Mwanariadha nyota wa Marekani, Tyson Gay amefanikiwa kufuzu kushiriki mbio za mita 200 za duniani zitakazofanyika jijini Moscow kwa kutumia muda wa sekunde 19.74 ambao ni muda wa haraka zaidi kwa mwaka huu. Gay ambaye ni bingwa wa dunia wa mwaka 2007, sasa atachuana na mwanariadha mwenye kasi zaidi duniani kutoka Jamaica, Usain Bolt katika mbio za mita 100 na 200 kwenye mashindano ya dunia yatakayofanyika jijini Moscow, Urusi Agosti mwaka huu. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka aliwashinda Isiah Young aliyeshika nafasi ya pili na Curtis Mitchell alishika nafasi ya tatu. Kwa upnde wa wanawake mwanadada nyota katika mbio fupi kutoka Marekani Allyson Felix alishindwa kutamba kwenye mbio za mita 200 baada kushindwa na Kimberlyn Duncan.
Monday, June 24, 2013
ARSHAVIN SASA AFIKIRIA KURUDI ALIPOTOKA KISOKA CLUB YA "ZSP"
SUAREZ AWEKA REKODI YA KUWA MCHEZAJI ALITUPIA MABAO MENGI NA TIMU YA TAIFA.
MSHAMBULIAJI Mahiri wa kimataifa wa Uruguay, Luis Suarez ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao waliibigiza Tahiti kwa mabao 8-1. Nyota anayekipiga katika klabu ya Liverpool ya Uingereza alifunga bao lake la 35 na 36 na kumpita mchezaji mwenzake wa nchi hiyo Diego Forlan wakati timu hiyo ilipokata tiketi ya kucheza nusu fainali dhidi ya wenyeji Brazil Jumatano huko Belo Horizonte. Mabao mengine ya Uruguay katika mchezo huo yalifungwa na Abel Hernandez aliyefunga manne huku Diego Perez na Nicolas Lodeiro wakifunga bao moja kila mmoja na kupelekea Tahiti chovu kuaga mashindano hayo na mzigo wa magoli 24 ya kufungwa. Uruguay ilitinga uwanjani bila kuwaanzisha nyota wake kama Forlan, Edinson Cavani na Suarez ambaye aliingia kipindi cha pili kwa ajili ya kuwapumzisha kwa ajili ya mchezo wa Jumatano.
FIFA YASEMA RAVSHAN AKIRI KUWAPA ITALY BAO LA PILI-KOMBE LA MABARA
SHIRIKISHO la Soka Dunia-FIFA limedai kuwa mwamuzi Ravshan Irmatov amekiri kuwapa Italia bao la pili kwa makosa wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya timu hiyo na Brazil ambao ndio wenyeji hao walitoa dozi ya mabao 4-2. Mabao hayo yalitiwa kimianina Giorgio Chiellini.
aidha bao hilo lilikubaliwa ingawa mwamuzi alishapuliza filimbi kuashiria penati kwenda kwa Italia kitendo ambacho kiliwaudhi wachezaji wa Brazil na kuzonga mwamuzi juu ya uwamuzi wake huo. FIFA imesema kuwa mwamuzi huyo wa Uzbekstan baadae alikiri kufanya kosa hilo na kukiri kupuliza filimbi kuashiria penati. Lakini pamoja na kukiri kutenda kosa kwa mwamuzi huyo FIFA hawajathibitisha kama watamrudisha nyumbani au ataendelea kuchezesha mechi za nusu fainali ya michuano hiyo.
JE?UNAMFAHAMU KWA UZURI DAVID SILVA KATIKA ULIMWENGU WA SOKA TAFAKARI ZAIDI".
