- Taifa Stars imetua jijini Addis Ababa, Ethiopia leo (Mei 28 mwaka huu) alfajiri kwa ndege ya EgyptAir ambapo itaweka kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco (Lions of the Atlas) itakayochezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech. Stars iliyotua na kikosi cha wachezaji 21 imefikia hoteli ya Hilton, na imeanza mazoezi leo (Mei 28 mwaka huu) saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Addis. Kwa mujibu wa Kocha Kim Poulsen, Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa na vipindi (sessions) vinne vya mazoezi kabla ya kucheza mechi ya kirafiki na Sudan (Nile Crocodile). Mechi dhidi yan Sudan itachezwa Jumapili kuanzia saa 11 jioni kwenye Uwanja wa Addis. Sudan ambayo pia imeweka kambi yake Addis Ababa kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia ilicheza mechi yake ya kwanza jana (Mei 27 mwaka huu) dhidi ya wenyeji Ethiopia na kulala mabao 2-0. Wachezaji wanaounda Stars ni nahodha Juma Kaseja, nahodha msaidizi Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi. Kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka Addis Ababa kwenda Marrakech alfajiri ya Juni 3 mwaka huu kwa ndege ya EgyptAir. Stars itatua siku hiyo hiyo Casabalanca na kuunganisha moja kwa moja kwenda Marrakech.
Tuesday, May 28, 2013
TAIFA STARS YAANZA KUJINOA ADDIS ABABA.
KING KIBADEN MPUTA AANZA KUINOA RASMI SIMBA SC LEO KATIKA UWANJA WA KINESI

Kabla ya kuanza usaili Kibadeni alianza kutoa mazoezi kwa wachezaji wa simba mara baada ya hapo usaili ukafuata kwa wachezaji waliojitokeza kuomba kusajiliwa katika timu hiyo.
Kibadeni ataanza rasmi leo na atasaini mkataba kesho ikumbukwe kibadeni alikuwa akiifundisha Kagera Sugar ambapo katika msimu uliomalizika wa ligi kuu vodacom tanzania bara ameiwezesha Kagera Sugar kushika nafasi ya nne ikiwa na jumla ya point 43.
aidha ikumbukwe kibadeni amechuwa nafasi ya mfaransa patric liewig alitupiwa virago clubuni hapo baada ya kuyashindwa maisha ya msimbazi.
hivyo kwa sasa simba itakuwa chini ya kocha mkuu king kabadeni mputa akisaidiwa na jamhuri kihwelu julio pamoja na suleimani abdallah matola.
WASIFU WA KING KIBADEN
1949- Oktoba 11; Alizaliwa Mbagala Kiburugwa Dar es Salaam.
1959- Alitungwa jina Kibadeni na watoto wenzake kutokana kucheza soka ya nguvu akiwa mdogo na mfupi, ambalo limefunika jina lake halisi la Abdallah Athumani Seif. Mwenyewe anasema Kibadeni maana yake ni kitu cha baadaye. Kwamba kila siku alikuwa akionekana bado kwa umri na umbo wakati anaweza soka.
1969- Februari 2; Alijiunga na Simba SC ikiitwa Sunderland akitokea Kahe Republic ya Mtaa wa Kongo na Mchikichi, Kariakoo.
1974- Alifunga bao la pili katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Hearts Of Oak ya Ghana nchini Ghana katika Robo Fainali ya Kwanza ya Klabu Bingwa Afrika.
1974- Aliiongoza Simba kuwa klabu ya kwanza na pekee Tanzania kufika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika hadi sasa.
1975- Aliiongoza Simba kuwa klabu ya kwanza kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati Dar es Salaam.
1977- Alifunga mabao matatu peke yake katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Yanga SC.
1993- Aliiwezesha Simba SC kufika Fainali ya Kombe la CAF akiwa Kocha, rekodi ambayo haijavunjwa hadi leo ikiwa ni miaka 20 baadaye
1978-Aling’atuka Simba SC na kwenda kuwa kocha mchezaji Majimaji ya Songea.
2011- Alikwenda Hijja.

NEYMAR ATANGAZA RASMI KUWA MCHEZAJI RASMI WA BARCELONA.
