Tuesday, June 4, 2013

MAN CITY YAMNASA WINGA WA SEVILLA JESUS NAVAS.

Club ya soka ya Manchester City wamefikia makubaliano na Klabu ya Spain Sevilla ya kumnunua Winga wa Kimataifa wa Spain Jesus Navas.
Navas, mwenye Miaka 27, anategemewa kununuliwa kwa gharama ya Pauni Milioni 17.
Navas yumo kwenye Kikosi cha Spain kitakachocheza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara huko Brazil kuanzia Juni 15.
Hadi sasa Man City haijatangaza nani Meneja wao mpya baada ya kumtimua Roberto Mancini ingawa wengi wanategemea Manuel Pellegrini, aliekuwa Malaga, ndio atachukua nafasi hiyo.

NEYMAR ASEMA MESS ATAENDELEA KUTISHA ZAIDI DUNIANI.

MSHAMBULIAJI nyota mpya wa klabu ya Barcelona, Neymar ametanabaisha anataka kumsadia nyota wa klabu hiyo Lionel Messi aendelee kung’ara duniani baada ya kukamilisha taratibu zote za uhamisho wake kutoka klabu ya Santos. Neymar mwenye umri wa miaka alikamilisha uhamisho wake wenye thamani ya euro million 57 na kumaliza utata wa miezi kadhaa juu ya mstakabali wa nyota huyo. Akihojiwa mara baada ya kutambulishwa rasmi mbele ya maelfu ya mashabiki katika uwanja wa Camp Nou, Neymar amesema anataka kuisaidia timu kwasababu Barcelona ni zaidi ya klabu na pia anataka kumsadia Messi aendelee kung’ara zaidi. Nyota huyo aliendelea kusema kuwa ilikuwa ni ndoto zake kucheza katika klabu ambayo inahesabika kama mojawapo ya klabu bora duniani huku akizungukwa na wachezaji nyota. Neymar anaondoka Santos akiwa ameshinda Kombe la Brazil mwaka 2010, Kombe la Klabu Bingwa ya Amerika Kusini mwaka 2011 huku akiwa amefunga mabao 138 katika mechi 229 alizocheza akiwa katika klabu hiyo.

TAIFA STAR YATUA MORROCO RASMI KWA MAANDALIZI YA MECHI ITAKAYO PIGWA JUNE 8.

Taifa Stars imewasili hapa Marrakech, Morocco leo- Juni 3 mwaka huu tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Morocco itakayochezwa Jumamosi- Juni 8 mwaka huu.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia hoteli ya Pullman ambayo pia Ivory Coast ilifikia ilipokuja kucheza hapa dhidi ya Morocco. Stars imetua na wachezaji 21 huku Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu waliokuwa Maputo, Msumbiji kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho na timu yao ya TP Mazembe watawasili kesho- Juni 4 mwaka huu saa 8 mchana.
Mechi kati ya Stars na Morocco itachezwa kuanzia saa 3 usiku kwa saa za hapa wakati nyumbani itakuwa ni saa 5 usiku.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Marrakech, Morocco

Monday, June 3, 2013

ALVES AMFAGILIA MSHAMBULIAJI MPYA WA TIMU HIYO NEYMAR

BEKI wa kimataifa wa Brazil na klabu ya Barcelona, Dani Alves amedai kuwa mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Neymar atang’ara na hatahitaji muda mrefu wa kuzoea mazingira mapya msimu ujao. Neymar mwenye umri wa miaka 21 anatarajia kuondoka klabu ya Santos kwenda Barcelona baada ya kukubalia kusaini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo ambapo Alves anaamini nyota huyo atapata mafanikio akiwa Camp Nou. Alves amesema nyota huyo ana kipaji cha hali ya juu ndio maana Barcelona wakaamua kumsajili kutoka Santos na ni mategemeo yao atazoea mazingira ya Barcelona haraka kwasababu atakuwa akifanya kitu anachokipenda nacho ni kucheza soka. Neymar anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya na Barcelona leo kabla ya kumalizia taratibu za uhamisho wake.

CHELSEA YAMTAMBULISHA RASMI MTU SPESHO"MOURINHO"

