Monday, June 24, 2013

NIGERIA YATUPWA NJE KATIKA MICHUANO YA KOMBE LA MABARA 3-0

Timu ya taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles ambao ni mabingwawa Afrika katika michuano ya CHAN  imeondolewa kwenye michuano ya kombe la mabara baada ya kutandikwa mabao 3-0 na mabingwa wa dunia Hispania. Mabao mawili ya beki wa klabu ya Barcelona, Jordi Alba na moja la mshambuliaji wa Chelsea, Fernando Torres yalitosha kuisambaratisha Nigeria ambao wameshinda mechi moja pekee dhidi ya Tahiti wikiendi iliyopita. Nigeria wameyaaga mashindano hayo baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye kundi B wakiwa na pointi tatu nyuma ya Uruguay walioko kwenye nafasi ya pili wakiwa na point sita. Hispania ni vinara wa kundi B wakiwa wamemaliza hatua ya makundi na ushindi wa asilimia mia moja wakiwa na pointi tisa ambapo sasa watakwenda kuwavaa Italia katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo hapo siku ya siku ya alhamisi mjini Fortaleza. Uruguay wao wametoa kipigo cha magoli 8-0 kwa timu chovu kwenye michuano hiyo Tahiti ambao wameondoka na jumla ya magoli 24 ya kufungwa na kupata bao moja pekee walipocheza na Nigeria. Kwa matokeo hayo, Uruguay watacheza nusu fainali dhidi ya wenyeji Brazil, hapo siku ya jumatano.
MATOKEO
Uruguay 8
*Abel Mathias Hernandez Dakika ya 2, 24, 45 & 67 [Penati]
*Diego Perez 27
*Nicolas Rodiero 62
*Luis Suarez 82 & 88
     vs 
Tahiti 0
>>>>>
Spain 3
    vs
Nigeria
>>>>>
Nusu fainali
Jumanne Juni 26
Brazil v Uruguay
Muda saa 4 usiku
uwanja:Belo Horizonte
Jumatano Juni 27
Spain v Italy
uwanja Fortaleza
Muda saa 4 usiku
Mshindi wa tatu
Jumapili Juni 30
uwanja Salvador
Saa 1 usiku
Fainali
Jumapili Juni 30
Rio De Janeiro