
Hivyo kuwasili kwa mshambuliaji
wa Santos na timu ya taifa ya Hispania, Neymar,
katika kikosi cha Barcelona, inamaanisha kuwa Barcelona imeendelea kutumia
fedha nyingi kusaka mshambuliaji ambaye anaweza kung’ara vyema kwa pamoja na
staa wao, Lionel Messi.
Katika kipindi cha miaka
mitano iliyopita, Barcelona imetumia jumla ya Euro 205 milioni kwa ajili ya
kusaka mshambuliaji ambaye anaweza kumpunguzia Messi mzigo wa ustaa alioubeba
kwa muda mrefu klabuni hapo.
Thierry
Henry
Katika msimu wake wa
kwanza tu ndipo Henry alifikia matarajio ya mashabiki wa Barcelona. Baadaye
kuibuka kwa kinda wa Kihispaniola, Pedro Rodriguez, kulimfanya Henry apate
nafasi finyu ya kucheza katika kikosi cha kwanza na mwisho aliamua kutimkia
Marekani katika klabu ya New York Bulls.
Hata hivyo Henry
hakufikia kiwango alichokuwanacho wakati anachezea Arsenal chini ya Arsene
Wenger ingawa katika kipindi chake na Barcelona alishinda mataji kadhaa.
Zlatan
Ibrahimovich
Ukitazama hapa katika
hali ya kawaida kilikuwa kipindi kibaya katika harakati za maisha ya soka ya
Ibrahimovich. Tofauti na matarajio ya wengi, licha ya kusajiliwa kwa Euro 46
milioni huku pia Barcelona wakimtoa Samuel Eto’o kwenda Inter Milan, bado
Ibrahimovich hakutamba sana Nou Camp.
Mwishowe alijikuta
akiingia katika mgogoro mkubwa na kocha wa wakati huo, Pep Guardiola.
Ibrahimovich alimshutumu Guardiola kwamba alikuwa anampendelea zaidi Messi huku
wakati mwingine akimchezesha nafasi ya kati wakati yeye yuko benchi.
Baada ya msimu mmoja tu,
Zlatan aliondoka akarudi Italia ambako alijiunga na AC Milan.
David
Villa
Alionekana mmoja kati ya
wachezaji ambao wangeweza kumpunguzia mzigo wa mabao staa huyu wa Argentina.
Alianza vema, lakini baadaye aliumia katika michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia,
ilikuwa Desemba 2011.
Mbali na hilo tangu hapo
kasi yake imepungua uwanjani na sasa inasemekana ataondoka zake Barcelona
katika kipindi hiki cha uhamisho wa wachezaji.