DAVID SILVA
![]() | |||
Taarifa kuhusu yeye | |||
---|---|---|---|
Full name | David Josué Jiménez Silva | ||
Date of birth | 8 January 1986 (age 27) | ||
Place of birth | Arguineguín, Spain | ||
Height | 1.70 m (5 ft 7 in) | ||
Playing position | Attacking midfielder / Winger | ||
Taarifa kuhusu club | |||
Current club | Manchester City | ||
Number | 21 | ||
Timu za Ujana | |||
1995–2000 | UD San Fernando | ||
2000–2003 | Valencia | ||
Timu za Ukubwa | |||
Mwaka | Timu | Mechi | Goli |
2003–2004 | Valencia B | 14 | (1) |
2004–2010 | Valencia | 119 | (21) |
2004–2005 | Eibar (mkopo) | 35 | (4) |
2005–2006 | Celta Vigo (mkopo) | 34 | (4) |
2010– | Manchester City | 103 | (14) |
Timu ya Taifa | |||
2001–2002 | Spain U16 | 6 | (2) |
2002–2003 | Spain U17 | 20 | (5) |
2004–2005 | Spain U19 | 14 | (5) |
2005 | Spain U20 | 5 | (4) |
2004–2006 | Spain U21 | 9 | (7) |
2006– | Spain | 74 | (20) |
David Josué Jiménez Silva alizaliwa 8 Januari 1986 Arguineguín huko Las Palmas Hispain ni mchezaji mpira
mhispania ambaye kwa sasa anachezea timu ya Man city na timu ya taifa ya
Uhispania.Silva ana uwezo wa
kucheza upande wowote au kama namba 10 na
wakati mwingine kama mshambulizi msaidizi.Ni mchezaji mwenye mwili
mdogo, na mara nyingi hulinganishwa na Aimar Pablo, alipochukua nafasi yake
huko Valencia, akivalia nambari iliyohusishwa sana na Aimar; namba 21.
|
WASIFU WA KLABU
Silva alianza kucheza
mpira wa kulipwa msimu wa 2004-05 katika Ngazi ya pili katika timu ya SD Eibar,
akiwa amekopwa kutoka Valencia CF na alicheza mechi 35 katika daraja hilimna
kufunga mabao matano.Msimu uliofuatia, alikopwa tena, lakini wakati huu alikopwa
na timu ya Celta de Vigo, ambapo alicheza mechi 34, na kufunga mabao
manne.
Baada ya kucheza mechi
mbili ambazo aliingia uwanjani katika dakika za mwisho za mechi hizo, ambapo
mechi ya kwanza iliisha kwa Celta de Vigo kushinda 2-0 nyumbani dhidi ya Malaga
CF tarehe 28 Agosti 2005.
Silva akamaalizia msimu
huo kama mshambulizi bora huku timu hii ya Kigalisia ikifuzu katika kombe la
UEFA moja kwa moja kutoka daraja la pili.Katika misimu miwili, alikosa kucheza
mechi sita tu ilhali alifunga mabao 14 (bao la kwanza alilifunga tarehe 5
Novemba 2006 katika tasa ya 1-1 ugenini RCD Espanyol). Baada ya kutocheza kwa
muda wa miezi mitatu kutokana na jeraha la kisigino ambapo alifanyiwa upasuaji,
Silva alirejea kikosini
katikati mwa Desemba.Silva aliwakilishwa Uhispania akiwa na Cesc Fabregas mara
ya kwanza mwaka wa 2003 katika michezo ya ubingwa duniani ya FIFA ya wachezaji
wasiozidi umri wa miaka 17 huko Finland, ambapo alifunga mabao matatu.
Mwaka wa 2006, alijiunga
na timu ya Uhispania ya wachezaji wasiozidi umri wa 21 na alifunga mabao manne
katika kombe la vijana duniani la FIFA mwaka 2005; hii ilimwezesha kunyakua
nafasi ya 4 katika orodha ya wafungaji bora, pamoja na mshambulizi mwitaliano
Graziano Pellè.
WASIFU WA TIMU YA
TAIFA
Tarehe 22 Agosti 2007,
Silva aliifungia Uhispania mabao yake ya kwanza kikosini mwa Uhispania, na
alifunga mara mbili katika mechi hiyo ambapo waliishinda Ugiriki 3-2 katika
mechi ya kirafiki.
Baadaye aliitwa ajiunge
na kikosi cha wachezaji 23 ambao wangeiwakilisha nchi yao katika dimba la Euro
2008.
