MENEJA wa zamani wa klabu ya Wigan Athletic, Roberto Martinez ameteuliwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Everton akichukua mikoba ilioachwa wazi na David Moyes aliyekwenda Manchester United. Martinez mwenye umri wa miaka 39 alifanikiwa kutwaa taji la Kombe la FA msimu huu, lakini aliomba kuondoka baada ya kuihakikishia timu hiyo nafasi ya kubakia katika Ligi Kuu nchini Uingereza. Mwenyekiti wa Wigan, Dave Whelan alimruhusu kocha huyo raia wa Hispania kuondoka na tayari wako katika mchakato wa kutafuta kocha mwingine wa kuziba pengo hilo. Martinez ambaye pia amewahi kuinoa Swansea City alijiunga na Wigan Juni mwaka 2009 na Aston Villa walitaka kumchukua mwaka 2011 lakini aliamua kubakia Wigan mpaka msimu huu alipoamua kuelekea Everton.
Thursday, June 6, 2013
Tuesday, June 4, 2013
PEREZ AWEKA WAZI KUWA RONALDO ATABAKI REAL MADRID"
Florentino Perez rais wa club ya Real
Madrid ametanabaisha kuwa ana mategemeo kuwa mshambuliaji nyota wa klabu
hiyo Cristiano Ronaldo atabakia Santiago Bernabeu katika kipindi chote
cha maisha yake ya soka. Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Ureno, mapema mwaka jana alidokeza kuwa hakuwa
anafurahia maisha ya Madrid na toka wakati huko amekuwa akihusishwa na
mpango wa kurejea Manchester United pamoja na Paris Saint-Germain-PSG. Lakini
Perez amedai kuwa atafanya kila awezalo ili nyota huyo aweze kuwa na
furaha katika klabu hiyo na kumalizika muda wake wa kucheza soka akiwa
hapo. Perez pia
aluzungumzia mustakabali ya mshambuliaji mwingine Gonzalo Higuain na
kudai kuwa hakuna yoyote aliyemwambia kwamba mchezaji huyo ataondoka
kwani klabu hiyo haijamuweka sokoni katika kipindi cha usajili. Ambapo
aliongeza kuwa kama mchezaji mwenyewe ndio anataka kuondoka basi klabu
itakayomhitaji itatakiwa kuwalipa lakini mpaka sasa ahkuna klabu yoyote
iliyojitokeza kumtaka mchezaji huyo.
KATIKA MISUKOSUKO YA HAPA NA PALE SASA ATUA COAST"
Baada ya kupata
misukosuko ya hapa na pale katika Club ya wekundu wa msimbazi SC kiungo Haruna
Moshi Shaaban ‘Boban hatimaye amefanikiwa kutua ndani ya jiji la tanga
kuichezea Coastal union mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara.
hivyo mpaka sasa
Coastal union imekamilisha usajili wa wachezaji wanne wapya, akiwemo mchezaji
bora wa Ligi Kuu ya Zanzibar msimu huu, Abdallah Othman Ally.
Ally anayecheza
upande wa pembeni juu kushoto mwenye speed na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira,
amesaini Mkataba wa miaka miwili na Coastal Union ambayo tangu ipande tena Ligi
Kuu mwaka juzi, imepania kurejesha makali yake. Mbali na Ally anayechezea pia
timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes.
Wagosi wa Kaya
wamemrejesha kiungo waliyemuibua mwaka 2000 kabla ya kufuata maslahi Moro
United, baadaye Simba SC na Geffle FF ya Sweden’.
Boban amerejea
Tanga alipoanzia kucheza soka ya ushindani mwaka 2000 chini ya kocha maarufu
zamani Mansour Magram, sasa marehemu akitokea sekondari ya Makongo, Dar es
Salaam.
Aidha wagosi hao
pia imesajili wachezaji wawili kutoka JKT Oljoro ya Arusha, kipa Said Lubawa na
sentahafu Marcus Ndehele ambapo Mwenyekiti wa Coastal Union Hemed Aurora
hmed akizungumza na mtandao huu ametanabaisha na kusema kuwa bado wanatazama
harakati za kuwanasa wachezaji watano zaidi kulingana na mapendekezo ya benchi
la ufundi.
Aidha Aurora
ameongeza na kusema kuwa huu ni usajili wa uliokuwa na malengo na si wa
kukurupuka na pia vilevile ni usajili unaotokana na mapendekezo ya benchi la ufundi
la timu chini ya kocha mkuu, Ahmed Morocco ambaye alitaka wachezaji tisa ambao
aliwapendekeza kwa majina yeye mwenyewe na sisi tumekuwa tukimfuata mmoja baada
ya mwingine na kumalizana naye.
Hivyo kwa wakati
huu bado tupo kwenye harakati za kumalizana na wengine watano ambpo Lengo letu
ni kuhakikisha kocha anakuwa na timu atakayoridhika nayo kulingana na
mapendekezo yake, hatutaki kuingilia kusajili hata mchezaji mmoja, alisema
Aurora.
