NEYMAR ASEMA MESS ATAENDELEA KUTISHA ZAIDI DUNIANI.
MSHAMBULIAJI nyota mpya
wa klabu ya Barcelona, Neymar ametanabaisha anataka kumsadia nyota wa klabu
hiyo Lionel Messi aendelee kung’ara duniani baada ya kukamilisha
taratibu zote za uhamisho wake kutoka klabu ya Santos. Neymar
mwenye umri wa miaka alikamilisha uhamisho wake wenye thamani ya euro
million 57 na kumaliza utata wa miezi kadhaa juu ya mstakabali wa nyota
huyo. Akihojiwa
mara baada ya kutambulishwa rasmi mbele ya maelfu ya mashabiki katika
uwanja wa Camp Nou, Neymar amesema anataka kuisaidia timu kwasababu
Barcelona ni zaidi ya klabu na pia anataka kumsadia Messi aendelee
kung’ara zaidi. Nyota
huyo aliendelea kusema kuwa ilikuwa ni ndoto zake kucheza katika klabu
ambayo inahesabika kama mojawapo ya klabu bora duniani huku akizungukwa
na wachezaji nyota. Neymar
anaondoka Santos akiwa ameshinda Kombe la Brazil mwaka 2010, Kombe la
Klabu Bingwa ya Amerika Kusini mwaka 2011 huku akiwa amefunga mabao 138
katika mechi 229 alizocheza akiwa katika klabu hiyo.