira huo wa Marhaba umefanyiwa vipimo vyote stahiki na kuthibitishwa kuwa unaweza kutumika katika hali yeyote katika michuano hiyo.


SERIKALI YATOA SH. BILIONI 5 KIANZIO UJENZI WA JENGO LA MAABARA YA UPASUAJI.

JUMLA  ya shilingi  bilioni tano  zimetolewa  na serikali  kama kianzio cha ujenzi wa jengo la upasuaji  ujenzi wa maabara pamoja na kununua dawa katika hospitali teule ya rufaa  ya Tumbi mkoani Pwani.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa na naibu waziri ofisi ya waziri mkuu Aggrey Mwanri mjini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu ambapo amekiri kuwa miundombinu ya hospitali hiyo haiendani na mahitaji yaliyopo.

Amesema kuwa ili kukabiliana na hali hiyo serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya upanuzi wa hospitali hiyo, ambapo inakadiriwa shilingi bilioni 30 zilitumika kwa ajili ya shughuli za ujenzi huo kwa mwaka 2010.

ASKARI POLISI WILAYA CHUNYA ATIWA NGUVUNI KWA TUHUMA ZA MAUAJI.

ASKARI polisi wa kitengo cha usalama barabarani Wilayani Chunya Mkoani Mbeya, PC  Zeferin Didas Focas mwenye umri wa miaka (34) amefukuzwa kazi kwa tuhuma za kuhusika na mauji ya raia Abisai Wadi mwenye miaka 22.
Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya, Ahmed Msangi, amethibitisha kufukwa kazi kwa askari huyo baada ya husika na mauji ya raia huyo yaliyotokea  katika Kata ya Igalula barabara ya Itindi Mkwajuni  Wilayani Chunya Mkoani Mbeya.
Amesema,  askari huyo akiwa na mwezie aliisimamisha pikipiki iliyokuwa imempakia abiria nyuma ambapo dereva huyo alikaidi, ndipo askari huyo alichukua jiwe na kuitupia pikipiki hiyo iliyokuwa katika mwendo kasi  na kumpata abiria huyo.
Amesema, jiwe hilo linasemekana lilimkuta abiria aliyepakizwa kwenye poikipiki hiyo lakini haikuwekwa wazi kwamba jiwe hilo lilimpata katika sehemu ipi ya mwili wa marehemu huyo.

Amesema, askari huyo ambaye kwa sasa anatambulika kwa namba ya X6710 anatarajiwa kufikishwa mahakamani  ili kujibu tuhuma za mauji zinazomkabili mbele yake.

