Monday, June 24, 2013

NIGERIA YATUPWA NJE KATIKA MICHUANO YA KOMBE LA MABARA 3-0

Timu ya taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles ambao ni mabingwawa Afrika katika michuano ya CHAN  imeondolewa kwenye michuano ya kombe la mabara baada ya kutandikwa mabao 3-0 na mabingwa wa dunia Hispania. Mabao mawili ya beki wa klabu ya Barcelona, Jordi Alba na moja la mshambuliaji wa Chelsea, Fernando Torres yalitosha kuisambaratisha Nigeria ambao wameshinda mechi moja pekee dhidi ya Tahiti wikiendi iliyopita. Nigeria wameyaaga mashindano hayo baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye kundi B wakiwa na pointi tatu nyuma ya Uruguay walioko kwenye nafasi ya pili wakiwa na point sita. Hispania ni vinara wa kundi B wakiwa wamemaliza hatua ya makundi na ushindi wa asilimia mia moja wakiwa na pointi tisa ambapo sasa watakwenda kuwavaa Italia katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo hapo siku ya siku ya alhamisi mjini Fortaleza. Uruguay wao wametoa kipigo cha magoli 8-0 kwa timu chovu kwenye michuano hiyo Tahiti ambao wameondoka na jumla ya magoli 24 ya kufungwa na kupata bao moja pekee walipocheza na Nigeria. Kwa matokeo hayo, Uruguay watacheza nusu fainali dhidi ya wenyeji Brazil, hapo siku ya jumatano.
MATOKEO
Uruguay 8
*Abel Mathias Hernandez Dakika ya 2, 24, 45 & 67 [Penati]
*Diego Perez 27
*Nicolas Rodiero 62
*Luis Suarez 82 & 88
     vs 
Tahiti 0
>>>>>
Spain 3
    vs
Nigeria
>>>>>
Nusu fainali
Jumanne Juni 26
Brazil v Uruguay
Muda saa 4 usiku
uwanja:Belo Horizonte
Jumatano Juni 27
Spain v Italy
uwanja Fortaleza
Muda saa 4 usiku
Mshindi wa tatu
Jumapili Juni 30
uwanja Salvador
Saa 1 usiku
Fainali
Jumapili Juni 30
Rio De Janeiro

Saturday, June 22, 2013

AFRICAN LYON YAJIPANGA KURUDI LIGI KUU TANZANIA BARA.

Mwanariadha nyota wa Marekani, Tyson Gay amefanikiwa kufuzu kushiriki mbio za mita 200 za duniani zitakazofanyika jijini Moscow kwa kutumia muda wa sekunde 19.74 ambao ni muda wa haraka zaidi kwa mwaka huu. Gay ambaye ni bingwa wa dunia wa mwaka 2007, sasa atachuana na mwanariadha mwenye kasi zaidi duniani kutoka Jamaica, Usain Bolt katika mbio za mita 100 na 200 kwenye mashindano ya dunia yatakayofanyika jijini Moscow, Urusi Agosti mwaka huu. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka aliwashinda Isiah Young aliyeshika nafasi ya pili na Curtis Mitchell alishika nafasi ya tatu. Kwa upnde wa wanawake mwanadada nyota katika mbio fupi kutoka Marekani Allyson Felix alishindwa kutamba kwenye mbio za mita 200 baada kushindwa na Kimberlyn Duncan.

