Florentino Perez rais wa club ya Real
Madrid ametanabaisha kuwa ana mategemeo kuwa mshambuliaji nyota wa klabu
hiyo Cristiano Ronaldo atabakia Santiago Bernabeu katika kipindi chote
cha maisha yake ya soka. Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Ureno, mapema mwaka jana alidokeza kuwa hakuwa
anafurahia maisha ya Madrid na toka wakati huko amekuwa akihusishwa na
mpango wa kurejea Manchester United pamoja na Paris Saint-Germain-PSG. Lakini
Perez amedai kuwa atafanya kila awezalo ili nyota huyo aweze kuwa na
furaha katika klabu hiyo na kumalizika muda wake wa kucheza soka akiwa
hapo. Perez pia
aluzungumzia mustakabali ya mshambuliaji mwingine Gonzalo Higuain na
kudai kuwa hakuna yoyote aliyemwambia kwamba mchezaji huyo ataondoka
kwani klabu hiyo haijamuweka sokoni katika kipindi cha usajili. Ambapo
aliongeza kuwa kama mchezaji mwenyewe ndio anataka kuondoka basi klabu
itakayomhitaji itatakiwa kuwalipa lakini mpaka sasa ahkuna klabu yoyote
iliyojitokeza kumtaka mchezaji huyo.