Friday, November 7, 2014

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU MAHAKAMA ZA MWANZO KUAMUA MASHAURI YA KESI ZA ARDHI.

SERIKALI, imezipiga marufuku Mahakama za Mwanzo kuamua mashauri ya kesi za Ardhi kwani jukumu hilo ni la Mabaraza ya Ardhi ya Wilaya.
Onyo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angellah Kairuki, wakati alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nkenge, Assumpter Mshama (CCM), lililoulizwa kwa niaba yake na Mbunge wa Mwibara, Alphaxard Lugola (CCM).
Mbunge huyo ametaka kujua kwanini serikali isitoe kauli na tamko la kuwataka Mahakimu wa Mahakama za Mwanzo kutopokea kesi hizo na badala yake izipeleke kwenye mabaraza ya ardhi.
Amesema, kukomesha tabia ya mahakama za Mwanzo kuhukumu kesi la Ardhi serikali itawasiliana na Makama za mwanzo ili ziweze kuchukua hatua stahiki katika jambo hilo.
Kuhusu, ucheleweshwaji wa kesi taratibu  zinafahamika kwa wale ambao watakuwa na sababu za msingi lakini mahakama zimekuwa haziahirishi kesi bila sababu yoyote endapo itakuwa kusababu zimeeleweka kamati za mahakimu na za majaji wataweza kufuatilia na kuchukua hatua.