Wednesday, August 6, 2014

SIMBA YA MNASA ABDI BANDA WA COASTAL UNION

CLUB ya Simba sc wazee wa Msimbazi wamefanikiwa kumsajili beki wa kushoto wa Coastal Union Abdi Banda baada ya kumuweka kwenye rada zake kwa muda mrefu.
Nyota huyo kinda mwenye uwezo wa kucheza nafasi zote za ulinzi, lakini beki ya kushoto ndio mahala pake haswaa , alisaini mkataba wa miaka mitatu jana na mara moja atajiunga na kikosi cha Simba kinachofanya mazoezi chini ya kocha mkuu, Mcroatia, Zdravko Logarusic.

Banda aliwahi kuripotiwa kuwindwa na Yanga katika dirisha dogo la usajili mwaka huu, lakini ilishindikana kwasababu alikuwa na mkataba na wagosi wa kaya na viongozi wa klabu hiyo walilalamika kitendo cha wanajangwani kumrubuni kijana huyo.

YANGA WAISHANGA CECAFA KUWEKA PEMBENI.

UONGOZI wa klabu ya Young Africans leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu na kusema kilichofanywa na waandaji wa michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuiondoa timu isishiriki ni cha kushangaza sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.

Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema walipata barua ya mwaliko wa kushiriki mashindano tarehe 25/7/2014 na kudhibitisha kushiriki michuano hiyo kwa kuandika barua iliyokwenda TFF na kisha wao kuiwasilisha kwa CECAFA.

Tuesday, August 5, 2014

AZAM FC YACHUKUA NAFASI YA YANGA KAGAME CUP 2014 BAADA YA YANGA SC KUSUASUA.

BARAZA la vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki na kati, CECAFA limeiengua rasmi klabu Yanga kushiri kombe la Kagame 2014 na nafasi yake imechukuliwa na mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc.
Tangu awali, CECAFA walitoa taarifa kuwa Azam watapewa nafasi ya upendeleo katika michuano hiyo inayoanza kushika kasi Agosti 8 mwaka huu, mjini Kigali nchini Rwanda, lakini mpaka jana wana Lambalamba walikuwa hawana taarifa rasmi.
azam-vs-yanga
Yanga sc ndio walitakiwa kushiriki michuano hiyo, lakini waliamua kupeleka kikosi B ambapo CECAFA ilikikataa na kuitaka timu hiyo ya makutano ya Twiga na Jangwani, Kariokoo jijini Dar es salaam ipeleke kikosi cha kwanza pamoja na kocha mkuu, Mbrazil Marcio Maximo.
Lakini Baada ya Yanga sc kuenguliwa kushiriki michuano ya klabu bingwa kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati , maarufu kama Kombe la Kagame, kwa kugoma kupelekea kikosi cha kwanza kama walivyoagizwa, Shirikisho la soka Tanzania TFF, limesema klabu hiyo ina haki kutoshiriki mashindano kama inaona haijajiandaa.
Boniface Wambura Afisa habari na mawasiliano wa TFF, Mgoyo huu mchana huu ameumbia mtandao wa mkali dimba tz kuwa klabu inapokuwa bingwa, hakuna kanuni inayoibana kwamba lazima ishiriki mashindo fulani, bali kama wanaona hawapo tayari wanaweza kuwasiliana na TFF, halafu klabu nyingine inatafutwa.

MALINZI ATUMA RAMBIRAMBI MSIBA WA MAKAMU WA RAIS FIFA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Shrikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Sepp Blatter kutokana na kifo cha makamu wake mwandamizi Julio Grondora.
julio1 Amesema yeye binafsi na jamii ya mpira wa miguu Tanzania kwa ujumla wanaomboleza msiba wa Grondora ambaye pia alikuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Argentina (AFA).
 Ameongeza kuwa Grondora alikuwa mtumishi mwandamizi wa mpira wa miguu, kwani alijitoa katika kuutumikia mpira wa miguu, na mchango wake katika maendeleo ya mchezo huo utaendelea kukumbukwa wakati wote.
 Rais Malinzi amesema familia ya mpira wa miguu nchini Argentina imepata pigo, na ametoa pole kwa familia ya marehemu, AFA na familia nzima ya FIFA na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
 Bwana ametoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina.

Monday, August 4, 2014

WASIWASI MCHEZO UMEIGHARIMU TAIFA STARS- NOOIJ

KOCHA TAIFASTARSKocha wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema moja ya sababu za kikosi chake kupoteza mechi dhidi ya Msumbiji (Mambas) ni wachezaji wake kucheza kwa wasiwasi katika kipindi cha kwanza.

Taifa Stars iliruhusu bao la kwanza sekunde chache kabla ya kumalizika kipindi cha kwanza katika mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kucheza hatua ya makundi iliyochezwa leo (Agosti 3 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa wa Zimpeto hapa Maputo.
KOCHA TAIFASTARS
Bao hilo katika mechi hiyo iliyomalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 4-3 lilifungwa kwa kichwa na mshambuliaji Josemar Machaisse.

