WINGA maarufu wa klabu ya Bayern Munich, Franck Ribery ametanabaisha kuwa alichukua Kombe la Ligi ya Mabingwa na kwenda nalo kitandani kufuatia ushindi wa timu yao wa mabao 2-1 dhidi ya Borussia Dortmund. Bayern wamefanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo mara tatu katika kipindi cha miaka minne lakini walifanikiwa kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza toka mwaka 2001 kwa ushindi waliopata katika Uwanja wa Wembley Jumamosi. Na Ribery alibainisha hilo katika sherehe za kulitembeza kombe hilo mtaani huko Ujerumani kwamba alichukua kombe hilo na kwenda nalo nyumbani. Nyota huyo raia wa Ufaransa amesema alikuwa macho mpaka alfajiri na baadae kwenda kulala akiwa na mke wake pamoja na kombe hilo. Bayern sasa wana nafasi ya kushinda matatu matatu kwa mkupuo kama wakifanikiwa kushinda taji la DFB Pokal Juni mosi mwaka huu.
Monday, May 27, 2013
BENITEZ ATAKA KUIFUNDISHA TIMU INAYOSHIRIKI LIGI YA MABINGWA ULAYA.
MENEJA wa muda wa
klabu ya Chelsea Rafael Benitez ametanabaisha kuwa anataka kufundisha timu
inayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kumaliza
kazi yake katika klabu hiyo.
Katika kipindi
kifupi kijacho Benitez ataondoka Stamford Bridge akiwa ameisimamia klabu hiyo
kwa mara ya mwisho Jumamosi iliyopita wakati walipocheza na Manchester City
katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jijini New York Marekani.
Kocha huyo raia wa
Hispania ameiongoza Chelsea kushinda taji la Europa League pamoja na kuisadia
kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kuajiriwa kwa
muda mfupi kuziba nafasi ya Roberto Di Matteo Novemba mwaka jana.
Banitez anaondoka
Chelsea kumpisha Jose Mourinho na kocha huyo sasa anaweza kuangalia mstakabali
wake wa kuhusishwa na tetesi za kwenda Napoli na Paris Saint-Germain ambapo
klabu zote hizo zinakidhi matakwa yake ya kushiriki Ligi ya Mabingwa.
RADAMEL FALCAO HATIMAYE ATUA KATIKA CLUB YA MONACO
STRAIKA MAHIRI wa Atletico Madrid,
Radamel Falcao, atapimwa afya yake kwenye Klabu ya Monaco ambayo
imepanda Daraja Msimu huu kurudi Ligue 1 ya France na Uhamisho wake
unatarajiwa kugharimu Dau la Pauni Milioni 51.
Habari hizi zimevuja huko Spain na kudaiwa kuwa Atraika huyo kutoka Colombo atapimwa afya yake siku ya Jumatatu Mei 27.
Monaco, ambayo imenunuliwa na Tajiri wa
Kirusi Dmitry Rybolovlev, tayari imeshawanunua Mastaa wa FC Porto Joao
Moutinho na James Rodriguez kwa Dau la Jumla ya Pauni Milioni 60 na
kutua kwa Falcao kutawafanya watatu hao wakutane tena kwani waliwahi
kuchezea Klabu moja.
Kuhama kwa Falcao kulidokezwa na Meneja
wa Atletico Madrid Diego Simeone ambae ameshasema hatakuwa na kinyongo
ikiwa Falcao, mwenye Miaka 27, atahama.
Hivi Juzi, Kocha Msaidizi wa Monaco,
Jean Petit, alidokeza wanatarajia Falcao na Wachezaji wengine wanne au
watano wa kiwango chake kununuliwa na Klabu yao.
Mwezi Desemba 2011, Dmitry Rybolovlev
alinunua Hisa za Asilimia 60 za Klabu ya Monaco na kuanza kuibadili
wakati huo ikiogelea Daraja la chini huko France, Ligue 2, na Mwezi Mei
2012 alimteua Kocha wa zamani wa Chelsea Claudio Ranieri kuiongoza
Monaco na amefanya hilo kwa mafanikio kwa kuirudisha Monaco Daraja la
juu huko France.
NEYMAR HATIMAYE SASA ATUA FC BARCELONA
CLUB ya soka FC Barcelona imefikia Makubaliano na Klabu
ya Brazil, Santos, ya kumsaini Neymar ambapo leo Jumatatu Mei 27 atasaini
Mkataba ili kukamilisha Dili hiyo ya Uhamisho.
Klabu ya Barcelona imetoa Taarifa rasmi ya kuthibitisha kufikia makubaliano ya kumsaini Nyota huyo wa Brazil mwenye Miaka 21.
WASIFU:
Neymar da Silva Santos Junior
KUZALIWA: 5 Februari 1992, Nchini Brazil
Santos: Mechi 229 Magoli 138
Brazil: Mechi 32 Magoli 20
Na
Mwenyewe Neymar alitoa Ujumbe kwenye Mtandao wa Instagram uliosema kuwa jumatatu nasaini Mkataba na Barcelona. Nataka kuwashukuru Mashabiki wa
Santos kwa Miaka hii 9 ya ajabu.
Juzi Klabu ya Santos ilitoa Taarifa kuwa
imepokea Ofa mbili za kumnunua Neymar na ilisadikiwa zimetoka toka
mbili kati ya Klabu za Barcelona, Real Madrid au Chelsea.
Mkataba wake na Santos ulitarajiwa kumalizika mwishoni mwa Msimu ujao, Mwezi Juni 2014.

