Tuesday, August 26, 2014

TFF YAWEKA ADHABU KALI KWA WATOA RUSHWA KATIKA SOKA.

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imeamua kuanzia sasa adhabu kwa watu wanaotoa rushwa au kupanga matokeo katika mchezo huo itakuwa ni kufungiwa maisha kujishughulisha na mchezo huo.

Taarifa katika tovuti 
ya TFF imesema kwamba hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo juzi.

Kwa muda sasa, kumekuwa na tuhuma nyingi za wachezaji na marefa kuhongwa ili kupanga matokeo- lakini hakukuwa na sheria madhubuti ya kupambana na hali hiyo- lakini kwa hatua hii mpya ya TFF dhahiri itasaidia kupunguza mchezo huo mchafu. 

Aidha, baada ya Libya kujitoa kuwa mwenyeji wa Fainali za Afrika (AFCON) za 2017, Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limealika nchi wanachama kuomba uenyeji wa fainali hizo.
Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Agosti 24, mwaka huu imeamua Tanzania kuomba uenyeji wa fainali hizo.

“Tunatambua kuwa moja ya masharti ya kuandaa fainali hizo ni pamoja na nchi kuwa imeandaa moja ya mashindano ya vijana. Lakini kwa kuwa suala hili liko katika mazingira maalumu (exceptional circumstances) tunaamini CAF watafikiria ombi letu kwa msingi huo.

Awali Libya ilipewa uenyeji wa fainali hizo 2015, lakini zikahamishiwa Afrika Kusini kutokana na sababu za kiusalama. Hivyo, Libya ikapewa fainali za 2017 ambapo sasa imejitoa yenyewe kuandaa fainali hizo.

Wakati huo huo: Kamati ya Utendaji ya TFF imemteua Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi mpya wa Mashindano kuanzia Septemba 1 mwaka huu.


Kabla ya uteuzi huo, Wambura alikuwa Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF kuanzia Januari 1, 2011. Nafasi hiyo sasa iko wazi na itajazwa baadaye na Kamati ya Utendaji.

MAXIMO ASEMA ANAWATAMBUA WACHEZAJI WATANO TU YANGA.

Kocha mkuu Mbrazil kwenye Ligi ya Tanzania, Marcio Maximo ametamka kuwa anawajua wachezaji watano tu wa kigeni Yanga na ndio atakaowatumia Miongoni mwao jina la Okwi ambaye yupo Dar es Salaam halimo.
Maximo amesema atafanya kazi na Hamis Kiiza raia wa Uganda, Wanyarwanda Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite pamoja Wabrazili Andrey Coutinho na Genilson Santos ‘Jaja’ ndiyo anaowatambua.
Pamoja na wachezaji hao watano wanaofanya mazoezi ya pamoja, Yanga ina mkataba na Okwi anayefanya timu kuwa na wachezaji sita wa kigeni idadi ambayo hadi kesho Jumatano siku ya kufunga dirisha la usajili lazima ipunguzwe kwa mmoja kutupiwa virago.
Maximo amesema Okwi sijamwona na hajaripoti kwenye timu yangu nifanyaje". Nitafanya kazi na hao tu ambapo awali Kiiza ndiyo alikuwa aachwe, lakini sasa hali imeanza kuwa shwari kwake kutokana na nidhamu yake na jinsi anavyojituma mazoezini.
Okwi ambaye alikuwa anapewa kipaumbele lakini alichelewa kujiunga na timu kwa sababu zisizojulikana, inadaiwa kuwa uongozi umemwambia ajieleze kwa barua na baada ya hapo atapewa adhabu ambayo ni siri.Okwi alichelewa kuja kambini kujiunga na Yanga kwa madai kwamba hajalipwa fedha zake.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Leonardo Neiva ambaye pia ni Mbrazili amesema wamefurahishwa na uwezo wa  Kiiza na kukiri kuwa ana sababu zote za kubaki Yanga.

KOCHA WA POLISI MORO AWATAKA WACHEZAJI WAKE KUJITUMA VPL.


Kocha Mkuu wa Polisi Morogoro Adolf’ Rishard ameweka wazi kuhusu timu yake timu yake ifanye vizuri msimu huu, wachezaji wanatakiwa wajitume, washikamane na kucheza kama timu moja.

Adolf ameyasema hayo wakati akizungumza na mtandao huu ambapo amesema ushindi unawezekana kama wachezaji wake watakuwa wanazingatia maelekezo wanayopewa.
Adolf amesema malengo yetu makubwa msimu ujao ni kufanya vizuri, na hayo yote yatawezekana kutokana na jinsi wachezaji watakavyojituma na kucheza kiushindani.
Katika kuhakikisha lengo linatimia tayari imeshafanya usajili wa wachezaji kadhaa wakiwamo Salum Machaku, Edward Chistopher aliyekuwa Simba, Dan Mrwanda, Labana Kambone wa Rhino Rangers, Toni Kavishe wa Mgambo JKT, Seleman Selembi wa Coastal Union na Mohamed Mpopo wa Villa Squad.

NOOIJ AITA 26 STARS KUIKABILI MOROCCO SEPTEMBA 5 MWAKA HUU.

Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya FIFA Date dhidi
ya Morocco itakayochezwa Septemba 5 mwaka huu nchini Morocco.
Wachezaji walioitwa ni makipa Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni Said Morad (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Shomari Kapombe (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Azam), Aggrey Morris (Azam), Joram Mgeveke (Simba) na Charles Edward (Yanga).
Viungo ni Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba), Said Juma (Yanga) na Haruna Chanongo (Simba).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City) na Juma Liuzio 9ZESCO, Zambia).
Timu hiyo itaingia kambini Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) mchana katika hoteli ya Accomondia.
                      Mart Nooij
Taarifa Binafsi
Full nameMartinus Ignatius Nooij 
Date of birthJune 3, 1954 (age 60)
Place of birthHeemskerkNetherlands
Timu anayofundisha
Current team
Tanzania
Timu alizofundisha
YearsTeam
2003Burkina Faso U20
2007–2011Mozambique
2012Santos Cape Town
2013–2014Saint George
2014–Tanzania