Nooij alisema wasiwasi katika kipindi cha kwanza ndio ulioipa Msumbiji fursa ya kutawala mechi hiyo katika kipindi hicho na kukimalizia ikiwa mbele kwa bao hilo la mshambuliaji huyo wa klabu ya Bravos de Maquis ya Angola.

Alisema timu yake ilitulia kipindi cha pili baada ya kumuingiza Amri Kiemba badala ya Khamis Mcha. Pia alilalamikia bao ambalo Taifa Stars ilifunga dakika ya 16 kupitia kwa John Bocco lakini likakataliwa na mwamuzi Dennis Bate kutoka Uganda.

Aliongeza kuwa mchezaji Elias Pelembe aliyeifungia Msumbiji bao la pili dakika ya 83 kwa mpira wa adhabu nje ya eneo la hatari ndiye aliyemaliza mchezo huo. Pia ni mchezaji huyo aliyebadili matokeo ya mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam ambapo Msumbiji ilisawazisha dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, na ambayo ilicheza vizuri kipindi cha pili ilipata bao lake dakika ya 78 na Mbwana Samata kwa shuti la pembeni akiwa nje ya eneo la hatari na kumshinda kipa Ricardo Campos.
Matokeo hayo yameipeleka Msumbiji katika kundi C lenye timu za Cape Verde, Niger na Zambia. Mechi za hatua ya makundi kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco zitaanza kuchezwa mwezi ujao.

Mechi hiyo ndiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya Tanzania na Msumbiji itakayoingia hatua ya makundi ya michuano ya Afrika kwa ajili ya kutafuta tiketi za Fainali itakayofanyika mwakani nchini Morocco.

Katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2. Timu itakayosonga mbele itaingia kwenye kundi lenye timu za Cape Verde, Niger na Zambia.

Taifa Stars inarejea Dar es Salaam kesho (Agosti 4 mwaka huu) saa 8 mchana kwa ndege ya Air Tanzania.

Kikosi cha Stars kilipangwa hivi; Deogratias Munishi, Said Moradi, Shomari Kapombe, Kelvin Yondani, Nadir Haroub, Erasto Nyoni, Mwinyi Kazimoto, Mcha Khamis/Amri Kiemba, John Bocco/Simon Msuva, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu/Mrisho Ngasa

Tuesday, July 22, 2014

CECAFA KAGAME CUP: RATIBA HADHARANIYANGA KUANZA NA RAYON!

Ratiba ya Mashindano ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA KAGAME CUP, ambayo yatachua nafasi huko Kigali Nchini Rwanda kuanzia Agosti 8 na kumalizika Agosti 24.
Yanga, ambao walipangwa Kundi A, wataanza kwa kuivaa Rayon Sports ya Rwanda kwenye Uwanja wa Amahoro, Kigali hapo Ijumaa Agosti 8.
KMKM ya Zanzibar, ambao wako Kundi moja na Yanga, wataanza kwa kuivaa Atlabara ya South Sudan Siku hiyohiyo Agosti 8 kwenye Uwanja wa Nyamirambo huko Kigali.
MAKUNDI:
KUNDI A
-Rayon Sports [Rwanda]
-Yanga [Tanzania]
-Coffee [Ethiopia]
­-Atlabara [South Sudan]
-KMKM [Zanzibar]
KUNDI B
-APR FC [Rwanda]
-KCCA [Uganda]
-Flambeau de l'est [Burundi]
-Gor Mahia [Kenya]
-Telecom [Djibouti]
KUNDI C
-Vital'O [Burundi]
-El Merreikh [Sudan]
-Benadir [Somalia]
-Polisi [Rwanda]
Michezo yote zitachezwa Mjini Kigali kwenye Viwanja vya Amahoro na Nyamirambo huku Rubavu ikiwa ni Uwanja wa Akiba.
Tangu Mwaka 2002 Mdhamini wake mkuu ni Rais Paul Kagame wa Rwanda ambae amekuwa akitoa Dola 60,000 kila Mwaka.
Mashindano haya yatarushwa moja kwa moja kwenye TV na SuperSport International ambacho hivi karibuni kilisaini Mkataba wa Miaka Minne na CECAFA.
Ratiba kamili itatolewa baadae na CECAFA baada Timu zote kuthibitisha kushiriki.
Mbali ya kutwaa Kombe, Bingwa wa Kagame Cup huzoa Donge la Dola 30,000, Mshindi wa Pili Dola 20,000 na Timu ya Tatu hupata Dola 10,000.
RATIBA KAMILI:
TAREHE NA MECHI KUNDI UWANJA
Ijumaa Agosti 8 1 Atlabara v KMKM A NYAMIRAMBO
2 Rayon v Yanga A AMAHORO
3 Gor Mahia v KCCA B AMAHORO
Jumamosi Agosti 9 4 Vital ‘O’ v Banadir C AMAHORO
5 Police v El Mereikh C AMAHORO
6 APR v Flambeau B AMAHORO
Jumapili Agosti 10 7 KMKM v Young A AMAHORO
8 Telecom Vs KCCA B NYAMIRAMBO
9 Coffee v Rayon A AMAHORO
Jumatatu Agosti 11 10 Banadir v El Mareikh C NYAMIRAMBO
11 Gor Mahia v Flambeau B ‘’
12 Vital ’O’ v Police C ‘’
Jumanne Agosti 12 13 KMKM v Coffee A ‘’
14 Yanga v Atlabara A ‘’
Jumatano Agosti 13 15 APR  v Telecom B ‘’
16 KCCA v Flambeau B ‘’
Alhamisi Agosti 14 17 Coffee v Atlabara A
18 Rayon  v KMKM A
19 Police v Banadir C
Ijumaa Agosti 15 20 Flambeau v Telecom B
21 APR v Gor mahia B
22 El Mareikh v Vital ‘O’ C
Jumamosi Agosti 16 23 Coffee v Yanga A
24 Rayon v Atlabara A
Jumapili Agosti 17 25 Telecom v Gormahia B
26 KCC v APR B
Jumatatu Agosti 18 MAPUMZIKO

