Kuelekea Mtanange wa Juma mosi Timu ya mbeya city itawakosa baadhi ya wachezaji wake watatu baada ya kuumia katika mechi ya jumamosi iliyopita dhidi ya JKT Ruvu iliyomalizika kwa suluhu ya bila kufungana, uwanja wa Sokoine, Mbeya, na watakaa nje ya uwanja kwa wiki mbili.
Akizungumza na Mkali wa dimba tz.blogspot Afisa habari wa mbeya city Dismas Ten amesema kuwa baada ya mechi iliyopita, wachezaji watano walipata majeruhi, lakini wawili kati yao watarejea uwanjani jumamosi ya septemba 27 kuchuana na Coastal Union.

Dismas aliongeza kuwa maandalizi ya mechi ya pili nyumbani yanakwenda vizuri na wachezaji wana morali ya kutafuta ushindi na kuendeleza rekodi yao ya msimu uliopita ambapo walimaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya Yanga na mabingwa Azam fc.
sanjari na hayo Dismas amesema kuwa Hali ya kambi ni nzuri, tunajiandaa vizuri na tunaamini tutaibuka na ushindi. Tulicheza mpira mkubwa sana dhidi ya JKT Ruvu.