MENEJA wa klabu ya
Borussia Dortmund, Jurgen Klopp ametanabaisha kuwa ataimarisha kikosi chake na
kufikia fainali nyingine ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kipigo
walichopata dhidi ya Bayern Munich. Dortmund
walipoteza mchezo huo ulizikutanisha timu zote kutoka Ujerumani kwa
mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Wembley baada ya bao la dakika za mwisho
lililofungw ana Arjen Robben. Lakini
kocha huyo ametamba kuwa pamoja na kushindwa katika fainali hiyo ya
Wembley lakini anaamini atafikia fainali nyingine katika kipindi kifupi
kijacho. Klopp
amesema kwasasa ana kazi kubwa ya kuimarisha kikosi chake baada ya
wachezaji kadhaa tegemeo kutaka kuondoka mwishoni mwa msimu huu lakini
anaamini mpaka kufikia msimu mpya tayari atakuwa na kikosi imara. Kiungo
tegemeo wa klabu hiyo Mario Gotze tayari imeshathibitishwa kwenda
Bayern Msimu ujao huku mshambuliaji wake nyota Robert Lewandowski naye
akijipanga kuelekea huko.
Monday, May 27, 2013
TAIFA STARS YAELEKEA ADDIS ABABA LEO.
TIMU ya Taifa ya
Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kuondoka leo (Mei 26 mwaka huu) usiku
kwenda Addis Ababa, Ethiopia ambapo itaweka kambi na kucheza mechi moja
ya kirafiki kabla ya kwenda Morocco. Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka saa 5 usiku kwa
ndege ya EgyptAir ikiwa na kikosi cha wachezaji 21 chini ya nahodha wake
kipa Juma Kaseja. Timu
hiyo ikiwa Ethiopia, Juni 2 mwaka huu itacheza mechi ya kirafiki dhidi
ya Sudan ambapo siku inayofuata itaondoka kwenda Marrakech, Morocco kwa
kupitia Cairo, Misri. Mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya
wenyeji Morocco itachezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.
Mbali
ya nahodha Kaseja, wachezaji wengine wanaoondoka katika kikosi hicho
ambacho kina wiki sasa tangu kingie kambini jijini Dar es Salaam ni
Mwadini Ally na Ally Mustafa ambao wote ni makipa. Wengine
ni Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Aggrey Morris, Haroub Nadir, Mwinyi
Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum
Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya,
Athuman Idd na Haruni Chanongo. Wachezaji
Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu ambao wako na timu yao ya TP Mazembe
ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo watajiunga moja kwa moja na Stars
jijini Marrakech, Juni 4 mwaka huu wakitokea Maputo, Msumbiji mara baada
ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Liga Muculumana ya huko. Katika
msafara huo wa Ethiopia benchi la ufundi la Stars linaundwa na Kim
Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi),Juma Pondamali
(Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja wa timu), Dk. Mwanandi
Mwankemwa (Daktari), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred
Chimela (Mtunza vifaa).
Saturday, May 25, 2013
30 TWIGA STARS WAITWA KAMBINI KESHO MEI 26 MWAKA HUU
Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ya wanawake ya mpira wa miguu (Twiga Stars), Rogasian
Kaijage amewaita kambini wachezaji 30 ikiwa ni mwendelezo wa kuijenga na
kuiimarisha timu hiyo.
Twiga
Stars itakuwa na kambi ya siku kumi kuanzia Jumapili (Mei 26 mwaka huu) ambapo
baadaye inatarajia kucheza mechi moja ya kirafiki kabla ya wachezaji kurudi
kwenye klabu zao.
Kambi
hiyo ni mwendelezo wa programu iliyopendekezwa na kocha kuijenga na kuiimarisha
timu hiyo kwa vile haina mashindano mwaka huu, na itakuwa kambi ya pili baada
ya ile iliyofanyika Machi mwaka huu.
Wachezaji
walioitwa na klabu zao kwenye mabano ni Asha Rashid (Mburahati Queens), Aziza
Mwadini (Zanzibar), Belina Julius (Lord Barden), Ester Chabruma (Sayari), Ester
Mayala (TSC Academy), Eto Mlenzi (JKT), Evelyn Sekikubo (Mburahati Queens) na
Fatuma Bushiri (Mburahati Queens).
Fatuma
Hassan (Mburahati Queens), Fatuma Omari (Sayari), Flora Kayanda (Tanzanite),
Hamisa Athuman (Marsh Academy), Hellen Peter (JKT), Maimuna Said (JKT), Mwajuma
Abdallah (Tanzanite), Mwanahamisi Omari (Mburahati Queens), Mwanaidi Tamba
(Mburahati Queens) na Mwapewa Mtumwa (Sayari).
