![]() | |||
Taarifa kuhusu yeye | |||
---|---|---|---|
Full name | David Josué Jiménez Silva | ||
Date of birth | 8 January 1986 | ||
Place of birth | Arguineguín, Spain | ||
Height | 1.70 m (5 ft 7 in) | ||
Playing position | Attacking midfielder / Winger | ||
Taarifa kuhusu club | |||
Current club | Manchester City | ||
Number | 21 | ||
Timu za Ujana | |||
1995–2000 | UD San Fernando | ||
2000–2003 | Valencia | ||
Timu za Ukubwa | |||
Mwaka | Timu | Mechi | Goli |
2003–2004 | Valencia B | 14 | (1) |
2004–2010 | Valencia | 119 | (21) |
2004–2005 | Eibar (mkopo) | 35 | (4) |
2005–2006 | Celta Vigo (mkopo) | 34 | (4) |
2010– | Manchester City | 103 | (14) |
Timu ya Taifa | |||
2001–2002 | Spain U16 | 6 | (2) |
2002–2003 | Spain U17 | 20 | (5) |
2004–2005 | Spain U19 | 14 | (5) |
2005 | Spain U20 | 5 | (4) |
2004–2006 | Spain U21 | 9 | (7) |
2006– | Spain | 74 | (20) |
David Josué Jiménez Silva alizaliwa 8 Januari 1986 Arguineguín huko Las Palmas Hispain ni mchezaji mpira
mhispania ambaye kwa sasa anachezea timu ya Man city na timu ya taifa ya
Uhispania.Silva ana uwezo wa
kucheza upande wowote au kama namba 10 na
wakati mwingine kama mshambulizi msaidizi.Ni mchezaji mwenye mwili
mdogo, na mara nyingi hulinganishwa na Aimar Pablo, alipochukua nafasi yake
huko Valencia, akivalia nambari iliyohusishwa sana na Aimar; namba 21.
|
WASIFU WA KLABU
Silva alianza kucheza
mpira wa kulipwa msimu wa 2004-05 katika Ngazi ya pili katika timu ya SD Eibar,
akiwa amekopwa kutoka Valencia CF na alicheza mechi 35 katika daraja hilimna
kufunga mabao matano.Msimu uliofuatia, alikopwa tena, lakini wakati huu alikopwa
na timu ya Celta de Vigo, ambapo alicheza mechi 34, na kufunga mabao
manne.
Baada ya kucheza mechi
mbili ambazo aliingia uwanjani katika dakika za mwisho za mechi hizo, ambapo
mechi ya kwanza iliisha kwa Celta de Vigo kushinda 2-0 nyumbani dhidi ya Malaga
CF tarehe 28 Agosti 2005.
Silva akamaalizia msimu
huo kama mshambulizi bora huku timu hii ya Kigalisia ikifuzu katika kombe la
UEFA moja kwa moja kutoka daraja la pili.Katika misimu miwili, alikosa kucheza
mechi sita tu ilhali alifunga mabao 14 (bao la kwanza alilifunga tarehe 5
Novemba 2006 katika tasa ya 1-1 ugenini RCD Espanyol). Baada ya kutocheza kwa
muda wa miezi mitatu kutokana na jeraha la kisigino ambapo alifanyiwa upasuaji,
Silva alirejea kikosini
katikati mwa Desemba.Silva aliwakilishwa Uhispania akiwa na Cesc Fabregas mara
ya kwanza mwaka wa 2003 katika michezo ya ubingwa duniani ya FIFA ya wachezaji
wasiozidi umri wa miaka 17 huko Finland, ambapo alifunga mabao matatu.
Mwaka wa 2006, alijiunga
na timu ya Uhispania ya wachezaji wasiozidi umri wa 21 na alifunga mabao manne
katika kombe la vijana duniani la FIFA mwaka 2005; hii ilimwezesha kunyakua
nafasi ya 4 katika orodha ya wafungaji bora, pamoja na mshambulizi mwitaliano
Graziano Pellè.
WASIFU WA TIMU YA
TAIFA
Tarehe 22 Agosti 2007,
Silva aliifungia Uhispania mabao yake ya kwanza kikosini mwa Uhispania, na
alifunga mara mbili katika mechi hiyo ambapo waliishinda Ugiriki 3-2 katika
mechi ya kirafiki.
Baadaye aliitwa ajiunge
na kikosi cha wachezaji 23 ambao wangeiwakilisha nchi yao katika dimba la Euro
2008.
Katika nusu fainali Silva
alifunga bao la tatu la Uhispania dhidi ya Urusi baada ya ushambulizi wa haraka
ambayo Cesc Fabregas alimpigia krosi Silva, ambaye alitia mpira ndani ya lango
la Igor Akinfeev kwa kutumia mguu wake wa kushoto.
Katika fainali, Silva
alihusika katika tukio fulani na mjerumani Lukas Podolski. Baada ya kumvuta
Podolski chini, Podolski alimwenedea Silva na kuzua ubishi mkali ambao
haukuadhibiwa na mwamuzi.
Muda mfupi baadaye, kocha
wa timu ya Uhispania, Luis Aragonés, alimwondoa Silva na kuleta Santi Cazorla
ili kuzuia wezekano la vita.