Tuesday, May 28, 2013

MFAHAMU KWA UZURI TORREZ ELININYOOO MKALI WA MABAOOO

Fernando Torres
TorresFinale12 cropped.jpg
Taarifa kuhusu yeye
Jina kamiliFernando José Torres Sanz
Kuzaliwa20 March 1984 (age 29)
NchiFuenlabrada, Spain
Urefu1.83 m (6 ft 0 in)
Nafasi Mshambuliaji
Timu ya sasa
Current clubChelsea
Number9
Timu ya ujana
1995–2001Atlético Madrid
Timu za ukubwa
YearsTeamMechiGoli
2001–2007Atlético Madrid214(82)
2007–2011Liverpool102(65)
2011–Chelsea82(15)
Timu ya taifa
2000Spain U151(0)
2001Spain U169(11)
2001Spain U174(1)
2002Spain U181(1)
2002Spain U195(6)
2002–2003Spain U2110(3)
2003–Spain101(31)
KLABU ALIZOCHEZA NA KUPATA MATAJI
Atletico Madrid
Segunda Division: 2001-02 
Chelsea
Kombe la FA: 2011-12 
Ligi ya Mabingwa: 2011-12 
UEFA Europa Ligi: 2012-13 
Timu ya Taifa
Hispania U-16
Kombe la Ulaya la Chini- michuano miaka 16 : 2001
Hispania U-19
Kombe la Ulaya la Chini ya miaka 19 Kandanda michuano: 2002
Timu kubwa Hispania
Soka Ulaya UEFA michuano ya (2): 2008, 2012
Kombe la Dunia: 2010 
TUZO BINAFSI
1.Mfungaji bora Kombe la nike : 1999
2.Algarve cup Mchezaji wa Mashindano: 2001
3.Algarve mashindano mfungaji bora: 2001
4.Kombe la Ulaya la Chini-16 Mchezaji wa bora wa Mashindano: 2001
5.Kombe la Ulaya la Chini-16  mfungaji bora: 2001
6.Kombe la Ulaya la Chini ya 19 Mchezaji bora wa Mashindano: 2002 
7.Kombe la Ulaya la Chini ya 19 mfungaji bora wa michuano Soka: 2002.
8.Ligi Kuu ya PFA Timu ya Mwaka (2): 2007-08, 2008-09
9.Ligi Kuu ya Mchezaji wa Mwezi (2): Februari 2008, Septemba 2009.
10.Ligi Kuu mfungaji bora wa Mwezi (2): Aprili 2009,  Machi 2010.
11.UEFA Euro Timu ya mashindano: 2008
12.UEFA Timu ya Mwaka: 2008
13.FIFPro World XI mchezaji bora  (2): 2008, 2009
14.FIFA World Mchezaji bora  wa Mwaka : 2008
15.Ballon d'Or Nafasi ya tatu: 2008
16.Kombe la Shirikisho la Silver Boot: 2009
17.FIFA Confederations Cup Timu ya mashindano: 2009 
18.UEFA Euro Golden Boot: 2012 
TUZO ZA KIENYEJI"
1.Mkuu wa Asturias tuzo kwa ajili ya Michezo: 2010
2.Medali ya dhahabu ya Mpango Royal ya Michezo kiutamaduni: 2011. 

