KITUO
cha Redio cha Napoli, Marte kimetangaza kuwa dau la Pauni Milioni
49.3 limetolewa na Chelsea kwa ajili ya mshambuliaji Edinson Cavani
ambaye muda wote anampasua kichwa mmiliki wa klabu ya Chelsea Bilionea
Roman Abramovich mwenye lengo la kuimarisha kikosi chake chini ya kocha
Jose Mourinho.
Katika
taarifa ya jana usiku, Radio Marte ilitangaza: “Tumepokea taarifa
kutoka ofisini kwa vyanzo vya kuaminika kwamba, Napoli imekubaliana dili
la kuiuzia Chelsea Cavani.
Kitu moto: Chelsea sasa ipo katika nafasi ya kumnasa Edinson Cavani
“Rafa
Benitez pia amebariki, lakini kabla ya kutangaza rasmi, Napoli inataka
kupata mshambuliaji atakayeziba pengo la Il Matador.
“Aurelio De Laurentiis”, klabu itasomba kiasi cha Euro Milioni 58, sawa na dili la Ezequiel Lavezzi kwenda PSG mwaka jana.
“Mchezaji huyo atajiingizia mshahara wa Euro Milioni 8.5 kwa msimu pamoja na haki za picha,”. Habari zimevuja kama kwamba Cavani
ametangaza anataka kukutana uso kwa uso na Rais, Aurelio de Laurentiis
na kuna taarifa kwamba Manchester United nayo imo kwenye mbio hizo.
Mshambuliaji
huyo wa Uruguayna baba yake awali walionyesha nia ya kutaka kwenda Real
Madrid. Klabu hiyo ya Hispani iliwasiliana na Napoli, lakini sasa
itabidi waipiku ofa iliyotolewa na Chelsea.