KLABU ya soka ya Chelsea imemteua rasmi Jose Mourinho kuwa meneja wa klabu hiyo kwa mkataba wa miaka minne. Mourinho ambaye ni raia wa Ureno atachukua nafasi ya Rafael banitez aliyejiunga na Napoli baada ya kuinoa klabu hiyo kwa miezi sita. Hii ni mara ya pili kwa Mourinho kurejea Stamford Brigde kama kocha kocha baada ya kuondoka miaka sita iliyopita. Mourinho ndiye alikuwa chaguo la kwanza la mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich baada ya kuinunua klabu hiyo mwaka 2003 na ndiye kocha pekee kati ya tisa waliopita klabuni hapo kuanzia kipindi hicho aliyeipa mafanikio zaidi.
MAMENEJA WA CHELSEA CHINI YA ROMAN ABRAMOVICH:
-Claudio Ranieri: Sep 2000 mpaka Mei 2004
-Jose Mourinho: Jun 2004 mpaka Sep 2007
-Avram Grant: Sep 2007 mpaka Mei 2008
-Luiz Felipe Scolari: Jul 2008 mpaka Feb 2009
-Guus Hiddink: Feb 2009 mpaka Mei 2009
-Carlo Ancelotti: Jun 2009 mpaka Mei 2011
-Andre Villas-Boas: Jun 2011 mpaka Machi 2012
-Roberto Di Matteo: Machi 2012 mpaka Nov 2012
-Rafael Benitez: Nov 2012 mpaka Mei 2013
-Jose Mourinho: Juni 2013 -

Mourinho anarejea kwa mara nyingine Chelsea na kuwakuta tena baadhi ya Wachezaji aliokuwa nao mara ya kwanza kina Petr Cech, Ashley Cole, Frank Lampard, John Mikel Obi na John Terry pamoja na Michael Essien ambae alikuwa nae huko Real alikopelekwa kwa Mkopo na Chelsea.
Akizungumza kuhusu Mourinho, Mchezaji mkongwe wa Chelsea, Frank Lampard, alisema: “Ni Meneja Bora! Nimesema hili zaidi ya mara milioni, kiasi cha kuonekana kero kwa Watu, lakini nimebahatika kufanya nae kazi!”


ANZHI YALITAKA FACAFOOT KUTOMTUMIA SAMWEL ETO"O

KLABU ya soka ya Anzhi Makhachkala ya Urusi imeliandikia Shirikisho la Soka nchini Cameroon-Fecafoot kuwataka kutomtumia mshambualiaji nyota wa timu hiyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa ya nchi hiyo, Samuel Eto’o katika mechi zao ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2014. Daktari wa viungo wa klabu hiyo Stijn Vendenbroucke amesema nyota huyo aliumia msuli katika fainali ya Kombe Urusi Jumamosi iliyopita na alitaka apumzike kwa wiki chache kabla ya kurejea uwanjani tena. Eto’o atasafiri kuelekea Cameroon leo ili aweze kufanyiwa vipimo vingine na daktari wa timu ya taifa ambaye ndiye atakayetoa uamuzi wa mwisho wa kama nyota huyo atakuwa fiti kucheza mechi dhidi ya Togo Juni 9 na nyingine dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC wiki moja baadae. Cameroon kwasasa wanaongoza kundi I wakiwa na alama sita, alama moja zaidi ya Libya wakati DRC wana alama nne na Togoalama moja.

BRAZIL YALAZIMISHWA SARE YA 2-2 DHIDI YA ENGLAND KATIKA MECHI YA KIRAFIKI"

Katika Mechi ya ufunguzi rasmi Uwanja wa Maracana iliyopigwa jana  kati ya wenyeji brazil na England jina rasmi  la uwanja huo kwa sasa ni Estadio Jornalista Mário Filho huko Mjini Rio De Janeiro Wenyeji Brazil walilazimishwa  sare ya kufungana Bao 2-2 na England hapo jana Usiku.

Brazil walitawala Kipindi chote cha kwanza lakini hawakupata Bao hasa kutokana na kusimama imara kwa Kipa Joe Hart.

MAGOLI:

Brazil 2
-Fred Dakika ya 57
-Paulinho 82
-England 2
- Oxlade-Chamberlain Dakika ya 67
-Rooney 79
Bao zote 4 za Mechi hiyo ziliwekwa kimiani Kipindi cha Pili na Brazil ndio waliotangulia kufunga kupitia Fred lakini Alex Oxlade-Chamberlain alisawazisha Bao hilo.
mchezo huo ulikuwa ni wakati wa kukumbukwa sana  kutokana na Baba yake Mzazi Alex Oxlade-Chamberlain, Mark Chamberlain, aliekuwa Winga wa Stoke City, aliichezea England mara ya mwisho ilipocheza Maracana Mwaka 1984 na kuifunga Brazil Bao 2-0 katika Mechi ya Kirafiki.
England walikuwa kifua mbele kwa Bao 2-1 kwa Bao la Wayne Rooney kwa Shuti la Mita 25 huku zikiwa zimebaki Dakika 11 Mpira kwisha lakini Paulinho aliisawazishia Brazil Dakika 3 tu baadae.
MATOKEO MECHI NYINGINE ZA KIRAFIKI :
Lesotho 0 South Africa 2
Sudan 0 Tanzania 0
Algeria 2 Burkina Faso 0
Ireland 4 Georgia 0
Ukraine 0 Cameroon 0
United States 4 Germany 3