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Brazil, Neymar amemwaga wino na rasmi kuwa mchezaji rasmi wa klabu ya Barcelona ya Hispania. Neymar amesema amesaini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo jana, zikiwa zimepita siku mbili baada ya kutangaza kuwa ameamua kuchagua timu hiyo badala ya mahasimu wao Real Madrid. Nyota huyo amesema anaondoka Santos huku akiwa na majonzi lakini pia ni heshima kwake kusajiliwa na klabu kama Barcelona ambapo katika hali ya kawaida amepata fursa ya kucheza na baadhi ya wachezaji bora kabisa duniani. Neymar mwenye umri wa miaka 21 atajiunga na nyota wenzake Barcelna akiwemo mshindi wan ne mfululizo wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia Lionel Messi, Xavi Hernandez na Andres Iniesta. Sio Neymar wala Barcelona walioweka wazi ada halisi ya uhamisho huo lakini vyombo vya habari nchini Brazil vimedai kuwa Barcelona watalipa kiasi cha euro milioni 30 kwa nyota huyo.
MFAHAMU KWA UZURI TORREZ ELININYOOO MKALI WA MABAOOO
![]() | |||
Taarifa kuhusu yeye | |||
---|---|---|---|
Jina kamili | Fernando José Torres Sanz | ||
Kuzaliwa | 20 March 1984 (age 29) | ||
Nchi | Fuenlabrada, Spain | ||
Urefu | 1.83 m (6 ft 0 in) | ||
Nafasi | Mshambuliaji | ||
Timu ya sasa | |||
Current club | Chelsea | ||
Number | 9 | ||
Timu ya ujana | |||
1995–2001 | Atlético Madrid | ||
Timu za ukubwa | |||
Years | Team | Mechi | Goli |
2001–2007 | Atlético Madrid | 214 | (82) |
2007–2011 | Liverpool | 102 | (65) |
2011– | Chelsea | 82 | (15) |
Timu ya taifa | |||
2000 | Spain U15 | 1 | (0) |
2001 | Spain U16 | 9 | (11) |
2001 | Spain U17 | 4 | (1) |
2002 | Spain U18 | 1 | (1) |
2002 | Spain U19 | 5 | (6) |
2002–2003 | Spain U21 | 10 | (3) |
2003– | Spain | 101 | (31) |
KLABU ALIZOCHEZA NA KUPATA MATAJI |
Atletico Madrid
Segunda Division: 2001-02
Chelsea
Kombe la FA: 2011-12
UEFA Europa Ligi: 2012-13
Timu ya Taifa
Hispania U-16
Kombe la Ulaya la Chini- michuano miaka 16 : 2001
Hispania U-19
Kombe la Ulaya la Chini ya miaka 19 Kandanda michuano: 2002
Timu kubwa Hispania
Soka Ulaya UEFA michuano ya (2): 2008, 2012
Kombe la Dunia: 2010
TUZO BINAFSI
1.Mfungaji bora Kombe la nike : 1999
2.Algarve cup Mchezaji wa Mashindano: 2001
3.Algarve mashindano mfungaji bora: 2001
5.Kombe la Ulaya la Chini-16 mfungaji bora: 2001
6.Kombe la Ulaya la Chini ya 19 Mchezaji bora wa Mashindano: 2002
7.Kombe la Ulaya la Chini ya 19 mfungaji bora wa michuano Soka: 2002.
8.Ligi Kuu ya PFA Timu ya Mwaka (2): 2007-08, 2008-09
9.Ligi Kuu ya Mchezaji wa Mwezi (2): Februari 2008, Septemba 2009.
10.Ligi Kuu mfungaji bora wa Mwezi (2): Aprili 2009, Machi 2010.
11.UEFA Euro Timu ya mashindano: 2008
12.UEFA Timu ya Mwaka: 2008
13.FIFPro World XI mchezaji bora (2): 2008, 2009
14.FIFA World Mchezaji bora wa Mwaka : 2008
15.Ballon d'Or Nafasi ya tatu: 2008
16.Kombe la Shirikisho la Silver Boot: 2009
18.UEFA Euro Golden Boot: 2012
TUZO ZA KIENYEJI"
1.Mkuu wa Asturias tuzo kwa ajili ya Michezo: 2010
2.Medali ya dhahabu ya Mpango Royal ya Michezo kiutamaduni: 2011.