Tuesday, November 25, 2014

MWAMBUSI AREJEA MBEYA CITY KUITIA MAKALI KWA LIGI KUU DEC 26

DSC_0051Klabu ya Mbeya City Council Football Club leo 25/11/2014 inatoa ufafanuzi wa mbalimbali ikiwemo suala la utaratibu wa maslahi kwa watumishi wake (benchi la ufundi, wachezaji na watumishi wengine) na uwepo wa fedha za wadhamini katika klabu yetu.
Uamuzi wa kutoa taarifa hii umefikiwa baada ya vikao vya menejimenti na kamati ya fedha na utawala kufuatia taarifa mbalimbali zinazozalishwa kila siku juu ya klabu yetu toka katika vyanzo ambavyo sio vya klabu.
slide3MASLAHI YA WACHEZAJI
Hivi karibuni baadhi ya wadau wa mchezo wa mpira wa miguu wamehusisha matokeo ya uwanjani iliyopata timu na maslahi kwa wafanyakazi wa klabu kama taasisi.
Sehemu kubwa ya wafanyakazi wa klabu ikijumuisha timu ni wafanyakazi chini ya masharti ya mkataba chini ya muajili ambaye ni Halmashauri ya jiji la Mbeya, Hivyo maslahi ya mfanyakazi(kwa kada hii) hujadiliwa na kukubaliana kwa pande zote mbili(Klabu kwa niaba ya muajiri na Mchezaji kama muajiriwa) kulingana na bei ya soko ndipo mkataba husainiwa.
Klabu imeweka utaratibu wa namna ya wafanyakazi wake kujadiliana na mwajili kuhusu mambo mbali mbali yenye lengo la kuboresha utendaji wa kazi na mazao yake pamoja na masuala ya maslahi pindi kukiwa na haja hiyo.
DSC_0058Mishahara ya wachezaji pamoja na kuamuliwa kwa makubaliano baada ya majadiliano ya pande zote mbili bei ya soko huangaliwa na kuzingatiwa. Msimu wa 2014/2015 mishahara ya wachezaji ilipanda kati ya asilimia 100 – 300(%) ikilinganishwa na msimu uliopita 2013/2014.
Posho zote zitolewazo na klabu zilirekebishwa ikilinganishwa na msimu uliopita kwa kuzingatia makubaliano kati ya wachezaji na menejimenti kabla ya kuanza kwa msimu huu.
Klabu inatambua wazi kuwa mpira ni ajira kama zilivyo ajira zingine,maslahi haya yamewekwa kwa makusudi ili kuboresha hali za maisha za wafanyakazi wetu hasa wachezaji kwani hiyo ndiyo ajira yao.
Ukiondoa mshahara unaoendelea kulipwa kila mwezi hakuna mfanyakazi yeyote anayedai chochote kati ya maslahi yake.

FEDHA ZA WADHAMINI:
Pamoja na kuwa na kipengele cha kutotoa siri (Confidentiality)za mikataba yetu na wadhamini wetu, klabu inasikitishwa namna ambavyo umma wa wanamichezo unavyopotoshwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa changamoto ambazo klabu inapitia hivi sasa kama taasisi zinatokana na kuwepo kwa fedha za wadhamini.
???????????????????????????????Klabu inaomba ikumbukwe kuwa katika msimu uliopita 2013/2014 ilitumia zaidi ya shilingi milioni 700 kutoka katika vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri ikiwa kama mmiliki wa klabu. Wadhamini kwa mujibu wa makubaliano hawajatoa wala hawatoi fedha zote mara moja kwa mujibu wa mkataba, fedha hizo hutolewa kila mwezi na kwa awamu.
Matumizi ya kawaida ya klabu kwa mwezi si chini ya shilingi 49,000,000.00(bila kuhusisha mishahara), katika kipindi cha Julai-Sept 2014, Klabu ilikuwa na mdhamini mmoja tu ambaye ni Binslum tyres Co Ltd anayetoa shilingi 15,000,000.00 kwa mwezi sawa na shilingi 180,000,000.00 kwa mwaka kwa mujibu wa mkataba uliopo.
Ukiangalia mahitaji ya klabu kwa mwezi mmoja hapo juu, fedha hizi za mdhamini zilichangia asilimia 30.6(%) ya gharama za klabu kwa mwezi. Hii ikiwa na maana kuwa bado asilimia 69.4(%) ya gharama za uendeshaji wa timu zilitoka Halmashauri.
Kuanzia mwezi oktoba 2014 ambapo kampuni ya coca cola ilisaini mkataba wa udhamini na klabu yetu. Kampuni ya Coca Cola itakuwa inatoa fedha taslimu Tsh 60 milioni ambazo inazitoa kwa mwaka. Fedha hizi hutolewa kila baada ya robo mwaka shilingi milioni 15. Hii ina maana kuwa coca cola inatoa shilingi 5,000,000.00 milioni kila mwezi.
Hivyo kuanzia mwezi oktoba klabu inapata toka kwa wadhamini wake wawili (Binslum Tyre Co Ltd na Coca Cola Kwanza) shilingi 20,000,000.00 kwa mwezi. Fedha hizi zinachangia asilimia 40.8(%) ya gharama za uendeshaji wa timu kwa mwezi na asilimia 59.2(%) ya gharama hizo bado zinabebwa na Halmashauri.
Uwepo wa wadhamini hivi sasa haujaongeza fedha kutoka katika bajeti hiyo bali umepunguza utegemezi wa timu kwa Halmashauri.
Hivyo basi shutuma zinazotolewa na baadhi ya wadau kuwa changamoto ambazo timu inazipitia kwa sasa ni kutokana na kuwepo kwa fedha za wadhamini ni UPOTOSHAJI MKUBWA.