Katika nusu fainali Silva
alifunga bao la tatu la Uhispania dhidi ya Urusi baada ya ushambulizi wa haraka
ambayo Cesc Fabregas alimpigia krosi Silva, ambaye alitia mpira ndani ya lango
la Igor Akinfeev kwa kutumia mguu wake wa kushoto.
Katika fainali, Silva
alihusika katika tukio fulani na mjerumani Lukas Podolski. Baada ya kumvuta
Podolski chini, Podolski alimwenedea Silva na kuzua ubishi mkali ambao
haukuadhibiwa na mwamuzi.
Muda mfupi baadaye, kocha
wa timu ya Uhispania, Luis Aragonés, alimwondoa Silva na kuleta Santi Cazorla
ili kuzuia wezekano la vita.
NIGERIA YATUPWA NJE KATIKA MICHUANO YA KOMBE LA MABARA 3-0
Timu ya taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles ambao ni mabingwawa Afrika katika michuano ya CHAN imeondolewa kwenye michuano ya kombe la mabara baada ya kutandikwa mabao 3-0 na mabingwa wa dunia Hispania. Mabao mawili ya beki wa klabu ya Barcelona, Jordi Alba na moja la mshambuliaji wa Chelsea, Fernando Torres yalitosha kuisambaratisha Nigeria ambao wameshinda mechi moja pekee dhidi ya Tahiti wikiendi iliyopita. Nigeria wameyaaga mashindano hayo baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye kundi B wakiwa na pointi tatu nyuma ya Uruguay walioko kwenye nafasi ya pili wakiwa na point sita. Hispania ni vinara wa kundi B wakiwa wamemaliza hatua ya makundi na ushindi wa asilimia mia moja wakiwa na pointi tisa ambapo sasa watakwenda kuwavaa Italia katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo hapo siku ya siku ya alhamisi mjini Fortaleza. Uruguay wao wametoa kipigo cha magoli 8-0 kwa timu chovu kwenye michuano hiyo Tahiti ambao wameondoka na jumla ya magoli 24 ya kufungwa na kupata bao moja pekee walipocheza na Nigeria. Kwa matokeo hayo, Uruguay watacheza nusu fainali dhidi ya wenyeji Brazil, hapo siku ya jumatano.
MATOKEO
Uruguay 8
MATOKEO
Uruguay 8
*Abel Mathias Hernandez Dakika ya 2, 24, 45 & 67 [Penati]
*Diego Perez 27
*Nicolas Rodiero 62
*Luis Suarez 82 & 88
vs
Tahiti 0
>>>>>
Spain 3
vs
Nigeria 0
>>>>>
Nusu fainali
Jumanne Juni 26
Brazil v Uruguay
Muda saa 4 usiku
uwanja:Belo Horizonte
Jumatano Juni 27
Spain v Italy
uwanja Fortaleza
Muda saa 4 usiku
Mshindi wa tatu
Jumapili Juni 30
uwanja Salvador
Saa 1 usiku
Fainali
Jumapili Juni 30
Rio De Janeiro
Saturday, June 22, 2013
AFRICAN LYON YAJIPANGA KURUDI LIGI KUU TANZANIA BARA.
Mwanariadha nyota wa Marekani, Tyson Gay amefanikiwa kufuzu kushiriki mbio za mita 200 za duniani zitakazofanyika jijini Moscow kwa kutumia muda wa sekunde 19.74 ambao ni muda wa haraka zaidi kwa mwaka huu. Gay ambaye ni bingwa wa dunia wa mwaka 2007, sasa atachuana na mwanariadha mwenye kasi zaidi duniani kutoka Jamaica, Usain Bolt katika mbio za mita 100 na 200 kwenye mashindano ya dunia yatakayofanyika jijini Moscow, Urusi Agosti mwaka huu. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka aliwashinda Isiah Young aliyeshika nafasi ya pili na Curtis Mitchell alishika nafasi ya tatu. Kwa upnde wa wanawake mwanadada nyota katika mbio fupi kutoka Marekani Allyson Felix alishindwa kutamba kwenye mbio za mita 200 baada kushindwa na Kimberlyn Duncan.
Subscribe to:
Posts (Atom)