Jumanne Agosti 19 ROBO FAINALI

27 C1 v B3
NYAMIRAMBO
28 A1 v B2
‘’
Jumatano Agosti 20 29 A2 v C2
‘’
30 B1 v A3
‘’
Alhamisi Agosti 21 MAPUMZIKO

Ijumaa Agosti 22 NUSU FAINALI

31
32
Mshindi 27 v Mshindi 28
Mshindi 29 v Mshindi 30

AMAHORO
Jumamosi Agosti 23 MAPUMZIKO

Jumapili Agosti 24 MSHINDI WA 3 & FAINALI

33
34
Mfungwa 31 v Mfungwa 32
Mshindi 31 v Mshindi 32

AMAHORO
MUDA WA KUANZA MECHI UTAAMULIWA KATI YA CECAFA, FERWAFA NA SUPERSPORT KWA AJILI YA MATANGAZO LAIVU YA TV.

Sunday, July 20, 2014

STARS YALAZIMISHWA SARE 2-2 NA MAMBAS MSUMBIJI TAIFA

Timu ya taifa ya Tanzzania Taifa Stars Leo ikiwa katika dimba la uwanja wa taifa imejiweka katika wakatik mgumu kutinga Hatua ya Makundi ya kutafuta nafasi za kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, huko Morocco Mwakani, baada kutoka Sare 2-2 na Msumbiji kwenye Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Stars, wakiwa chini ya Kocha Mart Nooij ambae kati ya Mwaka 2007 na 2011 alikuwa Kocha wa Msumbiji, walitanguliwa kufungwa kwa Bao la Penati iliyopigwa na Domingues lakini walijitutumua na kusawazisha kwa Bao la Mcha Khamis ambae pia alifunga Bao la Pili kwa Penati.
Hata hivyo, kazi hiyo njema ilipotea bure baada ya kuwaruhusu Msumbiji kusawazisha katika Dakika ya 89 kwa Bao la Isaac Carvalho.
MAGOLI:
Tanzania 2
-Mcha Khamis Dakika ya 66 & 71 [Penati]
Mozambique 2
-Gaspar Domingues Dakika ya 48 [Penati]
-Isac Carvalho 89

Kwenye Mechi nyingine iliyochezwa Leo huko Setsoto Stadium, Maseru, Wenyeji Lesotho waliifunga Kenya Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 70 la Moletsane.
Mechi za Marudiano zitachezwa Wikiendi ya Agosti 1 hadi 3.
AFCON 2015-MOROCCO
RATIBA/MATOKEO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Julai 19
Uganda 2 Equatorial Guinea 0
Botswana 2 Guinea-Bissau 0
Sierra Leone 2 Seychelles 0
TFF-TANZANIA-MSUMBIJIJumapili Julai 20
Lesotho 1 Kenya 0
Tanzania 2 Mozambique 2
17:30 Congo v Rwanda
18:00 Benin v Malawi
** Mechi za Marudiano zitachezwa Wikiendi ya Agosti 1 hadi 3.
MAKUNDI:
KUNDI A
-Nigeria
-South Africa
-Sudan
-Mshindi Congo/Rwanda
KUNDI B
-Mali
-Algeria
-Ethiopia
Mshindi Benin/Malawi
KUNDI C
-Burkina Faso
-Angola
-Gabon
-Mshindi Lesotho/Kenya
KUNDI D
-Ivory Coast
-Cameroun
-Congo DR
-Mshindi Sierra Leone/Seychelles
KUNDI E
-Ghana
-Togo
-Guinea
Mshindi Uganda/Mauritania
KUNDI F
-Zambia
-Cape Verde
-Niger
-Mshindi Tanzania/Msumbiji
KUNDI G
-Tunisia
-Egypt
-Senegal
-Mshindi Botswana/Guinea-Bissau