RAFAEL BENITEZ ATEULIWA KUWA KOCHA MPYA NAPOLI

Klabu ya Italy Napoli imemteuwa Rafael Benitez, Miaka 53 kuwa Meneja mpya wa klubu hiyo ambayo katika Msimu huu imeshika Nafasi ya Pili nyuma ya Mabingwa Juventus.
Msimu ujao wa 2013/14, Napoli itacheza UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
katika suala nzima la benitez kutua hapo ni kutokana na aliyekuwa Meneja wa club hiyo Walter Mazzarri, alitangazwa kuiacha Napoli na kuhamia Inter Milan.
Uteuzi huo wa Benitez ulithibitishwa na Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis ambae alimsifia Benitez na kumwita Kocha mwenye ujuzi wa Kimataifa.
aidha Benitez ndio kwanza amemaliza Kibarua cha kuwa Meneja wa muda Klabuni Chelsea na, Wiki mbili zilizopita, hapo Mei 15, aliiwezesha Chelsea kutwaa Kombe la EUROPA LIGI baada ya kuichapa Benfica Bao 2-1 kwenye Fainali.
hata hivyo Benitez aliteuliwa Meneja wa muda wa Chelsea Novemba Mwaka jana baada ya kufukuzwa Roberto Di Matteo.

LEWANDOWSKI ANANAFASI KUBWA KWENDA MUNICH-WAKALA

WAKALA wa mshambuliaji nyota wa klabu ya Borussia Dortmund, Robert Lewandowski amesema kuna uwezekano mkubwa wa mshambuliaji huyo kujiunga na mabingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya Bayern Munich. Hata hivyo, wakala huyoaitwaye Cezary Kucharski aliiambia luninga moja nchini Ujerumani kwamba Bayern bado hawajafikia makubaliano ya mambo binafsi ya nyota huyo wa kimataifa wa Poland. Wakala huyo aliendelea kusema kuwa wao wako tayari lakini badi hawajasaini chochote kwasababu klabu nayo inatakiwa iafiki makubaliano hayo. Bayern ambao ni mabingwa wapya wa Ujerumani tayari wamemnyakuwa kiungo wa Dortmund Mario Gotze mwenye umri wa miaka 20 kwa ada ya euro milioni 37.

TORRES VS CASILLAS WAITWA TIMU YA TAIFA

KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque amemuita golikipa Iker Casillas na mshambuliaji Fernando Torres katika kikosi cha wachezaji 26 ambacho kitaanza maandalizi ya Kombe la Shirikisho linalotarajiwa kuanza mwezi ujao nchini Brazil. Orodha hiyo ya wachezaji 26 itapunguzwa na kufikia 23 baada ya mzunguko wa mwisho wa mechi za Ligi Kuu nchini Hispania mwishoni mwa wiki ijayo. Hispania ambao ni mabingwa wa Dunia na Ulaya wana mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya Haiti Juni 8 na Ireland siku tatu baadae kabla ya kuelekea nchini Brazil. Katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Hispania imepangwa katika kundi B sambamba na Uruguay, Tahiti na Nigeria ambapo mchezo wa ufunguzi utachezwa Juni 16 dhidi ya Uruguay. 
Michuano hiyo ambayo inashirikisha timu nane inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 15 mpaka 30. 
Goalkeepers: Iker Casillas (Real Madrid), Victor Valdes (Barcelona), Pepe Reina (Liverpool)

Defenders: Alvaro Arbeloa (Real Madrid), Sergio Ramos (Real Madrid), Gerard Pique (Barcelona), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Jordi Alba (Barcelona), Ignacio Monreal (Arsenal), Raul Albiol (Real Madrid), Javi Garcia (Manchester City)

Midfielders: Javi Martinez (Bayern Munich), Xavi (Barcelona), Andres Iniesta (Barcelona), Sergio Busquets (Barcelona), Santi Cazorla (Arsenal), Xabi Alonso (Real Madrid), Benat Etxebarria (Real Betis)
Forwards: Cesc Fabregas (Barcelona), David Villa (Barcelona), David Silva (Manchester City), Roberto Soldado (Valencia), Pedro (Barcelona), Juan Mata (Chelsea), Jesus Navas (Sevilla), Fernando Torres (Chelsea).

Monday, May 27, 2013

FRANK RIBERY ATANABAISHA KULALA NA KOMBE LA UEFA LIGI.

