STRAIKA MAHIRI wa Atletico Madrid,
Radamel Falcao, atapimwa afya yake kwenye Klabu ya Monaco ambayo
imepanda Daraja Msimu huu kurudi Ligue 1 ya France na Uhamisho wake
unatarajiwa kugharimu Dau la Pauni Milioni 51.
Habari hizi zimevuja huko Spain na kudaiwa kuwa Atraika huyo kutoka Colombo atapimwa afya yake siku ya Jumatatu Mei 27.
Monaco, ambayo imenunuliwa na Tajiri wa
Kirusi Dmitry Rybolovlev, tayari imeshawanunua Mastaa wa FC Porto Joao
Moutinho na James Rodriguez kwa Dau la Jumla ya Pauni Milioni 60 na
kutua kwa Falcao kutawafanya watatu hao wakutane tena kwani waliwahi
kuchezea Klabu moja.
Kuhama kwa Falcao kulidokezwa na Meneja
wa Atletico Madrid Diego Simeone ambae ameshasema hatakuwa na kinyongo
ikiwa Falcao, mwenye Miaka 27, atahama.
Hivi Juzi, Kocha Msaidizi wa Monaco,
Jean Petit, alidokeza wanatarajia Falcao na Wachezaji wengine wanne au
watano wa kiwango chake kununuliwa na Klabu yao.
Mwezi Desemba 2011, Dmitry Rybolovlev
alinunua Hisa za Asilimia 60 za Klabu ya Monaco na kuanza kuibadili
wakati huo ikiogelea Daraja la chini huko France, Ligue 2, na Mwezi Mei
2012 alimteua Kocha wa zamani wa Chelsea Claudio Ranieri kuiongoza
Monaco na amefanya hilo kwa mafanikio kwa kuirudisha Monaco Daraja la
juu huko France.