Nabila
Ahmed (Marsh Academy), Pulkeria Charaji (Sayari), Rehema Abdul (Lord Barden),
Rukia Khamis (Uzuri Queens), Semeni Abeid (Tanzanite), Sharida Boniface
(Makongo Sekondari), Sophia Mwasikili (Sayari), Therese Yona (TSC Academy),
Vumilia Maarifa (Evergreen) na Zena Khamis (Mburahati Queens).
RCL
KUENDELEA KUTIMUA VUMBI KESHO
Raundi
ya pili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) inaendelea kesho (Mei 26 mwaka huu)
kwa mechi sita za kwanza zitakazochezwa katika miji sita tofauti.
Abajalo
ya Dar es Salaam na Kariakoo ya Lindi zitaumana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume, Dar es Salaam wakati Machava FC ya Kilimanjaro itakuwa mwenyeji wa
Mpwapwa Stars ya Dodoma kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
Nayo
Stand United FC ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Magic Pressure ya Singida kwenye
Uwanja wa Namfua mjini Singida huku Polisi Jamii ya Bunda mkoani Mara
ikimenyana na Biharamulo FC ya Kagera kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume
mjini Musoma.
Mjini
Kigoma kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika ni kati ya wenyeji Saigon FC na Katavi
Warriors ya Katavi wakati Njombe Mji itaikaribisha Kimondo SC ya Mbeya kwenye
Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.
Leo
(Mei 25 mwaka huu) Friends Rangers ya Kinondoni, Dar es Salaam inacheza na
African Sports ya Tanga kwenye Uwanja wa Azam Chamazi. Mechi za marudiano
zitachezwa kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu.
Timu
zitakazofuzu kucheza raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya Juni 8 na
9 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15 na 16 mwaka huu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Friday, May 24, 2013
UCL: WATOTO WA BABA MMOJA USO KWA USO WEMBLEY
NI FAINALI ya kukata na shoka hapo
Kesho katika dimba la uwanja wa wembley uliopo jijini london nchini uingereza
watoto wa baba mmoja kutoka ujerumani watavaana kucheza Fainali ya
Klabu Bingwa Ulaya ambapo Borussia Dortmund na Bayern Munich
watakukutana hapo kesho
Jumamosi Mei 25 na kila upande imejipanga kuhakikisha inaibuka na
ushindi hasa kisaikolojia
Hii ni mara ya kwanza kwa Klabu
za Germany kukutana Fainali ya UCL, hii itakuwa mara ya 4 kwa Klabu za
Nchi moja kukutana Fainali hizi.
Mwaka 2000, Klabu za Spain, Real Madrid
na Valencia, zilivaana, Mwaka 2003 AC Milan na Juventus za Italy
zilipigana na 2008 ni Man United v Chelsea za England.
Kwa Bayern Munich hii ni Fainali yao ya
10 ya Klabu Bingwa Ulaya wakiwa nyuma ya Real Madrid, waliofika Fainali
12, na AC Milan, Fainali 11,
Hii itakuwa Fainali ya 3 kwa Bayern ndani ya Misimu minne iliyopita lakini mara ya mwisho kutwaa Kombe la UCL ni Mwaka 2001.
Kwa Borussia Dortmund, hii ni Fainali ya Pili kwao ambapo walishinda ile ya kwanza ya Mwaka 1997.
Baada ya kutwaa Ubingwa wa Ulaya Mwaka
1997, Msimu uliofuata, 1997/98, Borussia Dortmund na Bayern Munich
zilikutana Robo Fainali ya UCL na Borussia kusonga kwa Jumla ya Bao 1-0.