WINGA maarufu wa klabu ya Bayern Munich, Franck Ribery ametanabaisha kuwa alichukua Kombe la Ligi ya Mabingwa na kwenda nalo kitandani kufuatia ushindi wa timu yao wa mabao 2-1 dhidi ya Borussia Dortmund. Bayern wamefanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo mara tatu katika kipindi cha  miaka minne lakini walifanikiwa kushinda taji hilo kwa mara ya kwanza toka mwaka 2001 kwa ushindi waliopata katika Uwanja wa Wembley Jumamosi. Na Ribery alibainisha hilo katika sherehe za kulitembeza kombe hilo mtaani huko Ujerumani kwamba alichukua kombe hilo na kwenda nalo nyumbani. Nyota huyo raia wa Ufaransa amesema alikuwa macho mpaka alfajiri na baadae kwenda kulala akiwa na mke wake pamoja na kombe hilo. Bayern sasa wana nafasi ya kushinda matatu matatu kwa mkupuo kama wakifanikiwa kushinda taji la DFB Pokal Juni mosi mwaka huu.

BENITEZ ATAKA KUIFUNDISHA TIMU INAYOSHIRIKI LIGI YA MABINGWA ULAYA.

MENEJA wa muda wa klabu ya Chelsea Rafael Benitez ametanabaisha kuwa anataka kufundisha timu inayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kumaliza kazi yake katika klabu hiyo.
Katika kipindi kifupi kijacho Benitez ataondoka Stamford Bridge akiwa ameisimamia klabu hiyo kwa mara ya mwisho Jumamosi iliyopita wakati walipocheza na Manchester City katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jijini New York Marekani.
Kocha huyo raia wa Hispania ameiongoza Chelsea kushinda taji la Europa League pamoja na kuisadia kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao baada ya kuajiriwa kwa muda mfupi kuziba nafasi ya Roberto Di Matteo Novemba mwaka jana. 
Banitez anaondoka Chelsea kumpisha Jose Mourinho na kocha huyo sasa anaweza kuangalia mstakabali wake wa kuhusishwa na tetesi za kwenda Napoli na Paris Saint-Germain ambapo klabu zote hizo zinakidhi matakwa yake ya kushiriki Ligi ya Mabingwa.

RADAMEL FALCAO HATIMAYE ATUA KATIKA CLUB YA MONACO

STRAIKA MAHIRI wa Atletico Madrid, Radamel Falcao, atapimwa afya yake kwenye Klabu ya Monaco ambayo imepanda Daraja Msimu huu kurudi Ligue 1 ya France na Uhamisho wake unatarajiwa kugharimu Dau la Pauni Milioni 51.
Habari hizi zimevuja huko Spain na kudaiwa kuwa Atraika huyo kutoka Colombo atapimwa afya yake siku ya Jumatatu Mei 27.
Monaco, ambayo imenunuliwa na Tajiri wa Kirusi Dmitry Rybolovlev, tayari imeshawanunua Mastaa wa FC Porto Joao Moutinho na James Rodriguez kwa Dau la Jumla ya Pauni Milioni 60 na kutua kwa Falcao kutawafanya watatu hao wakutane tena kwani waliwahi kuchezea Klabu moja.
Kuhama kwa Falcao kulidokezwa na Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone ambae ameshasema hatakuwa na kinyongo ikiwa Falcao, mwenye Miaka 27, atahama.
Hivi Juzi, Kocha Msaidizi wa Monaco, Jean Petit, alidokeza wanatarajia Falcao na Wachezaji wengine wanne au watano wa kiwango chake kununuliwa na Klabu yao.
Mwezi Desemba 2011, Dmitry Rybolovlev alinunua Hisa za Asilimia 60 za Klabu ya Monaco na kuanza kuibadili wakati huo ikiogelea Daraja la chini huko France, Ligue 2, na Mwezi Mei 2012 alimteua Kocha wa zamani wa Chelsea Claudio Ranieri kuiongoza Monaco na amefanya hilo kwa mafanikio kwa kuirudisha Monaco Daraja la juu huko France.