MENEJA wa klabu ya
Borussia Dortmund, Jurgen Klopp ametanabaisha kuwa ataimarisha kikosi chake na
kufikia fainali nyingine ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kipigo
walichopata dhidi ya Bayern Munich. Dortmund
walipoteza mchezo huo ulizikutanisha timu zote kutoka Ujerumani kwa
mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Wembley baada ya bao la dakika za mwisho
lililofungw ana Arjen Robben. Lakini
kocha huyo ametamba kuwa pamoja na kushindwa katika fainali hiyo ya
Wembley lakini anaamini atafikia fainali nyingine katika kipindi kifupi
kijacho. Klopp
amesema kwasasa ana kazi kubwa ya kuimarisha kikosi chake baada ya
wachezaji kadhaa tegemeo kutaka kuondoka mwishoni mwa msimu huu lakini
anaamini mpaka kufikia msimu mpya tayari atakuwa na kikosi imara. Kiungo
tegemeo wa klabu hiyo Mario Gotze tayari imeshathibitishwa kwenda
Bayern Msimu ujao huku mshambuliaji wake nyota Robert Lewandowski naye
akijipanga kuelekea huko.