MASAU BWIRE ASEMA TUPO VIZURI MSIMU UJAO WA VPL


Timu ya soka Ruvu Shooting Maafande wa kibaha mkoani pwani chini ya kocha Charles Boniface Mkwasa “Masta” wamendelea kutangaza vita kwa klabu za ligi kuu Tanzania bara msimu ujao, hususani Simba, Yanga na Azam fc.
Afisa habari wa klabu hiyo Masau Bwire akizungumza na mkali wa dimba amesema kuwa msimu ujao wa ligi kuu hakuna kulala, watapambana kufa na kupona kuhakikisha wanapata nafasi tatu za juu.
Masau amesema katika kuhakikisha wanafanikisha doto zao wameendelea kufanya vizuri katika usajili na mpaka sasa wamepata nyota watano.
Mchezaji  Juma Seif Dion "Kijiko" aliyekuwa akiichezea Africon Lyon msimu uliyopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara naye amejiunga na Ruvu Shooting ya Pwani kwa mkataba wa miaka miwili.
Kijiko aliyewahi pia kukipiga Yanga, alisaini mkataba huo  hivi karibuni katika ofisi za timu hiyo Mlandizi, Kibaha tayari kuitumikia kwa msimu ujao.
Kijiko ni mchezaji wa tano kusaini mkataba na timu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa ligi, wengine waliosaini ni Ciosmas Ader (Azam), Elias Maguli (Prison), Juma Nade (Kagera Sugar) na Lambale Jerome (Ashanti).
Wakati huo huo, uongozi wa timu hiyo ya Ruvu Shooting umetangaza kuwaacha wachezaji watano kutokana na kiwango chao cha kucheza mpira kushuka.
Aidha Masau Bwire amewataja wachezaji hao kua ni Pail Ndauka, Charles Nobart, Gido Chawala, Frank Mabande na Liberatus Manyasi.
Kwa mujibu wa Bwire, timu hiyo tayari iko kambini kikosi cha Jeshi 832 Ruvu JKT, itaanza mazoezi rasmi siku ya Jumatatu, Juni 24 chini ya Kocha Mkuu, Charles Mkwasa.
Bwire amewataka wachezaji wote ambao kawajaripoti kambini wafike haraka kabla ya Jumatatu ikiwa ni pamoja na wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu.

BLANC AKUBALIANA NBA PARIS SAINT-GERMAIN YA FRANCE

PSG" Club ya soka ya ufaransa Paris Saint-Germain- imefikia makubaliano na kocha Laurent Blanc kuwa meneja mpya wa klabu hiyo ambao ndio mabingwa wa Ligi Kuu nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1 msimu uliopita. Blanc mwenye umri wa miaka 45 amekaa bila kibarua toka alipoacha kuinoa timu ya taifa ya Ufaransa kufuatia kuenguliwa katika hatua ya robo fainai katika michuano ya Ulaya mwaka jana. Blanc ambaye alikuwa beki enzi zake akicheza soka amewahi kufundisha katika klabu ya Bordeaux kuanzia mwaka 2007 mpaka 2010 na kuisaidia timu hiyo kunyakuwa taji la Ligue 1 mwaka 2009. Hatua hiyo ya PSG imekuja kufuatia kocha wa sasa wa klabu hiyo Carlo Ancelotti kuomba kuondoka baada ya kuinoa kwa miezi 18 huku kukiwa na tetesi kuwa anataka kwenda Real Madrid ya Hispania. 

USAIN BOLT AFUZU KUSHIRIKI MBIO ZA MITA 100 ZA DUNIA.

Usain Bolt mwanariadha nyota wa mbio fupi kutoka Jamaica amefanikiwa kutinga hatua ya kushiriki mbio za mita 100 za dunia kwa kushinda michuano ya mchujo iliyofanyika nchini kwake kwa kutmia muda wa sekunde 9.94. Katika mbio hizo Bolt alianza taratibu lakini aliongeza kasi zaidi alipofikia mita 50 na kumkumpita Nickel Ashmeade na kujihakikishia nafasi ya kwenda jijini Moscow katika michuano ya dunia ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi kuanzia Agosti 10 mpaka 18. Mjamaica mwingine mkali katika mbio Yohan Blake yeye alishindwa kushiriki mbio za kuvuzu za mita 200 kwasababu ya majeraha lakini atashiriki mbio za mita 100 kama bingwa mtetezi baada ya Bolt kuenguliwa katika mbio hizo kwenye michuano ya dunia iliyofanyika jijini Daegu mwaka 2011. Kwa upnde wa Marekani nyota wa mbio hizo Tyson Gay naye amefanikiwa kukata tiketi ya kwenda Moscow baada ya kumshinda Justin Gatlin katika mbio za mita 100 kwa kutuimia muda wa sekunde 9.75 ukiwa ni muda wake wa haaka zaidi kwa mwaka huu.

ACCELOTT MTAZAMA ROONEY KWA JICHO LA TATU ZAIDI"

Carlo Ancelott ambaye kwa sasa ni kocha mpya wa Real Madrid, katika moja ya harakati zak ni kumsajili Wayne Rooney majira haya ya joto kama mshambuliaji huyo asiye na furaha atashindwa kumaliza tofauti zake na Manchester United.
Katika hali ya kawaida tunafahamu kabisa Rooney anapenda zaidi kuungana na Jose Mourinho ndani ya Chelsea ikiwa atamaliza miaka yake tisa ya kuishi United, lakini Madrid itakuwa na nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ikiwa ataondoka.
Klabu zote  hizi mbili zina uwezo sana tu wa kulipa Pauni Milioni 30 za ada ya uhamisho wake na kumlipa mchezaji mwenyewe mshahara wa Pauni 250,000 kwa wiki.