KLABU ZA NCHI MOJA KUUMANA FAINALI ULAYA
KLABU ZA NCHI MOJA KUUMANA FAINALI ULAYA
1999/2000 Real Madrid 3-0 Valencia CF
2002/03 AC Milan 0-0 Juventus (AC Milan washinda kwa Penati 3-2)
2007/08 Manchester United 1-1 Chelsea FC (Man United washinda kwa Penati 6-5)
UEFA CUP
1979/80 VfL Borussia Mönchengladbach 3-2 Eintracht Frankfurt
WAPI WAMETOKA MPAKA KUFIKA FAINALI:
FAHAMU: -N: Nyumbani -U: Ugenini
| BORUSSIA DORTMUND | BAYERN MUNICH |
| KUNDI D: | KUNDI F: |
| MSHINDI | MSHINDI |
| -Ajax: 1-0 [N] 4-1 [U] | -Valencia: 2-1 [N] 1-1 [U] |
| -Man City: 1-1 [U]] 1-0 [N] | -BATE Borislov:1-3 [U] 4-1 [N] |
| -Real Madrid: 2-1 [N] 2-2 [U] | Lille: 1-0 [U] 6-1 [N] |
| RAUNDI ZA MTOANO: | RAUNDI ZA MTOANO: |
| -Donetsk: 2-2 [U] 3-0 [N] | -Arsenal: 3-1 [U] 0-2 [N] |
| -Malaga: 0-0 [U] 3-2 [N] | -Juventus: 2-0 [N] 2-0 [U] |
| -Real Madrid: 4-1 [N] 2-0 [U] | -Barcelona: 4-0 [N] 3-0 [U] |
DONDOO MUHIMU:
REFA:
-Nicola Rizzoli [Italy]
akisaidiwa na wenzake toka Italy Renato Faverani na Andrea Stefani na
Refa wa Akiba, Damir Skomina, wa Slovenia.
BALOZI MAALUM:
-Steve McManaman, Mshindi mara mbili wa UCL, ni Mchezaji wa zamani wa Kimataifa wa England
SHERIA ZA FAINALI:
-Baada Dakika 90 kama Sare, zitachezwa Dakika za Nyongeza 30 na kama bado Sare ni Mikwaju ya Penati kuamua Bingwa.
-Kila Timu itakuwa na Wachezaji wa Akiba 7
-Kila Timu inaruhusiwa kubadili Wachezaji Watatu tu.
UWANJA: Wembley Stadium
-Ndio Uwanja wa Nyumbani wa Timu ya Taifa ya England.
-Ingawa ndio ilichezwa
Fainali ya UCL Mwaka 2011, UEFA imeuteua tena kwa kuadhimisha Miaka 150
ya uhai wa FA, Chama cha Soka England.
-Ni mara ya 7 kwa Wembley
kutumika kwa Fainali za Klabu Bingwa Ulaya nyingine zikiwa za Miaka ya
1963, 1968, 1971, 1978, 1992 na 2011.
-Katika Fainali za Miaka ya
1968 na 1978, Klabu za England zilitwaa Ubingwa kwa Mwaka 1968
Manchester United kuichapa Benfica Bao 4-1 na Liverpool kuifunga Club
Brugge 1-0 Mwaka 1978.
MATOKEO MICHIZO ZA HIVI KARIBUNI
[BUNDESLIGA PAMOJA NA DFB POKAL]
04/05/13 Borussia Dortmund v Bayern Munich 1 : 1
27/02/13 Bayern Munich v Borussia Dortmund 1 : 0
01/12/12 Bayern Munich v Borussia Dortmund 1 : 1
12/08/12 Bayern Munich v Borussia Dortmund 2 : 1
12/05/12 Borussia Dortmund v Bayern Munich 5 : 2
11/04/12 Borussia Dortmund v Bayern Munich 1 : 0
19/11/11 Bayern Munich v Borussia Dortmund 0 : 1
26/02/11 Bayern Munich v Borussia Dortmund 1 : 3
03/10/10 Borussia Dortmund v Bayern Munich 2 : 0
13/02/10 Bayern Munich v Borussia Dortmund 3 : 1
12/09/09 Borussia Dortmund v Bayern Munich 1 : 5
08/02/09 Bayern Munich v Borussia Dortmund 3 : 1
23/08/08 Borussia Dortmund v Bayern Munich 1 : 1
23/07/08 Borussia Dortmund v Bayern Munich 2 : 1
19/04/08 Borussia Dortmund v Bayern Munich 1 : 2
13/04/08 Bayern Munich v Borussia Dortmund 5 : 0
28/10/07 Borussia Dortmund v Bayern Munich 0 : 0
26/01/07 Borussia Dortmund v Bayern Munich 3 : 2
11/08/06 Bayern Munich v Borussia Dortmund 2 : 0
13/05/06 Bayern Munich v Borussia Dortmund 3 : 3
17/12/05 Borussia Dortmund v Bayern Munich 1 : 2
19/02/0 Bayern Munich v Borussia Dortmund 5 : 0
18/09/04 Borussia Dortmund v Bayern Munich 2 : 2
17/04/04 Borussia Dortmund v Bayern Munich 2 : 0