RAFAEL BENITEZ ATEULIWA KUWA KOCHA MPYA NAPOLI
Klabu ya Italy Napoli imemteuwa Rafael Benitez, Miaka 53 kuwa Meneja mpya wa klubu hiyo ambayo katika Msimu huu imeshika Nafasi ya Pili nyuma ya Mabingwa Juventus.
Msimu ujao wa 2013/14, Napoli itacheza UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
katika suala nzima la benitez kutua hapo ni kutokana na aliyekuwa Meneja wa club hiyo Walter Mazzarri, alitangazwa kuiacha Napoli na kuhamia Inter Milan.
Uteuzi huo wa Benitez ulithibitishwa na Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis ambae alimsifia Benitez na kumwita Kocha mwenye ujuzi wa Kimataifa.
aidha Benitez ndio kwanza amemaliza Kibarua cha kuwa Meneja wa muda Klabuni Chelsea na, Wiki mbili zilizopita, hapo Mei 15, aliiwezesha Chelsea kutwaa Kombe la EUROPA LIGI baada ya kuichapa Benfica Bao 2-1 kwenye Fainali.
hata hivyo Benitez aliteuliwa Meneja wa muda wa Chelsea Novemba Mwaka jana baada ya kufukuzwa Roberto Di Matteo.
LEWANDOWSKI ANANAFASI KUBWA KWENDA MUNICH-WAKALA
WAKALA
wa mshambuliaji nyota wa klabu ya Borussia Dortmund, Robert Lewandowski
amesema kuna uwezekano mkubwa wa mshambuliaji huyo kujiunga na mabingwa
wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya Bayern Munich. Hata
hivyo, wakala huyoaitwaye Cezary Kucharski aliiambia luninga moja
nchini Ujerumani kwamba Bayern bado hawajafikia makubaliano ya mambo
binafsi ya nyota huyo wa kimataifa wa Poland. Wakala
huyo aliendelea kusema kuwa wao wako tayari lakini badi hawajasaini
chochote kwasababu klabu nayo inatakiwa iafiki makubaliano hayo. Bayern
ambao ni mabingwa wapya wa Ujerumani tayari wamemnyakuwa kiungo wa
Dortmund Mario Gotze mwenye umri wa miaka 20 kwa ada ya euro milioni 37.
TORRES VS CASILLAS WAITWA TIMU YA TAIFA
KOCHA wa timu ya taifa
ya Hispania, Vicente del Bosque amemuita golikipa Iker Casillas na
mshambuliaji Fernando Torres katika kikosi cha wachezaji 26 ambacho
kitaanza maandalizi ya Kombe la Shirikisho linalotarajiwa kuanza mwezi
ujao nchini Brazil. Orodha
hiyo ya wachezaji 26 itapunguzwa na kufikia 23 baada ya mzunguko wa
mwisho wa mechi za Ligi Kuu nchini Hispania mwishoni mwa wiki ijayo. Hispania
ambao ni mabingwa wa Dunia na Ulaya wana mechi mbili za kimataifa za
kirafiki dhidi ya Haiti Juni 8 na Ireland siku tatu baadae kabla ya
kuelekea nchini Brazil. Katika
michuano ya Kombe la Shirikisho, Hispania imepangwa katika kundi B
sambamba na Uruguay, Tahiti na Nigeria ambapo mchezo wa ufunguzi
utachezwa Juni 16 dhidi ya Uruguay.
Michuano hiyo ambayo inashirikisha timu nane inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 15 mpaka 30.
Goalkeepers: Iker Casillas (Real Madrid), Victor Valdes (Barcelona), Pepe Reina (Liverpool)
Defenders: Alvaro Arbeloa (Real Madrid), Sergio Ramos (Real Madrid), Gerard Pique (Barcelona), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Jordi Alba (Barcelona), Ignacio Monreal (Arsenal), Raul Albiol (Real Madrid), Javi Garcia (Manchester City)
Midfielders: Javi Martinez (Bayern Munich), Xavi (Barcelona), Andres Iniesta (Barcelona), Sergio Busquets (Barcelona), Santi Cazorla (Arsenal), Xabi Alonso (Real Madrid), Benat Etxebarria (Real Betis)Forwards: Cesc Fabregas (Barcelona), David Villa (Barcelona), David Silva (Manchester City), Roberto Soldado (Valencia), Pedro (Barcelona), Juan Mata (Chelsea), Jesus Navas (Sevilla), Fernando Torres (Chelsea).

Subscribe to:
Posts (Atom)