MESSI AFURAHIA KUVAA JEZI NAMBA 10 AKIWA KATIKA TIMU HIYO.
MSHAMBULIAJI nyota maarufu dunia wa
klabu ya Barcelona Lionel Messi amesema anajisikia raha na heshima kubwa kuvaa
jezi namba 10 akiwa katika klabu hiyo na kufuata nyayo za Ronaldinho na
nyota wengine waliokuwa wakivaa jezi hiyo. Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Argentina alirithi namba ya jezi ya Ronaldinho
wakati nyota huyo wa Brazil alipoondoka Barcelona kwenda AC Milan katika
kipindi cha majira ya kiangazi mwaka 2008 na kudai kuwa ilikuwa na
maana kubwa kwake wakati anaanza kuivaa. Messi
amesema wakati anapewa jezi hiyo namba 10 alijisikia furaha kwa ni jezi
ambayo imekuwa ikivaliwa na wachezaji waliofanya mambo makubwa katika
klabu hiyo. Nyota
huyo pia alielezea nia yake ya kutaka kuiongoza timu ya taifa ya nchi
yake kunyakuwa Kombe la Dunia huku akitaka mataji zaidi katika klabu
yake ya Barcelona.