Tuesday, September 23, 2014

CAF YAITIA KITANZI MIAKA 2 JS KABYLIE KWA KIFO CHA MCHEZAJI EBOSSE

CAF_CHAMPIONS_LEAGUE_LOGOKLABU ya Algerian JS Kabylie  imefungiwa Miaka Miwili kutocheza Mashindano ya Afrika kwa sababu ya Kifo cha Mchezaji wake kutoka Cameroon Albert Ebosse.
Albert Ebosse, mwenye Miaka 24, alipigwa Kichwani na Mawe wakati akitoka Uwanjani baada ya Timu yake JS Kabylie kufungwa Nyumbani kwao na USM Alger Bao 2-1 huko Tizi Ouzou0 huku Bao pekee la JS Kabylie likifungwa na Ebosse.
JS Kabylie  imefuzu kucheza CAF CHAMPIONZ LIGI Mwakani baada ya kumaliza Ligi ya Algeria ikiwa Nafasi ya Pili lakini sasa watayakosa Mashindano hayo.
Uamuzi huo wa CAF umetolewa huko Ethiopia kwenye Kikao chao ambacho pia kimeamua kutoa Tuzo ya kila Mwaka ya Mchezo wa Haki kwa Jina la Ebosse kwa Chama cha Soka kitakachoshinda viwango vya Uchezaji Haki ambavyo vitaamuliwa na Kamati Kuu ya CAF kufuatia utendaji wao kwenye Mashindano ya CAF.
Mbali ya Adhabu hii ya Kifungo toka CAF, Viongozi wa Soka huko Algeria tayari wameshaiadhibu JS Kabylie  kwa kuizuia kucheza Mechi zao za Nyumbani za Msimu wa 2014/15 kwenye Uwanja wao, 1st November 1954, na pia kuwapiga marufuku Washabiki wao kuhudhuria Mechi yeyote ya Klabu hiyo hadi mwanzoni mwa Mwaka ujao.
Mara baada ya maafa ya Kifo cha Ebosse, Shirikisho la Soka Algeria lilitoa Dola 100,000 kwa Familia ya Ebosse na pia kulipa Fedha zote ambazo angelipwa kwa muda wake wote wa Mkataba wake na Klabu ya JS Kabylie.
Pia kila Mchezaji wa JS Kabylie alijitolea Mshahara wake wa Mwezi mmoja kwa Familia ya Mchezaji huyo.