Neymar ndie ameiongoza Santos kupata
mafanikio makubwa tangu Nguli Pele aache kuichezea Klabu hiyo kwenye
Miaka ya 1970 kwa kuisaidia kutwaa Kombe la Brazil Mwaka 2010, Copa
Libertadores Mwaka 2011 na Ubingwa wa Jimbo la Sao Paolo kwa mara 3
mfululizo.
Nayo Klabu ya Santos imesema kuwa ilijaribu kila njia ili Neymar abaki kwao lakini Ofa za nje zimewafanya wasiweze kushindana.
Hata hivyo, Santos imekataa kutaja Dili hiyo ya Uhamisho imegharimu kiasi gani kwa vile kila upande umekubaliana kuwa iwe siri.
WASIFU WA NEYMAR | |||
Taarifa kuhusu yeye | |||
---|---|---|---|
Full name | Neymar da Silva Santos Júnior | ||
Date of birth | 5 February 1992 (age 21) | ||
Place of birth | Mogi das Cruzes, Brazi | ||
Height | 1.74 m (5 ft 9 in) | ||
Playing position | Mshambuliaji | ||
Club ya sasa | |||
Current club | Santos | ||
Number | 11 | ||
Timu za ujana | |||
1999–2003 | Portuguesa Santista | ||
2003–2009 | Santos | ||
Timu ya ukubwa | |||
Years | Team | Mechi | Goli |
2009– | Santos | 103 | (54) |
Timu ya Taifa | |||
2009 | Brazil U17 | 3 | (1) |
2011 | Brazil U20 | 7 | (9) |
2012 | Brazil U23 | 7 | (4) |
2010– | Brazil | 32 | (20) |
AGUERO BADO NIPO NIPO MAN CITY MPAKA 2017.
MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Manchester City, Sergio Aguero ameongeza mkataba wa mwaka mmoja ambao utamuweka katika klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uingereza mpaka mwaka 2017. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 24 amefunga mabao 12 katika mechi 30 za ligi alizocheza msimu uliopita na kufunga bao la ushindi dhidi ya Queens Park Rangers lililowapa taji la ligi katika msimu wa 2011-2012. Mara baada ya kusaini mkataba huyo Aguero aliuambia mtandao wa klabu hiyo kwamba anajisikia furaha na kuhitajika hivyo atafanya kila awezalo ili aendelee kufanya kazi vyema na kuipa mataji klabu hiyo. Vyombo vya habari nchini Uingereza vilikuwa vikiripoti kuwa mchezaji huyo anaweza kutimkia Real Madrid lakini tetesi hizo zitakwisha baada ya kuwa mchezaji mwingine wa timu hiyo kuongeza mkataba baada ya Gael Clichy, Yaya Toure na David Silva kufanya hivyo.
KLOPP ASEMA TUTAIMARISHA KIKOSI FAINALI ZIJAZO
MENEJA wa klabu ya
Borussia Dortmund, Jurgen Klopp ametanabaisha kuwa ataimarisha kikosi chake na
kufikia fainali nyingine ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kipigo
walichopata dhidi ya Bayern Munich. Dortmund
walipoteza mchezo huo ulizikutanisha timu zote kutoka Ujerumani kwa
mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Wembley baada ya bao la dakika za mwisho
lililofungw ana Arjen Robben. Lakini
kocha huyo ametamba kuwa pamoja na kushindwa katika fainali hiyo ya
Wembley lakini anaamini atafikia fainali nyingine katika kipindi kifupi
kijacho. Klopp
amesema kwasasa ana kazi kubwa ya kuimarisha kikosi chake baada ya
wachezaji kadhaa tegemeo kutaka kuondoka mwishoni mwa msimu huu lakini
anaamini mpaka kufikia msimu mpya tayari atakuwa na kikosi imara. Kiungo
tegemeo wa klabu hiyo Mario Gotze tayari imeshathibitishwa kwenda
Bayern Msimu ujao huku mshambuliaji wake nyota Robert Lewandowski naye
akijipanga kuelekea huko.
TAIFA STARS YAELEKEA ADDIS ABABA LEO.
TIMU ya Taifa ya
Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kuondoka leo (Mei 26 mwaka huu) usiku
kwenda Addis Ababa, Ethiopia ambapo itaweka kambi na kucheza mechi moja
ya kirafiki kabla ya kwenda Morocco. Stars
inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka saa 5 usiku kwa
ndege ya EgyptAir ikiwa na kikosi cha wachezaji 21 chini ya nahodha wake
kipa Juma Kaseja. Timu
hiyo ikiwa Ethiopia, Juni 2 mwaka huu itacheza mechi ya kirafiki dhidi
ya Sudan ambapo siku inayofuata itaondoka kwenda Marrakech, Morocco kwa
kupitia Cairo, Misri. Mechi hiyo ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya
wenyeji Morocco itachezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech.
Mbali
ya nahodha Kaseja, wachezaji wengine wanaoondoka katika kikosi hicho
ambacho kina wiki sasa tangu kingie kambini jijini Dar es Salaam ni
Mwadini Ally na Ally Mustafa ambao wote ni makipa. Wengine
ni Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Aggrey Morris, Haroub Nadir, Mwinyi
Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum
Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya,
Athuman Idd na Haruni Chanongo. Wachezaji
Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu ambao wako na timu yao ya TP Mazembe
ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo watajiunga moja kwa moja na Stars
jijini Marrakech, Juni 4 mwaka huu wakitokea Maputo, Msumbiji mara baada
ya mechi yao ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Liga Muculumana ya huko. Katika
msafara huo wa Ethiopia benchi la ufundi la Stars linaundwa na Kim
Poulsen (Kocha Mkuu), Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi),Juma Pondamali
(Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja wa timu), Dk. Mwanandi
Mwankemwa (Daktari), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred
Chimela (Mtunza vifaa).
Subscribe to:
Posts (Atom)