09/11/03 Bayern Munich v Borussia Dortmund 4 : 1
19/04/03 Borussia Dortmund v Bayern Munich 1 : 0
Ukitazama kuelekea mchezo wa kesho Bayen munich inanafasi kubwa kutwaa kombe hili lakini ukitazama zaidi timu hizi zinaupinzani wa hali ya juu hivyo timu ambayo itakuwa imejipanga na kufanya maandalizi mazuri basi inanafasi ya kutwaa ubingwa msimu wa UCL UEFA CHAMPION LIGI MSIMU WA 2012-2013
*FAHAMU NI BINGWA BAYERN MUNICH BUNDASLIGA
NA
|
TIMU
|
P
|
W
|
D
|
L
|
F
|
A
|
GD
|
PTS
|
1
|
Bayern Munich
|
34
|
28
|
4
|
1
|
94
|
18
|
82
|
92
|
2
|
BV Borussia Dortmund
|
34
|
19
|
9
|
5
|
80
|
42
|
41
|
66
|
MABINGWA WALIOPITA WA UCL
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
WENYEVITI WA FA NDIYO WASIMAMIZI RCL WIKIENDI HII
WAKATI Mechi za kwanza za raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa
(RCL) zinachezwa wikiendi hii, Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imesisitiza kuwa wasimamizi wa mechi za
ligi hiyo ni wenyeviti wa mikoa wa vyama vya mpira wa miguu.
Kamati
hiyo chini ya uenyekiti wa Ramadhan Nassib ilikutana jana (Mei 23 mwaka
huu) kupitia ripoti za makamishna kwa mechi za raundi ya kwanza ya RCL
iliyomalizika wikiendi ya Mei 18 na 19 mwaka huu.
Kuhusu
viwanja vinavyotumika kwa ligi hiyo, Kamati imesema vitaendelea kuwa
vile vya makao makuu ya mikoa, na kwa vile vilivyokuwa vimeombwa
vifanyiwe marekebisho ili viweze kukaguliwa kwa ajili ya RCL msimu ujao.
Pia imeitaka mikoa kuendelea kuboresha viwanja vinavyotumika sasa,
lakini vina upungufu.
Vilevile
Kamati imebaini kuwa zimekuwepo pingamizi kuhusu usajili wa wachezaji
ambapo imesema haiwezi kujadili pingamizi hizo kwa vile mikoa yote
haikuwasilisha usajili wa wachezaji wa klabu husika uliofanyika mikoani
kama ilivyoagizwa na kuelekezwa na TFF.
Hata hivyo, Kamati imeitaka mikoa ambayo klabu zao zimefanikiwa kuingia raundi ya pili kuwasilisha usajili huo haraka.
Pia
Kamati imebaini kuwa zipo baadhi ya klabu ambazo zimekata rufani kuhusu
usajili wa baadhi ya wachezaji, na kusisitiza kilichowasilishwa ni
pingamizi kwa vile kwa mujibu wa kanuni masuala ya uwanjani hayakatiwi
rufani. Hivyo, Kamati imeshauri klabu zilizokata rufani zilirejeshewe
ada zilizolipa kwa ajili hiyo.
Makamishna
na waamuzi wanaosimamia mechi za RCL wamekumbushwa kuwa ili mchezaji
aruhusiwe kucheza mechi ni lazima awe na leseni yake (kadi ya usajili),
vinginevyo asiruhusiwe kucheza mechi husika.
Mechi
za RCL zinaendelea wikiendi hii ambapo zote zitachezwa Jumapili (Mei 26
mwaka huu) isipokuwa mechi kati ya Friends Rangers ya Dar es Salaam na
African Sports ya Tanga itakayochezwa Jumamosi (Mei 25 mwaka huu) kwenye
Uwanja wa Azam ulioko Chamazi.
Nayo
mechi kati ya Abajalo ya Dar es Salaam na Kariakoo ya Lindi iliyokuwa
ichezwe Jumamosi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam
sasa itachezwa Jumapili kwa vile siku hiyo uwanja huo utatumika kwa
mazoezi ya Taifa Stars.
Mechi
nyingine za RCL zitakazochezwa Mei 26 mwaka huu ni Machava FC ya
Kilimanjaro dhidi ya Mpwapwa Stars ya Dodoma kwenye Uwanja wa Ushirika
mjini Moshi, Stand United FC ya Shinyanga itakuwa mgeni wa Magic
Pressure ya Singida kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.