Mbali na hilo
Aurora ameudokeza mtandao huu kuwa miongoni mwa wachezaji hao waliobaki mtazamo
zaidi ni kumnasa beki aliepatwa na misukosuko kama ya Boban yaani beki mwenye
nguvu na na uwezo wa kukaba Juma Nyoso.
Hata hivyo Aurora
ameongeza na kusema kuwa mazoezi ya Coastal Union yataanza wiki ya kwanza ya
mwezi Julai mwaka huu, nje kidogo ya mji ambako kikosi kitapiga kambi kujiandaa
kikamilifu kwa ajili ya msimu mpya.
MAN CITY YAMNASA WINGA WA SEVILLA JESUS NAVAS.
Club ya soka ya Manchester City wamefikia makubaliano na Klabu ya Spain Sevilla ya kumnunua Winga wa Kimataifa wa Spain Jesus Navas.
Navas, mwenye Miaka 27, anategemewa kununuliwa kwa gharama ya Pauni Milioni 17.
Navas yumo kwenye Kikosi cha Spain kitakachocheza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara huko Brazil kuanzia Juni 15.
Hadi sasa Man City haijatangaza nani
Meneja wao mpya baada ya kumtimua Roberto Mancini ingawa wengi
wanategemea Manuel Pellegrini, aliekuwa Malaga, ndio atachukua nafasi
hiyo.
NEYMAR ASEMA MESS ATAENDELEA KUTISHA ZAIDI DUNIANI.
MSHAMBULIAJI nyota mpya
wa klabu ya Barcelona, Neymar ametanabaisha anataka kumsadia nyota wa klabu
hiyo Lionel Messi aendelee kung’ara duniani baada ya kukamilisha
taratibu zote za uhamisho wake kutoka klabu ya Santos. Neymar
mwenye umri wa miaka alikamilisha uhamisho wake wenye thamani ya euro
million 57 na kumaliza utata wa miezi kadhaa juu ya mstakabali wa nyota
huyo. Akihojiwa
mara baada ya kutambulishwa rasmi mbele ya maelfu ya mashabiki katika
uwanja wa Camp Nou, Neymar amesema anataka kuisaidia timu kwasababu
Barcelona ni zaidi ya klabu na pia anataka kumsadia Messi aendelee
kung’ara zaidi. Nyota
huyo aliendelea kusema kuwa ilikuwa ni ndoto zake kucheza katika klabu
ambayo inahesabika kama mojawapo ya klabu bora duniani huku akizungukwa
na wachezaji nyota. Neymar
anaondoka Santos akiwa ameshinda Kombe la Brazil mwaka 2010, Kombe la
Klabu Bingwa ya Amerika Kusini mwaka 2011 huku akiwa amefunga mabao 138
katika mechi 229 alizocheza akiwa katika klabu hiyo.TAIFA STAR YATUA MORROCO RASMI KWA MAANDALIZI YA MECHI ITAKAYO PIGWA JUNE 8.
Taifa Stars imewasili hapa Marrakech, Morocco leo- Juni 3 mwaka huu tayari kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Morocco itakayochezwa Jumamosi- Juni 8 mwaka huu.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia hoteli ya Pullman ambayo pia Ivory Coast ilifikia ilipokuja kucheza hapa dhidi ya Morocco. Stars imetua na wachezaji 21 huku Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu waliokuwa Maputo, Msumbiji kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho na timu yao ya TP Mazembe watawasili kesho- Juni 4 mwaka huu saa 8 mchana.
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia hoteli ya Pullman ambayo pia Ivory Coast ilifikia ilipokuja kucheza hapa dhidi ya Morocco. Stars imetua na wachezaji 21 huku Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu waliokuwa Maputo, Msumbiji kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho na timu yao ya TP Mazembe watawasili kesho- Juni 4 mwaka huu saa 8 mchana.
Mechi kati ya Stars na Morocco itachezwa kuanzia saa 3 usiku kwa saa za hapa wakati nyumbani itakuwa ni saa 5 usiku.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Marrakech, Morocco
Monday, June 3, 2013
ALVES AMFAGILIA MSHAMBULIAJI MPYA WA TIMU HIYO NEYMAR
BEKI wa kimataifa wa Brazil na klabu ya Barcelona, Dani Alves amedai kuwa mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Neymar atang’ara na hatahitaji muda mrefu wa kuzoea mazingira mapya msimu ujao. Neymar mwenye umri wa miaka 21 anatarajia kuondoka klabu ya Santos kwenda Barcelona baada ya kukubalia kusaini mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo ambapo Alves anaamini nyota huyo atapata mafanikio akiwa Camp Nou. Alves amesema nyota huyo ana kipaji cha hali ya juu ndio maana Barcelona wakaamua kumsajili kutoka Santos na ni mategemeo yao atazoea mazingira ya Barcelona haraka kwasababu atakuwa akifanya kitu anachokipenda nacho ni kucheza soka. Neymar anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya na Barcelona leo kabla ya kumalizia taratibu za uhamisho wake.
Subscribe to:
Posts (Atom)



