AGUERO BADO NIPO NIPO MAN CITY MPAKA 2017.
MSHAMBULIAJI nyota wa
klabu ya Manchester City, Sergio Aguero ameongeza mkataba wa mwaka mmoja
ambao utamuweka katika klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini
Uingereza mpaka mwaka 2017. Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 24 amefunga mabao
12 katika mechi 30 za ligi alizocheza msimu uliopita na kufunga bao la
ushindi dhidi ya Queens Park Rangers lililowapa taji la ligi katika
msimu wa 2011-2012. Mara
baada ya kusaini mkataba huyo Aguero aliuambia mtandao wa klabu hiyo
kwamba anajisikia furaha na kuhitajika hivyo atafanya kila awezalo ili
aendelee kufanya kazi vyema na kuipa mataji klabu hiyo. Vyombo
vya habari nchini Uingereza vilikuwa vikiripoti kuwa mchezaji huyo
anaweza kutimkia Real Madrid lakini tetesi hizo zitakwisha baada ya kuwa
mchezaji mwingine wa timu hiyo kuongeza mkataba baada ya Gael Clichy,
Yaya Toure na David Silva kufanya hivyo.