Kocha wa zamani wa Chelsea, Ancelotti anatarajiwa kuthibitishwa kuwa mrithi wa Mourinho Jumatatu na atakabidhiwa orodha ya wachezaji wanaotakiwa, wakiwemo Rooney, Gareth Bale, Edinson Cavani na Luis Suarez.
Rooney, ambaye amebakiza miaka miwili katika Mkataba wake, atakuwa na mazungumzo na kocha mpya wa United, David Moyes baada ya wote kurejea baada ya wote kurejea kutoka mapumzikoni siku chache zijazo, lakini inaonekana kama atabadilisha mawazo yake juu ya kwenda kuanza maisha mapya. 
Wakati huo huo, kocha wa zamani wa Ufaransa, Laurent Blanc anajiandaa kurithi mikoba ya Ancelotti ya ukocha wa Paris Saint-Germain.

Baada ya mpango wa mabingwa hao wa Ufaransa kumchukua kocha wa zamani wa England, Fabio Capello kukwama, sasa beki wa zamani wa Manchester United, Blanc, mwenye umri wa miaka 47 atapewa mikoba

Makubaliano Kati ya Laurent Blanc na Paris St Germain  yamefikiwa leo yeye kuwa kocha mpya wa klabu ya Jiji  hapa ni kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa.
Makubaliano baina ya kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa na PSG yamekubaliwa kwa miaka miwili. Ilipangwa kwamba, atasaini Mkataba wiki ijayo,

Friday, June 21, 2013

NAE DAVID LUHENDE APATA NAFASI AONGEZWA KATIKA KIKOSI CHA TAIFA STARS.


BEKI wa Yanga, David Luhende ameongezwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kwa ajili ya mechi dhidi ya Uganda (The Cranes) kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Afrika Kusini.

Kocha Kim Poulsen amesema kutokana na uamuzi huo wa kumuongeza beki huyo wa kushoto amemuondoa mchezaji mmoja kwenye kikosi chake. Mchezaji huyo ni mshambuliaji Zahoro Pazi wa JKT Ruvu.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager sasa itaingia kambini kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam, Julai 3 mwaka huu badala ya Julai 4 mwaka huu kama ilivyokuwa imepangwa awali.

Mechi ya Uganda itachezwa Julai 13 mwaka huu, saa 9 kamili alasiri kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati ile ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye jijini Kampala, Uganda.

Wachezaji wanaotakiwa kambini ni Aggrey Morris (Azam), Aishi Manula (Azam), Ally Mustafa (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruni Chanongo (Simba), John Bocco (Azam), Juma Kaseja (Simba), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar) na Kelvin Yondani (Yanga).

Wengine ni Khamis Mcha (Azam), Mrisho Ngasa (Simba), Mudathiri Yahya (Azam), Mwadini Ali (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Nadir Haroub (Yanga), Salum Abubakar (Azam), Shomari Kapombe (Simba), Simon Msuva (Yanga) na Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar).
TIMU NNE KUCHEZA NUSU FAINALI RCL
Timu nne zimefuzu kucheza hatua ya nne (nusu fainali) ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) baada ya kushinda mechi zao za hatua ya tatu ya michuano hiyo itakayotoa washindi watatu watakaocheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao.
Katika hatua hiyo Polisi Jamii ya Mara itaikaribisha Kimondo SC ya Mbeya kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma wakati Stand United FC ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Friends Rangers ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Azam Chamazi.

Mechi za kwanza zitachezwa Juni 23 mwaka huu wakati zile za marudiano zitafanyika kwenye viwanja vya Sokoine jijini Mbeya na Kambarage mjini Shinyanga, Juni 30 mwaka huu.

Kwenye hatua ya tatu ya RCL, Friends Rangers iliing’oa Kariakoo ya Lindi kwa jumla ya mabao 2-0, Stand United FC ikaitoa Machava FC ya Kilimanjaro kwa mabao 2-1, Kimondo SC ikaishinda Njombe Mji mabao 6-5 wakati Polisi Jamii iliitambia Katavi Warriors kwa mabao 7-6.

Hatua ya mwisho ya ligi hiyo itachezwa Julai 3 mwaka huu kwa mechi za kwanza wakati zile za marudiano zitakuwa Julai 7 mwaka huu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)