CLUB YA SANTOS YAKATAA OFA YA PILI YA BARCA
MAKAMU wa rais wa klabu
ya Santos ya Brazil, Odilio Rodrigues amedai kwamba wamekataa ofa ya klabu
ya Barcelona ya Hispania kutaka kumsajili mshambuliaji wao nyota Neymar
kwa mara ya pili. Katika
siku za hivi karibuni Barcelona ndiyo pekee wameonyesha nia ya kumhitaji
mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil na kuripoti kuwa walitaka
kuwapa Santos euro milioni 20 ili waweze kumiliki haki za mchezaji huyo
kwa asilimia 55. Wakati
mahasimu wao nao Real madrid wakiongeza mbio ya kumfukuzia mshambuliaji huyo,
Barcelona walitoa kiasi hicho ili waweze kumaliza suala hilo lakini
Rodrigues amesisitiza kuwa hawana haraka ya kumuuza Neymar kwa kiasi
kidogo kuliko wanachotaka. Rodrigues
alithibitisha kuwa ni kweli walipata ofa ya Barcelona kwa mara ya pili
lakini waliikataa kwasababu hawakufikia kiwango walichokuwa
wakikihitaji. Neymar
katika siku karibu ameweka wazi nia yake ya kubakia Santos mpaka baada
ya michuano ya Kombe la Dunia 2014, ingawa uhamisho wa kwenda barani
Ulaya katika kipindi hiki cha usajili unaonekana kama unaweza kuwepo.