Uuzaji mchanganyiko wa tiketi za elektroniki kwenye Ligi Kuu ya
Vodacom (VPL) utakoma baada ya mechi mbili za wikiendi hii kati ya Yanga na
Mgambo Shooting na Simba na Ruvu Shooting zitakazochezwa Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Ligi itasimama kupisha mechi ya Kalenda ya
FIFA, mashindano ya Chalenji na dirisha dogo la usajili. Baada ya hapo tiketi
zote zitauzwa kwa njia ya mtandao, hivyo hakutakuwepo na vibanda vya kuuza
tiketi viwanjani.