Polisi
Jamii ya Bunda mkoani Mara na Biharamulo FC ya Kagera zitaumana kwenye
Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma. Mjini Kigoma kwenye Uwanja
wa Lake Tanganyika ni kati ya wenyeji Saigon FC na Katavi Warriors ya
Katavi.
Nayo
Kimondo SC ya Mbeya itakuwa mgeni wa Njombe Mji ya Njombe katika mechi
itakayochezwa Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe. Mechi za marudiano
zitachezwa kati ya Juni 1 na 2 mwaka huu.
Timu
zitakazofuzu kucheza raundi ya tatu zitacheza mechi za kwanza kati ya
Juni 8 na 9 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakuwa kati ya Juni 15
na 16 mwaka huu.
SEMINA YA USAJILI- TMS KUFANYIKA MEI 25
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeandaa semina ya usajili kwa njia
ya mtandao (Transfer Matching System-TMS) kwa klabu za Ligi Kuu ya
Vodacom kwa ajili ya msimu wa 2013/2014.
Semina
hiyo itafanyika Jumamosi (Mei 25 mwaka huu) kwenye ofisi za TFF saa 3
kamili asubuhi ikishirikisha watu wawili kutoka kila klabu ambao ni TMS
Manager, na ofisa mwingine wa klabu.
Klabu
za ligi hiyo zinazotakiwa kuhudhuria semina ya usajili ni Ashanti
United, Azam, Coastal Union, JKT Ruvu, Kagera Sugar, Mbeya City, Mgambo
Shooting, Mtibwa Sugar, Oljoro JKT, Rhino Rangers, Ruvu Shooting, Simba,
Tanzania Prisons na Yanga.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Thursday, May 23, 2013
CITY YAKANUSHA KUWAWINDA FALCAO NA NEYMAR

MKURUGENZI MKUU wa Manchester City chief Ferran Soriano amekanusha taarifa kuwa wanahaha kuwasaini Masupastaa Radamel Falcao na Neymar.
Hivi karibuni kumezagaa ripoti kuwa Man City ni miongoni mwa Klabu zinazokimbiza saini za Straika wa Atletico Madrid, Radamel Falcao, na yule wa Santos ya Brazil, Neymar.
Falcao anawindwa na msululu wa Klabu zikiwemo Chelsea, Monaco na Real Madrid baada ya kung’ara sana kwa kuifungia Atletico Mabao muhimu kwa Misimu kadhaa.
Nae Neymar, anaewindwa na Klabu kubwa Barani Ulaya, anatarajiwa kuihama Brazil baada ya Nchi hiyo kuwa Mwenyeji wa Kombe la Dunia Mwaka 2014.
Hata hivyo, Soriano amekanusha kwa kutamka: “Neymar na Falcao? Habari hizo ni uongo, hawajawahi kuwa kwenye ajenda yetu!”
Vile vile, Soriano aliponda habari kuwa wanataka kumuuza Straika wao mahiri Serio Aguero, mwenye Miaka 24, huku Real Madrid ikitajwa kuwa ndio atatua.
Soriano amesisitiza: “Hatujawahi kufikiria kumuuza Aguero. El Kun ana furaha kubaki kwetu Mwaka huu!”
MESSI AFURAHIA KUVAA JEZI NAMBA 10 AKIWA KATIKA TIMU HIYO.
MSHAMBULIAJI nyota maarufu dunia wa
klabu ya Barcelona Lionel Messi amesema anajisikia raha na heshima kubwa kuvaa
jezi namba 10 akiwa katika klabu hiyo na kufuata nyayo za Ronaldinho na
nyota wengine waliokuwa wakivaa jezi hiyo. Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Argentina alirithi namba ya jezi ya Ronaldinho
wakati nyota huyo wa Brazil alipoondoka Barcelona kwenda AC Milan katika
kipindi cha majira ya kiangazi mwaka 2008 na kudai kuwa ilikuwa na
maana kubwa kwake wakati anaanza kuivaa. Messi
amesema wakati anapewa jezi hiyo namba 10 alijisikia furaha kwa ni jezi
ambayo imekuwa ikivaliwa na wachezaji waliofanya mambo makubwa katika
klabu hiyo. Nyota
huyo pia alielezea nia yake ya kutaka kuiongoza timu ya taifa ya nchi
yake kunyakuwa Kombe la Dunia huku akitaka mataji zaidi katika klabu
yake ya Barcelona.
Subscribe to:
Posts (Atom)



