Kocha wa Real madrid Jose Mourinho pamoja na nyota wa
klabu hiyo Cristiano Ronaldo wamefungiwa mechi mbili za michuano ya Kombe la Mfalme baada ya kutolewa
nje katika fainali dhidi ya Atletico Madrid. Mourinho
mwenye umri wa miaka 50 alitolewa nje baada ya kumshambulia mwamuzi kwa
maamuzi aliyotoa adhabu ambayo hataweza kuitumikia baada ya kutangaza
kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu. Ronaldo
mwenye umri wa miaka 28 alipewa kadi nyekundu baada kukutwa na hatia ya
kumpiga teke la uso kwa makusudi mchezaji wa Atletico, Gabi. Wote wawili Ronaldo na Mourinho watakuwepo katika michezo miwili ya mwisho ya ligi ya Madrid.