MWALIMU JUMA MWAMBUSI
Mwalimu Juma Mwambusi ni muajiriwa wa Halmashauri ya jiji la Mbeya anayesimamia benchi la ufundi la timu yetu.Menejiment ilikutana na Mwl Juma Mwambusi katika vikao vyake vya kawaida kupitia changamoto kadhaa zilizojitokeza katika michezo saba ya awali mara baada ya kuwasilisha ripoti ya maendeleo ya timu. Mwalimu Mwambusi na menejiment tumeridhiana kwa faida ya mpira wa miguu na jamii inayoizunguka timu yetu anaendelea kuifundisha timu ya Mbeya City Fc.
slide3Nachukua nafasi hii kuujulisha umma kuwa Mwl.Juma Mwambusi ndiye Kocha Mkuu wa timu na hivi sasa anandaa program ya mafunzo kwa mzunguko wa pili wa ligi unaotarajia kuanza disemba 2014.
MWISHO
Klabu kama taasisi inayokuwa inapitia katika changamoto mbalimbali, ni imani ya menejimenti kuwa changamoto hizi zitaiimarisha na kuikomaza klabu ili kuwa klabu bora zaidi kwa vizazi vijavyo.
Tunatoa shukrani za dhati kwa wadau wetu wote wanaoendelea kutuunga mkono katika kipindi hiki.
Imetolewa na
E.E.Kimbe
KATIBU MKUU
MCC FC

STAND UNITED YATUA JANGWANI KUWAFUATA BAHANUZI,SEME.


UONGOZI wa Stand United ya shinynga inmayoshiririki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu, umesafiri kutoka usukumani mjini Shinyanga hadi maeneo ya Jangwani jijini Dar es salaam kuzungumza na uongozi wa Yanga SC ili uwasajili Said Bahanunzi, Omega Seme na Hamis Thabit kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo.

Mkurugenzi wa Ufundi wa Stand United, Muhibu Kanu akizungumza na mkali wa dimba kupitia mtandao huu kwa njia ya simu amesema kuwa wameamua kufika jijini dar kuuona uongozi wa Yanga SC ili aruhusiwe kuwanasa wachezaji hao kuimarisha kikosi chao kilichop[o nfasi ya 10 katika msimamo wa VPL kikiwa na pointi tisa sawa na Mgambo walioko nafasi ya tisa, Polisi Morogoro (8) na Simba (7).

TFF YAWAPA FURSA TFF YAWAPA FURSA WATANZANIA WAIPIGIE KURA JEZI YA STARS

 watanzania wanatakiwa kupigia kura jezi ya timu ya Taifa ya nyumbani na ugenini kupitia mtandao wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wawww.tff.or.tz ambapo jezi hizo zimewekwa.



TFF ilipokea mapendekezo ya mwonekano mpya wa jezi ya timu ya Taifa kutoka kwa Watanzania 86. Jezi 11 za nyumbani, bukta nane za nyumbani, jezi nane za ugenini na bukta tano za ugenini ndizo zimepitishwa kwa ajili ya kupigiwa kura.

Mwisho wa kupiga kura ni Desemba 31 mwaka huu. Mpigaji kura anatakiwa kubonyeza kwenye jezi na bukta ambayo ameichagua. Anatakiwa kufanya hivyo kwa jezi ya nyumbani na jezi ya ugenini.


Tunawashukuru wote waliojitokeza kupendekeza mwonekano mpya wa jezi ya timu ya Taifa.