Tuesday, June 4, 2013

KATIKA MISUKOSUKO YA HAPA NA PALE SASA ATUA COAST"


Baada ya kupata misukosuko ya hapa na pale katika Club ya wekundu wa msimbazi SC kiungo Haruna Moshi Shaaban ‘Boban hatimaye amefanikiwa kutua  ndani ya jiji la tanga kuichezea Coastal union mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
hivyo mpaka sasa Coastal union imekamilisha usajili wa wachezaji wanne wapya, akiwemo mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Zanzibar msimu huu, Abdallah Othman Ally. 
Ally anayecheza upande wa pembeni juu kushoto mwenye speed na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, amesaini Mkataba wa miaka miwili na Coastal Union ambayo tangu ipande tena Ligi Kuu mwaka juzi, imepania kurejesha makali yake. Mbali na Ally anayechezea pia timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes.
Wagosi wa Kaya wamemrejesha kiungo waliyemuibua mwaka 2000 kabla ya kufuata maslahi Moro United, baadaye Simba SC na Geffle FF ya Sweden’.
Boban amerejea Tanga alipoanzia kucheza soka ya ushindani mwaka 2000 chini ya kocha maarufu zamani Mansour Magram, sasa marehemu akitokea sekondari ya Makongo, Dar es Salaam.
Aidha wagosi hao pia imesajili wachezaji wawili kutoka JKT Oljoro ya Arusha, kipa Said Lubawa na sentahafu Marcus Ndehele ambapo Mwenyekiti wa  Coastal Union Hemed Aurora hmed akizungumza na mtandao huu ametanabaisha na kusema kuwa bado wanatazama harakati za kuwanasa wachezaji watano zaidi kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi.  

Aidha Aurora ameongeza na kusema kuwa huu ni usajili wa uliokuwa na malengo na si wa kukurupuka na pia vilevile ni usajili unaotokana na mapendekezo ya benchi la ufundi la timu chini ya kocha mkuu, Ahmed Morocco ambaye alitaka wachezaji tisa ambao aliwapendekeza kwa majina yeye mwenyewe na sisi tumekuwa tukimfuata mmoja baada ya mwingine na kumalizana naye.
Hivyo kwa wakati huu bado tupo kwenye harakati za kumalizana na wengine watano ambpo Lengo letu ni kuhakikisha kocha anakuwa na timu atakayoridhika nayo kulingana na mapendekezo yake, hatutaki kuingilia kusajili hata mchezaji mmoja, alisema Aurora.
Mbali na hilo Aurora ameudokeza mtandao huu kuwa miongoni mwa wachezaji hao waliobaki mtazamo zaidi ni kumnasa beki aliepatwa na misukosuko kama ya Boban yaani beki mwenye nguvu na na uwezo wa kukaba Juma Nyoso.

Hata hivyo Aurora ameongeza na kusema kuwa mazoezi ya Coastal Union yataanza wiki ya kwanza ya mwezi Julai mwaka huu, nje kidogo ya mji ambako kikosi kitapiga kambi kujiandaa kikamilifu kwa ajili ya msimu mpya.